Hussein Tuwa vs Eric Shigongo (Riwaya)

Hussein Tuwa vs Eric Shigongo (Riwaya)

Kucompare watu maarufu si kitu kibaya, mara nyingi ni kuangalia mazuri na kuyaendeleza na yale mapungufu kuyarekebisha.

Kwenye suala la hadithi(riwaya) za magazetini, mimi nilijitahidi sana kufuatilia hadithi za Eric Shigongo(Ijumaa) na hadithi mbili tu za Hussein Hassan Tuwa(Mtuhumiwa na Mkimbizi).

Kwa maoni yangu, hadithi za Mr. Tuwa zilikuwa zina msisimko zaidi. Zilikuwa zinakupa nafasi ya muhusika kuwa kama ndiye uliyeko kwenye hadithi. Ilikuwa unapata picha kabisa.

Kwa maoni yangu naona Hussein Hassan Tuwa ni mtunzi mahiri na hodari kuliko Eric Shigongo.

Constructive comparison please!!

View attachment 66403

Naomba ukasome "No Orchid for Miss Blandish"ya J.H.Chase,halafu rudi kwa "Mkimbizi" ya H.Tuwa na rejea maelezo(ushabiki?) wako.
 
Wanaotaka kusoma hadithi za hussein tuwa. nenda ka-like ukurasa unaitwa "kona ya riwaya reloaded" hukoo facebook. Mpaka sasa hivi ameandika hadithi 2.
- mtafiti
- miss tanzania.... ambayo inaendelea sasa hivi.
 
Hussein Tuwa ni mtunzi mahiri sana! Ametunga hadith chache na zina msisimko wa ajab...


Shigongo ni mtunzi mzuri pia, tatizo hadith zake zinafanana sanaaa na zina usuper man sana (hazina uhalisia)
 
Wakati najifunza kusoma riwaya miaka ya 80 mwishoni ,nilisoma nyingi za kiswahili,na nilifurahi.90's nilianza kusoma za kiingereza nikapata tofauti kubwa.Hasa za J.H.Chase.Changanya zote ili upate ladha tofauti.
 
Shigongo ni sio muandishi bali ni mkalimani anayecopy kazi za watu na kutafsiri kwa kiswahili kisha huweka jina lake kama yeye ndo kaandika riwaya hiyo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

una uhakika?tafuta novel hata 1 dunian ambayo ameikop coz alishatangaza dau,the guy z talented jaman
 
Shigongo ni sio muandishi bali ni mkalimani anayecopy kazi za watu na kutafsiri kwa kiswahili kisha huweka jina lake kama yeye ndo kaandika riwaya hiyo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

thibitisha kauli ako kwa mfano wa hadith ake ambayo amecopy
 
Naomba ukasome "No Orchid for Miss Blandish"ya J.H.Chase,halafu rudi kwa "Mkimbizi" ya H.Tuwa na rejea maelezo(ushabiki?) wako.

Chase si wa kumfananisha na Tuwa,ni disrespecf kwa James Hadley Chase.But between Tuwa ns Shigongi i agree riwaya za Tuwa zina msisimko mno.
 
Nikikumbuka ile riwaya ya utata duuuh, mh. Tuwa namnyoshea mikono asee
 
hivi ukitaka vitabu vya riwaya vya husen tuwa utavipata wapi?
 
Shigongo ndo habar ya mjini. fatilia hata mauzo ya vitabu vyake utagundua jamaa anauza sana
 
dharau hizo Tuwa kumfananisha na Shigongo .Tuwa yuko juu!
 
Me namjua Shigongo,huyo mwingine simjui.Nachojua mimi ni kwamba Shigongo ni mtunzi mahiri wa hadithi kuliko wote niliowahi kuwajua bongo

Umenifurahisha sana yaani hujui watunzi wengine lakini unasema shigongo ndio best
 
well hata mimi nimesoma hadithi mbili tu za Tuwa lakini nyingi sana za Shigongo. Mara ya mwisho kusoma hadithi hizo ilikuwa 2002, za shigongo ninazozikumbuka kama 'escape from rwanda', 'before i die the world should forgive me' na moja ya yule bibi aliyekuwa na uwezo wa kuongoza jeshi la wanyama na wadudu, ile novel yake ya kwanza, hiyo ya 'rais anampenda mke wangu sikuimalizia, kuna ile ya yule msichana mwenye mzimu wa lutego, kuna ya yule dogo aliyekuwa na akili akawa anagombaniwa na marekani na tz, kuna ya kolo na yule binti wa balozi, na nyinginezo nyingi.

Shigongo alikuwa(nadhani bado) anaandika hadithi nyingi sana katika magazeti yake(nafikiri kila siku ya wiki ana gazeti) kwa hiyo kufuatilia si jambo rahisi.

Kingine sisi Waswahili hatupendi kusoma vitabu/riwaya yaani ni wavivu mno. Kama Shigongo angeweza kuchapisha riwaya moja USA or UK angefika mbali sana kwani naona anawazidi kiuwezo wakina Rene Bravan Robinson(James H Chase), Sydney Sheldon, John Grisham, Jeanne Rowling, Danielle Steel, Jilly Cooper, Dan Brown. Kwani yeye novel zake haziko typecast sio za aina moja kwani kwa Sydney Sheldon mara nyingi kunakuwa na mwanamke ambaye anakuwa na nguvu sana, hapo hapo anakuwepo mwanaume ambaye yuko naye karibu ingawa ana malengo mabaya naye na mwisho wa novel mwanamke yule anaanguka au kushindwa katika jambo fulani, ingawa baadhi ya novel ziko tofauti na muundo huu kama 'are you afraid of the dark','the other side of me' na 'nothing last forever'. John Grisham novel zake zote ni zinahusiana na sheria zaidi. JK Rowling ni Harry Potter pekee(magic).

Shigongo ana kipaji cha kuelezea(story telling) lakini sidhani kama huwa anafanya utafiti wowote kabla ya kuandika novel yake. Kama angeweza angekuwa anafanya utafiti hata mwaka mzima kabla ya kuandika novel yoyote hizo za magazetini aachie watu wengine watumie jina lake kama pen name, yeye aandike moja ikiwezekana kwa kiingereza atafute publishers wa UK or USA. Kama atatengeneza jina ataweza kufikia mbali sio kukaa kugombana na kina chameleon.

Binafsi niliacha kusoma hadithi zake kwa sababu hazikuwa na quality kama zile za bestsellers wa nje, halafu alikuwa hatoi novel ya pamoja mpaka ukasome gazeti sasa unakuta j3-Ijumaa kila siku hadithi tofauti tofauti ufaitiliaji unakuwa mgumu.

Kwa upande wa Tuwa anajua sana storytelling bila haja ya kutaja vitu vigumu vigumu au sehemu za nje ya nchi, lakini ameandika hadithi chache kushindanisha na shigongo kwa hiyo labda alibahatisha au amekosa platform ya kuonesha kazi zake. Kwa hiyo kwa upande mmoja naona si sahihi kumlinganisa Tuwa na Shigongo ni kama vile kumlinganisha Dean Ashton na Wayne Rooney

Unakosea sana kusema Tuwa alibahatisha,hii inatokana na kuwa labda hujafuatilia sana riwaya zake.

Jamaa sio mmiliki wa gazeti lolote so huwa anatoa kwenye gazeti la kiu kwa kupokezana either na Beka Mfaume au Amri Bhawji.

Mfano wa riwaya ambazo nimezisoma za Tuwa ni
1.Mkimbizi
2.Mtuhumiwa
3.Utata wa 9/12
4.Mdunguaji
5.Bondia
6.Mfadhili (tena hiki kitabu kilichukua hadi tuzo ya MacMillan na kikawa kinatumika mashuleni kwa wale wa wanaosoma Kiswahili advance)

Nimesoma hadithi za Shigongo nyiingi saana ila uwezo wa Hussein Issa Tuwa upo juu sana.Tafuta kitabu chake hata kimoja nakuhakikishia hutojuta na nnauhakika utajiunga katika chama cha Tuwa ktk riwaya

Ahsante.
 
Hadithi za Hussein Tuwa kwa kweli zinamsisimko ukiwa unazisoma mfano ile ya Miss Tanzania au Mkimbizi ukisoma hadi unapata mdadi..
 
Me namjua Shigongo,huyo mwingine simjui.Nachojua mimi ni kwamba Shigongo ni mtunzi mahiri wa hadithi kuliko wote niliowahi kuwajua bongo

Ulishahi kusoma hadithi za Musiba, kama sanda ya jambazi, kikomo no 1 na no 2 na vingine vingi alivokua akitunga kabla ya kuzuiwa na serikali, ama wewe ni kizazi kipya?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom