Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,708
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!.

Watanzania wengi wameshakata tamaa ya maisha na hii si kwa wasiyo nacho tu, bali hata kwa walionacho!.

Kila mtu anatafuta pesa kwa njia anayoifahamu yeye ilimradi tu kujijengea heshima kwa watu wake wa karibu na ukoo wake kutokana na dharau ambazo wamekuwa wakimuonyeshea.

Sasa kama mjuavyo ndugu zangu,mimi biashara yangu kubwa ni Bodaboda na jina langu ni kubwa sana hizi pande za Bunju ambapo mara nyingi ndipo kijiwe changu kilipo,sasa kuna mshikaji wangu mmoja ni Daktari hospitali fulani hapa mjini,jamaa mara zote huwa namchukuaga ile asubuhi mahali anapoishi na kumpeleka kazini kwake huko kwenye hiyo hospitali anayofanyia kazi,jamaa amekuwa zaidi ya rafiki kwasababu mambo kadhaa ambayo huwa anahitaji ushauri ananipigia simu namshauri kama brother.

Jamaa nadhani huwa hatumii JF kwasababu laiti kama angekuwa anatumia na akagundua mimi UMUGHAKA ninayembeba kila siku ndiye nilikuwa rafiki yake na Ally Mpemba tena nilikuwa napiga pesa kipindi fulani za mazonge mazonge,basi jamaa angenikomalia nimpeleke huko zenji au nimuunganishe na Ally kwa udi na uvumba.Kwakuwa hakufahamu chochote hivyo nikawa nimezikwepa bugudha zake.

Sasa haka ni kakisa kafupi ambako nasimulia ili kuwasanua wabongo waepukane na waganga wa kongo ambao wengi wao wamekuwa ni matapeli baada ya kuona watanzania wengi wanauhitaji wa kuwa matajiri.

Mwaka jana kati ya mwezi 8 - 11,jamaa yangu huyo au Bosi wangu huyo(Hapa nimuite Kamugisha)ingawa si jina lake halisi ili kuficha Identity yake,aliniambia mapema siku ya ijumaa nikiwa namtoa kazini kwake kwamba siku itakayofuatia yaani jumamosi tutafute mahali wanapochoma kitimoto angalau tule wakati huo tukipiga bia mbili tatu;Mi nilimwambia sitoweza kujumuika naye kwasababu kwanza Imani yangu hairuhusu mimi kula kitimonga,pili siku hiyo ya jumamosi ningekuwa kanisani nikimuabudu Mungu wangu.

Kamugisha "Ooh Mwanangu nisamehe sana nilikuwa nimesahau"

Aliendelea "Basi tufanye tu hata J'pili"

Mimi "Sawa bro hakuna tatizo ila mimi nitakula nyama choma ya kawaida tu,nguruwe situmii"

Kamugisha "Sawa mdogo wangu usijali,nathamini sana imani za watu wengine wala usiwe na shaka"


Kama nilivyosema,jamaa ni mshikaji ambaye tumefahamiana naye kwakuwa amekuwa mteja wangu,Pia amekuwa akinilipa pesa zangu kila mwisho wa mwezi ambazo ni Tsh 120000/=;Kwa maana kwamba kila siku ninapompeleka kazini kwake na kumfuata Jioni ni Tsh 4000/=,hivyo kwa mwezi ndiyo ananilipa kiasi hicho.

J'pili nilimcheki mshikaji akaniambia tuelekee mitaa ya river side pale Micasa lounge.


Mimi "Nichukue chombo yangu au tutapanda Daladala "

Kamugisha "Usijali mdogo wangu,leo ni wikiendi hivyo njia huwa ina mikosi ya walevi,pikipiki inaweza isiwe salama sana,nita-request Bolt"

Mimi "Sawa Bro"

Mimi "Tukutane wapi?"

Kamugisha "Nadhani tukutane hapo njia panda ya Goba"


Mimi ingawa nafanya kazi Bunju na ndipo kijiwe changu kilipo ila makazi yangu ni Mbezi - kwa Msuguri.Jamaa yeye anaishi Goba,hivyo ile asubuhi nikiwa natoka kituo cha kwanza ni kwake namchukua nampeleka kazini kwake kisha mimi naelekea kijiweni kwangu kama kawaida.

Kweli,hatimaye tulikutana jamaa aka-request Bolt tukaondoka zetu hadi Micasa Lounge,hili eneo kwangu haikuwa mara ya kwanza kufika kwasababu kuna abiria nishawapeleka hapo na kuwafuata pia,pia nikiwa ninapita mara kadhaa nikiwa kwenye mishemishe,nimekuwa nikiliona lilivochangamka.

Tulivyofika pale siku hiyo kulikuwa na live band ambayo ilikuwa inapiga kitu kama Karioke music na hiyo ilikuwa mida ya jioni saa 12 kuelekea saa 1 usiku.

Kila mmoja aliagiza kinywaji anachopiga akaletewa na muhudumu akaanza kupiga,jamaa Pombe ilipoanza kumuondolea aibu alianza kuongea bila uoga mambo ambayo nadhani ndiyo alitaka kuniambia.

Kamugisha "Mdogo wangu hivi huwa umeoa?"

Mimi "Ninaye mwanamke bro ila yeye yupo kikazi huko Moro"

Kamugisha "Sawa mdogo wangu,wewe nakupenda sana kama mdogo wangu kwakuwa ni mpambanaji sana na ninavyokuona utafika mbali sana"


Jamaa alipoaniambia nitafika mbali sana nikabaki namuangalia tu,angekuwa anajua huko mbali nilishafika kisha nikaamua kurudi tena nyuma wala asingeniambia hivyo bali nadhani angeshikwa na hasira sana kwanini niliamua kuacha mambo hayo.

Kamugisha "Mmebarikiwa watoto?"

Mimi "Nina mtoto mmoja tu kaka yupo na mama yake huko,huku huwa wanakuja wakati wa likizo tu"

Kamugisha "Ooh hongereni sana"

Aliendelea "Mimi kuishi na mwanamke nilishashindwa mdogo wangu,hivyo nikiona wewe una mwanamke napaswa kukupongeza sana"

Aliendelea "Wanawake ni manyang'au tu,mimi sasa hivi naangalia pesa tu,wanawake ndo kama hivi nikija sehemu kama hizi nikiwa na nyege nakamata li moja,naenda kulikung'uta mambo yanaisha kila mtu anaendelea na mishe zake".

Muda huo jamaa anaongea mimi natikisa kichwa tu kuonyesha tuko pamoja katika mazungumzo.

Kamugisha "Mdogo wangu mi ninataka hela tu kwa nguvu zote"

Mimi "Bora angalau wewe bro una ajira ya uhakika,sisi wengine tusipotoka hatuli"

Kamugisha "Ajira wapi mdogo wangu hizi kazi ni mateso tu,mshahara wenyewe ninaolipwa nikikwambia ni kituko cha karne"

Mimi "Bro mshahara ni mshahara tu,sisi wengine tusiyokuwa na mishahara ndiyo tunapata taabu"

Kamugisha "Mdogo wangu nalipwa milioni 1.2,hiyo hela nikikwambia kwa matumizi yangu na wategemezi kadhaa huwa nabaki na pesa ndogo sana"


Jamaa kile kitendo cha kuniambia analipwa milioni 1.2 halafu bado analia hana hela niliamaki kidogo kwasababu sisi wengine tunapambana kwa siku unapata hata elfu 10 unamshukuru Mungu.

Baada ya jamaa kuniambia vile,alizama kwenye mfuko wake wa jeans aliyokuwa amevaa akatoa simu yake kubwa aina ya I phone 12 kisha akaingia YouTube akanipatia na mimi nitazame,sasa nilikuwa nikiangalia YouTube kuna mshikaji mmoja alikuwa anaelezea namna alivyowahi kuwa tajiri kwa kwenda huko Congo na kupatiwa utajiri na mganga mmoja.

Kamugisha "Una muona huyo mshikaji?,jamaa amewahi kuwa tajiri mkubwa sana East Africa,kuna mshikaji niliongea nae akawa ameniambia hapo Congo kuna waganga hatari na hiyo kitu wanaitoa tena bure kabisa"

Mimi "Usiniambie kaka!"

Kamugisha "Kweli kabisa kwanini nikutanie!"


Jamaa wakati anaongea hakufahamu kabisa kwamba na mimi nimewahi kuwa na tuhela tudogo kwa kushikwa mkono na Ally Mpemba,nilitaka nimwambie lakini nikaamua kukausha tu.

Kamugisha "Nina taka siku moja niende kwa huyo mganga nasikia ni gwiji wa magwiji"

Aliendelea "Mdogo wangu haya siyo maisha,maisha ya kuendesha bodaboda na kupata hela ya kula tu siyo maisha kabisa,au wewe umeridhika nayo?"

Mimi "Bro nitafanye tena,ndo hivyo hivyo nasonga kibishi"

Kamugisha "Huwezi kujifariji kwa kusema unasonga kibishi mdogo wangu,tafuta hela uheshimike,dunia hii bila hela kwasasa hata kama uwe handsome vp bado utadhalaurika mdogo wangu,pesa ndiyo kila kitu"

Aliendelea "Mimi natafuta likizo halafu niende kwa huyo mtaalamu"

Kamugisha "Vp au mwenzangu hupendi hela nini!?"

Mimi "Kaka kuna mtu asiyependa hela?"

Kamugisha "Sasa mimi naona naongea peke yangu tu ndugu yangu na wewe huchangii chochote!"

Mimi "Bro napenda sana kuwa na pesa ila sasa hata ukisema niende huko kwasasa sina hela,labda mpaka nijipange"

Sikutaka kabisa hizo habari lakini niliamua kumtia moyo ili asijisikie vibaya,mimi nishapita huko na ninafahamu hali ilivyokuwa.

Kamugisha "Hela siyo tatizo dogo,wewe kama unataka tuungane twende niambie nitaomba likizo tusepe"

Mimi "Sawa kaka,kama ukinifadhiri nauli hakuna tatizo tutakwenda"

Kamugisha "Huo ndiyo uamuzi wa kiume dogo,hizi starehe zote ni hela,unaona watu walivyobaki mandinga hapo nje,hiyo yote ni hela bila hela utaonekana kibaka tu mbele ya watu wenye nazo hata kama unayoheshima"

Baada ya mazungumzo yale na vyombo kukolea kichwani kwa Kamugisha,jamaa aliamka akawa anacheza muziki bila aibu huku akimuita kila muhudumu wa kike aliyejipitisha mbele yake na kuanza kujichekesha chekesha bila sababu za msingi.



Naendelea................
 
SEHEMU YA PILI

Tuliendelea kukaa pale Micasa lounge hadi mida ya saa 4 usiku ndipo jamaa ali-request tena Bolt tukarudi zetu maskani.Mimi niliendelea kama kawaida kupambana na maisha yangu haya ya Bodaboda huku jukumu langu kila siku likiwa ni lilelile la kumpeleka Jamaa kazini kwake na kumfuata.

Baada ya wiki moja jamaa aliniambia yeye alikuwa ameomba likizo ya muda mfupi(Takribani wiki 3)na amekubaliwa hivyo akanitaka tufanye haraka twende na tuwahi kugeuka;Sasa kwakuwa jamaa utaratibu wote wa kuelekea Congo alikuwa nao,aliniomba majina yangu ili anitengenezee cheti cha chanjo ya Korona pamoja na cheti cha chanjo ya Homa ya manjano,vyeti vyote hivi jamaa alivitengeneza yeye mimi nikapewa tu bure!.

Kamugisha "Hivi huwa unapasipoti kweli?"

Mimi "Sina kaka"

Kamugisha "Jitahidi basi upate pasipoti maana hiyo ni muhimu sana"

Kiukweli nilidhani uenda jamaa angenipatia hela nikakate hiyo pasipoti ila nilivyoona amekausha ikabidi niende mwenyewe kuitafuta katika ofisi za wilaya ya Ubungo pale Luguruni.Mimi nilikuwa sitaki kabisa kuelekea huko Congo kwasababu niliona siku zote hizo nitakazokuwa huko ina maana sitoingiza chochote.Nia na madhumuni ya kwenda Congo ilikuwa kumuunga mkono jamaa ili asije akajisikia vibaya kwasababu tayari nishamkubalia tangu siku ile tumeenda pale Micasa,malengo yangu yalikuwa si kujipatia mali kwa njia ya waganga ila kama kweli yangekuwepo ningeyapokea kwa mikono miwili,pia nilikuwa nina kimuhe muhe cha kukanyaga Congo kwa mara ya kwanza kwasababu nimekuwa nikiisikia tu.

Kweli!,nilienda nikaipambania pasipoti ya muda nikawa nimeipata,nilipoipata tu nikamjulisha mshikaji kwamba nishaipata.

Kamugisha "Ok sawa,sasa nadhani leo ngoja nikakate tiketi ya gari halafu kesho tuondoke!"

Mimi "Sawa kaka hakuna tatizo"

Jamaa alienda akakata tiketi ya gari ijulikanayo kama MAJINJAH EXPRESS,Baada ya jamaa kuniambia tutapanda gari la MAJINJA nikafahamu kabisa tutakuwa tunapitia Sumbawanga,mimi nilikuwa najua uenda tulikuwa tunapitia Kigoma kumbe ni Sumbawanga,sasa sikutaka kabisa kumwambia kwamba huko Sumbawanga nishafika hadi huko Namanyere kwenye ishu za mihangaiko,nilijikausha kana kwamba ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza.

Asubuhi na mapema jamaa alinikuta mimi nishafika stendi ya Magufuli nikiwa nishaingia nimekaa ndani ya gari.Lile gari la Majinjah sitolisahau kwasababu lilikuwa ni tofauti na lile la mara ya kwanza wakati mimi naelekea Sumbawanga,Gari lile lilikuwa kana kwamba halioshwi kwasababu lilikuwa likinuka harufu fulani za mikojo,ukiacha hewa nzito yenye kiharufu fulani lakini pia kuwaona wadudu kama Mende na Kunguni lilikuwa jambo la kawaida.

Gari liling'oa nanga mida ya saa 12 asubuhi na ilipofika mida ya saa 2 usiku tulikuwa Mkoani Mbeya,kwakuwa jamaa alikuwa amekata tiketi ya moja kwa moja kutoka Dar to Sumbawanga tulivyofika pale Mbeya abiria wa Mbeya walitelemka kisha tukaendelea na safari.Tuliingia Tunduma mida ya Saa 4 Usiku,tulipofika Tunduma ile gari taa za mbele zikawa haziwaki vizuri,kuna mahali tulifika jamaa wakawa wamepaki gari kisha wakawa wanawasiliana na wenzao ili ikiwezekana waone namna nzuri ya kutufaulisha,jamaa waliwaambia hamna gari hivyo ni eidha atafutwe fundi wa umeme aje kutengeneza au ndiyo tuondoke hivyo hivyo kibishi.

Dereva na Konda walihangaika sana siku hiyo kuhusu fundi kwasababu mafundi wengi wa huko walikuwa wakipigiwa simu wanasema wamelala na wasingeweza kutoka usiku huo mpaka kesho ndiyo wangetusaidia.Hapa ndipo nikawadharau sana ndugu zangu watanzania,yaani muda wa saa 4 usiku unapigiwa simu uje upewe pesa nzuri wewe unasema umelala,tena walikuwa wanaongea kwa nyodo na dharau sana!,kibaya zaidi waliwapigia simu mafundi wawili kwa nyakati mbili tofauti lakini hakuna aliyekuja,nakumbuka Dereva alikuwa anawaambia watafuatwa popote walipo na Bodaboda na wakimaliza watarudishwa lakini jamaa wakagoma kabisa kukiachia kitanda.

Sasa dereva alipoona hakuna namna aliamua kuwasha chombo na kuondoka hivyo hivyo taa zikiwa haziwaki,sema uzuri ni kwamba yawezekana ile njia alikuwa ameiozoea,taa zilizokuwa zinawaka zilikuwa ni zile ndogo za parking,lakini taa kubwa ziligoma kabisa kuwaka,tulitembea mdogo mdogo na namshukuru Mungu tukafanikiwa kufika Sumbawanga mida ya saa 9 Usiku.

Tulipofika Sumbawanga tulitafuta Guest nzuri iliyokuwa jirani na Stendi kisha tukachukua vyumba kila mtu akaingia kulala,hata hivyo mimi sikulala kwasababu ni kama kulikuwa kumekucha tu!,nilijilaza nikawa nikama naiota ile safari namna ilivyokuwa ndefu na misukosuko ya hapa na pale.
Kulivyopambazuka jamaa alikuja kunigongea akaniambia nijiandae ili tuwahi kuondoka,Kwakuwa mimi tayari nilikuwa nimeshaoga na kujiandaa nilimwambia nilikuwa tayari.


Basi tuliondoka zetu kuelekea stendi ili tuelekee mahali ambapo jamaa yeye alikuwa ameelekezwa au kupewa ramani na mwenyeji wake.

Kamugisha "Nauli hadi Kirando ni shi ngapi?"

Konda "Ni elfu 10 boss"

Kamugisha "Ok nikatie tiketi mbili yangu naya jamaa hapa"

Baada ya kupewa tiketi tuliingia kwenye gari aina ya Tata lililokuwa la wastani kama Eicher,kisha lilipojaza tukaondoka zetu,gari iliondoka hapo stendi ya Sumbawanga mida ya saa 1:30 asubuhi na tukafika hapo Kirando mida ya 4 asubuhi.

Tulipofika pale Kirando jamaa aliniambia tuelekee eneo la bandari kulipokuwa na maboti ili tuone namna ya kupata usafiri wa kuelekea Congo ambapo alikuwa amepewa ramani na mwenyeji wake.Tulivyofika pale bandarini ilibidi tuulize utaratibu namna ulivyokuwa.

Kamugisha "Habari ya saa hizi mkuu"

Jamaa mmoja "Safi,habari ya kwako"

Kamugisha "Salama kabisa"

Aliendelea "Naomba kuuliza utaratibu wa boti hapa umekaa aje ?"

Jamaa "Boti za kwenda wapi?"

Kamugisha "Kuelekea Congo mkuu"

Jamaa "Congo ni kubwa,Congo sehemu gani?"

Kamugisha "Kuelekea Moba kaka"

Jamaa "Sasa hapa lazima muwe na vibali"

Kamugisha "Vibali tunavyo"

Jamaa "Ok sawa,sasa kuna jamaa mmoja anaitwa Seif,huyo ndiye anaye husika na mambo ya usafiri na maboti yote haya unayoyaona"

Kamugisha "Huyo Seif yuko wapi?"

Jamaa "Alikuwa hapa muda si mrefu sijui atakuwa ameelekea wapi ila nyie kaeni pale mumsubiri anakuja"

Tulisogea hadi mahali fulani ambapo kulikuwa na kituo cha mafuta ambacho kilikuwa hakitumiki tukakaa ili tumsubiri bwana Seif.



Inaendelea................
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom