Rais Samia ampokea Rais wa Hungary, Katalin Novak katika Ikulu ya Dar es Salaam, leo Julai 18, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Rais wa Hungary, Katalin Novak katika Ikulu ya Dar es Salaam, leo Julai 18, 2023.

Rais Katalin Novak yupo katika ziara ya siku nne Nchini Tanzania kuanzia Julai 17 hadi Julai 20, 2023, updates ya kinachoendelea Ikulu ya Magogoni itafuata muda si mrefu.

Baada ya kuwasili Rais Novák anatarajia kupokelewa na mwenyeji wake Rais Samia na kufanya mazungumzo rasmi na baadae viongozi hao kuzungumza na Waandishi wa Habari.

Hungary.jpg

===

Dondoo za uhusiano wa Tanzania na Hungary
-
Kozi ambazo Hungary imekuwa ikifadhili kwa Watanzania ni kozi za kimkakati ikiwemo Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.

- Rais Novák aliingia madarakani 10 Mei, 2022 na ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Urais nchini Hungary.

- Malengo mahsusi ya ziara ya Rais Novák nchini Tanzania ni kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi hizo mbili.

- Matukio ya kisiasa na kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 90 yalisababisha kupungua shughuli zao (Hungary) barani Afrika ikiwemo Tanzania.

- Kwa miaka mingi msaada wa kiufundi wa Hungary kwa Tanzania umekuwa ukilenga sekta ya Elimu hususan ufadhili wa masomo kwa Watanzania kwenda Hungary.

- Watanzania wamenufaika na ufadhili wa masomo katika Vyuo Vikuu vya Hungary kwenye fani za shahada ya kwanza, shahada za uzamili na shahada za uzamivu.

- Kozi ambazo Hungary imekuwa ikifadhili kwa Watanzania ni kozi za kimkakati ikiwemo Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.

Rais Samia Suluhu Hassan akimpokea Rais wa Jamhuri ya Hungary, Katalin Novàk, Ikulu Jijini Dar es Salaam
5cfc767d-c952-4cd7-bd79-f3eddd1e37a7.jpg

62182dc4-4dd1-42d7-a388-c8ccbfc34a9f.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na mgeni wake Rais wa Hungary, Katalin Novák mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 18 Julai, 2023.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anazungumza:
Nchi yetu imetengeneza historia ya viongozi wawili wajuu Wanawake kukutana Ikulu ya Dar es Salaam, nakukaribisha sana Rais wa Hungary, Katalin Novak, umekuwa ni wakati mzuri kuwa nawe hapa.

Tumejadili mambo mbalimbali kuhusu Nchi zetu, tumebadilishana mawazo jinsi ya kuboresha uhusiano.

Jambo zuri ni kuwa Hungary imeonesha nia ya kuendeleza ushirikiano na Nchi za Afrika.

Tumekubaliana kuboresha uhusiano wetu kwa Kidiplomasia katika ya Tanzania na Hungary, fursa hiyo itaendeleza uhusiano mzuri uliopo.

Kuna nafasi ya kuboresha fursa za kibiashara pia kati ya Nchi zetu. Tumejadiliana jinsi ya kuhamasisha uwekezaji katika nchi mbili kama vile katika madini, viwanda na biashara nyinginezo.

Kuhusu elimu, Hungary imekuwa na mchango mkubwa hasa katika elimu ya juu, kuna program mbalimbali zilizohusisha Wanafunzi wa Tanzania kwenda kusoma Hungary.

Katika makubaliano yetu kuna wanafunzi ambao watapata nafasi ya kuja kusoma Tanzania, tutaanza na wanafunzi watano kutoka Hungary kuja kusoma Tanzania wakati Hungary wao watachukua wanafunzi 30 kutoka Tanzania.

Mwaka 2022 Tanzania imepokea watalii zaidi ya 7,000 kutoka Hungary ambao ni wengi kulinganisha na Watalii kutoka Taifa hilo waliowahi kuja hapa nchini.

Kuhusu haki za kijinsia na kuwawezesha Wanawake ni moja ya ajenda ambazo zinapewa umuhimu mkubwa katika Serikali yangu, tumekubaliana kuendelea kuziweka juu ajenda hizo kwa Nchi zote mbili.

Naamini ziara hii itatengeneza uhusiano wa karibu zaidi baina ya nchi hizi mbili. Nachukua nafasi hii kukukaribisha wakati mwingine wowote.

331f8fd7-b25d-4e75-8d59-4718c40c1946.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Hungary, Katalin Novák wakati wakiangalia ngoma za asili mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Julai, 2023.
fe9209dd-35cd-4c2a-8e97-3b0aad601db5.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Hungary, Katalin Novák mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Julai, 2023.
Rais wa Hungary, Katalin Novak anazungumza:
Mkutano huu una umuhimu mkubwa kwanza kwa kuwa unwakutanisha Marais Wanawake.

Hii inatupa nafasi ya kuwaamasisha Wanawake wengine na wasichana wadogo kufanya vile ambavyo vinaweza kuwea na faida katika maisha yao.

Hawatakiwi kukata tamaa, iwe ni katika maisha ya kuwa mama au maisha ya kikazi.

Nchi yetu siyo kubwa, tumekuja Tanzania kwa kuwa tunahitaji kuwafahamu na kujifunza mambo mengi.

Tunathamini heshima ambayo ipo kati yetu, ushirikiano na urafiki wetu.

Tumepokea wakimbizi zaidi ya Milioni 2 kutokana na vita ya Ukraine, pia tumekutana na wakati mgumu kutokana na hali ya uchumi inayoendelea.

Hatukuwa na muda wa kuzungumza historia yetu, tumezungumza kuhusu changamoto, uzoefu na jinsi ya kupata utatuzi, nashukuru sana Rais Samia kwa mazungumzo yetu.

Moja kati ya hoja zetu ni suala la Elimu, elimu ni ndio ufunguo wa maisha yajayo, sio tu Tanzania bali hata Hungary na kwingine Duniani.

Kuna wanafunzi zaidi ya elfu mbili ambao wanasoma Hungary kupitia scholarship inayosimamiwa na Serikali ya Hungary.

Kuanzia leo pia kutakuwa na wanafunzi wa Hungary ambao watapata scholarship kutoka Serikali ya Tanzania.

Mawazo yetu ni kutengeneza fursa ya kujifunza kwa pande zote mbili, nashukuru sana Rais Samia kwa kutoa fursa ya scholarship kwa Wanafunzi wa Hungary.

Tumezungumzia kuhusu uchumi wa mataifa yetu, tunapenda kuendeleza uhusiano uliopo baina ya mataifa yetu.

Mwakani tunatarajia kuandaa kongamano la kibiashara ili tuweze kuangalia maeneo ya kuweza kufanya uwekezaji kwa ajili ya siku zijazo.

Namkaribisha Rais Samia katika kikao ambacho kitahusisha viongozi wanawake kitakachofanyika mwakani.

Nashukuru sana na ninaamini tutaendelea na ushirikiano, nashukuru sana.
af0715a6-9cde-48ae-bfdb-df04fbfd4e6e.jpg

788b5687-40a9-4541-a304-89dd326faedc.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mazungumzo Rasmi na Ujumbe wa Hungary ulioongozwa na Rais wa Nchi hiyo, Katalin Novák, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Julai, 2023.
 
View attachment 2691733

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Rais wa Hungary, Katalin Novak katika Ikulu ya Dar es Salaam, leo Julai 18, 2023.

Rais Katalin Novak yupo katika ziara ya siku tatu Nchini Tanzania, updates ya kinachoendelea Ikulu ya Magogoni itafuata muda si mrefu…
Amekuja kufanya utalii au anahitaji msaada wa kijeshi??
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Rais wa Hungary, Katalin Novak katika Ikulu ya Dar es Salaam, leo Julai 18, 2023.

Rais Katalin Novak yupo katika ziara ya siku tatu Nchini Tanzania, updates ya kinachoendelea Ikulu ya Magogoni itafuata muda si mrefu…

Dondoo za uhusiano wa Tanzania na Hungary
-
Kozi ambazo Hungary imekuwa ikifadhili kwa Watanzania ni kozi za kimkakati ikiwemo Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.

- Rais Novák aliingia madarakani 10 Mei, 2022 na ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Urais nchini Hungary.

- Malengo mahsusi ya ziara ya Rais Novák nchini Tanzania ni kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi hizo mbili.

- Matukio ya kisiasa na kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 90 yalisababisha kupungua shughuli zao (Hungary) barani Afrika ikiwemo Tanzania.

- Kwa miaka mingi msaada wa kiufundi wa Hungary kwa Tanzania umekuwa ukilenga sekta ya Elimu hususan ufadhili wa masomo kwa Watanzania kwenda Hungary.

- Watanzania wamenufaika na ufadhili wa masomo katika Vyuo Vikuu vya Hungary kwenye fani za shahada ya kwanza, shahada za uzamili na shahada za uzamivu.

- Kozi ambazo Hungary imekuwa ikifadhili kwa Watanzania ni kozi za kimkakati ikiwemo Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.
Leo watasaini MOU?
 
Wanahangaika hao wa Hungary na wanatafuta maeneo ya kuvuna na kutokea kwenyei ugomvi yao na E U

Na Chama chake cha siasa kina husishwa na wale wazungu wasiopenda watu weusi. (ultra conservative/right wing)Hivyo basi mkae mkijua hajaja kufanya mapenzi na sisi...hapendwi mtu hapa. Na wasiwasi katumwa huyo mdada kuja kumlainisha SSH.
 
Back
Top Bottom