Hussein Tuwa vs Eric Shigongo (Riwaya)

Tuwa ni mkali kuliko shigongo,namkubali sana yuko kwenye kiwango cha akina mtobwa,hammie rajabu,sama kitogo,na hata musiba.
 
Tuwa ni mkali kuliko shigongo,namkubali sana yuko kwenye kiwango cha akina mtobwa,hammie rajabu,sama kitogo,na hata musiba.
 
Dah jaman yan ulinganishe Shigongo na Hussein Tuwa au Amri Bawji duuh!!!!
 
H. Tuwa anaonekana anazingatia professionalism zaidi, hadithi yake ina mtiririko mzuri na scenario zake ni zinazoweza kutokea hata kwenye maisha ya kawaida.
Huyu Shiggy huwa anacheza zaidi na hisia za wasomaji, anatengeneza illusion ambazo kimsingi hazipo, kumbuka kuwa fasihi ni kioo cha jamii.
For that reason, me cast my vote for Hussein Tuwa.
 
Huyu jamaa ndo aliniafanya kipindi kile niwe nanunua gazeti la udaku la Kiu, time hizo linauzwa sh. 100
 
Wote ni wazuri na wanamapungufu yao kwa mfano shigongo amekosa ubunifu ana riwaya nyigi ila zote zinafanana na visa vyake unaweza tabiri kitakachotokea, tuwa anahadithi chache zinavutia sana ila hajaimudu lugha hana misemo ya kutosha pia anarudiarudia maneno. Pamoja na mapungufu hayo kura yangu nampa h.tuwa
 
Hussen Tuwa hadithi nyingine jamani, hebu tafuteni Mdunguaji au Mtuhumiwa haloo ni balaaa mwanzo mwisho
 
Kunfananisha Hussein Issa Tuwa na Shigongo aisee ni kumshushia hadhi Tuwa.
Tuwa mfananishe na Benny Mtobwa(RIP) au Elvis Musiba(RIP).
Tuwa anatisha.
 
Mi namkubali sana TUWA, nimesoma riwaya zake mbili tu ya MKIMBIZI na UTATA, aiseee jamaa anatisha kiukweli!
 
Kucompare watu maarufu si kitu kibaya, mara nyingi ni kuangalia mazuri na kuyaendeleza na yale mapungufu kuyarekebisha.

Kwenye suala la hadithi(riwaya) za magazetini, mimi nilijitahidi sana kufuatilia hadithi za Eric Shigongo(Ijumaa) na hadithi mbili tu za Hussein Hassan Tuwa(Mtuhumiwa na Mkimbizi).

Kwa maoni yangu, hadithi za Mr. Tuwa zilikuwa zina msisimko zaidi. Zilikuwa zinakupa nafasi ya muhusika kuwa kama ndiye uliyeko kwenye hadithi. Ilikuwa unapata picha kabisa.

Kwa maoni yangu naona Hussein Hassan Tuwa ni mtunzi mahiri na hodari kuliko Eric Shigongo.

Constructive comparison please!!

View attachment 66403

CHAI CHUNGU hana mpinzani!!
 
Hussein Tuwa huwezi kumfananisha na Shigongo,jamaa mkali sana,he is the best!
sijawahi kusoma za Tuwa, lakini nilisoma Shigongo - Rais anampenda mke wangu- mwisho wa siku niliboreka nikakiachilia mbali huku mwanzo aliaanza vizuri lakini hapo katikati akatoka kwenye mtiririko kama wanavyosema watu hafanyi utafiti.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom