Hussein Tuwa vs Eric Shigongo (Riwaya)

Tigga Mumba

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
746
473
Kucompare watu maarufu si kitu kibaya, mara nyingi ni kuangalia mazuri na kuyaendeleza na yale mapungufu kuyarekebisha.

Kwenye suala la hadithi(riwaya) za magazetini, mimi nilijitahidi sana kufuatilia hadithi za Eric Shigongo(Ijumaa) na hadithi mbili tu za Hussein Hassan Tuwa(Mtuhumiwa na Mkimbizi).

Kwa maoni yangu, hadithi za Mr. Tuwa zilikuwa zina msisimko zaidi. Zilikuwa zinakupa nafasi ya muhusika kuwa kama ndiye uliyeko kwenye hadithi. Ilikuwa unapata picha kabisa.

Kwa maoni yangu naona Hussein Hassan Tuwa ni mtunzi mahiri na hodari kuliko Eric Shigongo.

Constructive comparison please!!

books.jpg
 
Kwa hili jukwaa kazi yake imekuwa ni kupambanisha nani zaidi?

Naukishajua nani zaidi inatusaidia nini?

Wote wachovu tu hawana jipya!
 
Kwa hiyo hili jukwaa kazi yake imekuwa ni kupambanisha nani zaidi?

Naukishajua nani zaidi inatusaidia nini?

Wote wachovu tu hawana jipya!
 
Hussein tuwa ni best aisee
bahati mbaya sana sijazisoma hizi unazozisemea za mtuhumiwa na mkimbizi ila mwaka 2004-2005 nilisoma hadithi zake mbili znaitwa
utata wa 9/12
na mdunguaji

yaani nashindwa hata kuzielezea ni balaa shigongo hamna kitu
 
well hata mimi nimesoma hadithi mbili tu za Tuwa lakini nyingi sana za Shigongo. Mara ya mwisho kusoma hadithi hizo ilikuwa 2002, za shigongo ninazozikumbuka kama 'escape from rwanda', 'before i die the world should forgive me' na moja ya yule bibi aliyekuwa na uwezo wa kuongoza jeshi la wanyama na wadudu, ile novel yake ya kwanza, hiyo ya 'rais anampenda mke wangu sikuimalizia, kuna ile ya yule msichana mwenye mzimu wa lutego, kuna ya yule dogo aliyekuwa na akili akawa anagombaniwa na marekani na tz, kuna ya kolo na yule binti wa balozi, na nyinginezo nyingi.

Shigongo alikuwa(nadhani bado) anaandika hadithi nyingi sana katika magazeti yake(nafikiri kila siku ya wiki ana gazeti) kwa hiyo kufuatilia si jambo rahisi.

Kingine sisi Waswahili hatupendi kusoma vitabu/riwaya yaani ni wavivu mno. Kama Shigongo angeweza kuchapisha riwaya moja USA or UK angefika mbali sana kwani naona anawazidi kiuwezo wakina Rene Bravan Robinson(James H Chase), Sydney Sheldon, John Grisham, Jeanne Rowling, Danielle Steel, Jilly Cooper, Dan Brown. Kwani yeye novel zake haziko typecast sio za aina moja kwani kwa Sydney Sheldon mara nyingi kunakuwa na mwanamke ambaye anakuwa na nguvu sana, hapo hapo anakuwepo mwanaume ambaye yuko naye karibu ingawa ana malengo mabaya naye na mwisho wa novel mwanamke yule anaanguka au kushindwa katika jambo fulani, ingawa baadhi ya novel ziko tofauti na muundo huu kama 'are you afraid of the dark','the other side of me' na 'nothing last forever'. John Grisham novel zake zote ni zinahusiana na sheria zaidi. JK Rowling ni Harry Potter pekee(magic).

Shigongo ana kipaji cha kuelezea(story telling) lakini sidhani kama huwa anafanya utafiti wowote kabla ya kuandika novel yake. Kama angeweza angekuwa anafanya utafiti hata mwaka mzima kabla ya kuandika novel yoyote hizo za magazetini aachie watu wengine watumie jina lake kama pen name, yeye aandike moja ikiwezekana kwa kiingereza atafute publishers wa UK or USA. Kama atatengeneza jina ataweza kufikia mbali sio kukaa kugombana na kina chameleon.

Binafsi niliacha kusoma hadithi zake kwa sababu hazikuwa na quality kama zile za bestsellers wa nje, halafu alikuwa hatoi novel ya pamoja mpaka ukasome gazeti sasa unakuta j3-Ijumaa kila siku hadithi tofauti tofauti ufaitiliaji unakuwa mgumu.

Kwa upande wa Tuwa anajua sana storytelling bila haja ya kutaja vitu vigumu vigumu au sehemu za nje ya nchi, lakini ameandika hadithi chache kushindanisha na shigongo kwa hiyo labda alibahatisha au amekosa platform ya kuonesha kazi zake. Kwa hiyo kwa upande mmoja naona si sahihi kumlinganisa Tuwa na Shigongo ni kama vile kumlinganisha Dean Ashton na Wayne Rooney
 
Shigongo ni sio muandishi bali ni mkalimani anayecopy kazi za watu na kutafsiri kwa kiswahili kisha huweka jina lake kama yeye ndo kaandika riwaya hiyo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Me namjua Shigongo,huyo mwingine simjui.Nachojua mimi ni kwamba Shigongo ni mtunzi mahiri wa hadithi kuliko wote niliowahi kuwajua bongo
 
mimi nimesoma hadth zao wte, ukianza na shigongo hadith zake naamini huwa hafnyi utaft anatnga tu hadth but Tuwa that guy is genius kama kwenye futbal utasma mesi, csemi uongo niliacha stry za shgngo baada ya kuanza ksma za tuwa nakumbka mhska m1 alkua jon doe, ni mkali sana wa hadth siku hz anatoa vya shule sec "mfadhl" huyu jamaa anapatkana wapi?
 
sikubaliani na pianist kwamba tuwa ametnga hdth chche pngne amebahatisha, kwnza hadth c chche
1. mtuhumiwa
2. utata 9/12
3. mdunguaji
4. mkimbz
5. mfadhl
hz ni ambzo mi nimesma na zote ni kali kwa hyo huwez sma amebhatsha. mi binafs kwa tz hpa na hdth nilzsma nathbtu kusema hana mpinzani
 
kama wewe ni msomaji wa riwaya...huwezi kuwafanananisha watu hao wawili hata kidogo,
husein Tuwa naweza kumfananisha kidogo na Beka mfaume kidogo lakini hamfikii,
shigongo anaandika tu,hana ethics,knoweledge,hafanyi research na hadithi zake nyingi
hazina mashiko ni hadithi za kusomwa na wapuuzi.....Tuwa anajitahidi kidogo
 
yani Hussein Tuwa ni mkalii alinifanya niache kusoma hadithi za shigongo.
Soma Mkimbizi, Mtuhumiwa na utata yani ni noma jamaa anajua sana sana.
Hivi willy Gamba aliishia wapi??
 
hussein Tuwa ni mkali, hadithi zake zimetulia na ametumia akili, shigongo hana jipya hadithi zake zote zinafanana, hazihamasishi kusoma, na ukianza kusoma tu unapredict itakuaje maana matukio yafanana
 
Nikiwakumbuka character wa husein tuwa kuna Jadu Mfaume, kwenye utata wa 9/12
Swordfish, blackmamba, stealth kwenye Mdunguaji
Halafu kipindi hiko Hussei Tuwa alikuwa ameshinda Tuzo ya Africa ya uandishi wa Riwaya kama sikosei...
Sasa sijui shigongo ana tuzo hata za bakita?? Nauliza....
 
Nikiwakumbuka character wa husein tuwa kuna Jadu Mfaume, kwenye utata wa 9/12
Swordfish, blackmamba, stealth kwenye Mdunguaji
Halafu kipindi hiko Hussei Tuwa alikuwa ameshinda Tuzo ya Africa ya uandishi wa Riwaya kama sikosei...
Sasa sijui shigongo ana tuzo hata za bakita?? Nauliza....


really!!!? wabarikiwe waliotambua kazi ya ajabu ya huyu jamaa wakamtuza!kumfananisha na shigongo ni matusi kwa waandishi mahiri na wapenzi wa kweli wa riwaya!He is simply the best,this Tuwa dude!
 
''mkimbizi'' ilinifanya niwe mkimbizi tu muda wote hadi namaliza kuisoma aisee!halafu nikasoma 'sniper''...my my my ....the illest writer wa kizazi chake,ofkoz kuacha wale wazee ambao nakumbuka kazi zao with nostalgia(nyakati zinakwenda haraka sana aisee) kama mzee Musiba,Benny M,Hammie yule mama, na wanafasihi wote wakongwe wa kitanzania!
 
Wewe kujiita "TIGGA MUMBA" tayari inaonyesha nani unamkubali.

Wamfahamu JADU MFAUME? Nimekukumbusha ee?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom