Peru: Waziri Mkuu ajiuzulu baada ya mazungumzo yake ya faragha kuvuja

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
PERU: Waziri Mkuu, Alberto Otárola, (57) amejiuzulu baada ya tuhuma za kuwa alijaribu kutumia Ushawishi wake kumsaidia Mwanamke kupata Mikataba ya Serikali yenye faida baada ya mazungumzo yake na Mwanamke huyo kuvuja

Kulingana na kipindi cha Panorama ambacho kilirusha Mazungumzo hayo, Mwanamke huyo Yaziré Pinedo, (25) alipewa Mikataba Miwili kwa kazi katika Wizara ya Ulinzi mnamo 2023 ambayo ilimuingizia jumla ya Dola za Marekani 14,000 Takriban Tsh. Milioni 35.6

Otárola alikuwa Waziri wa ulinzi wa Peru hadi mwisho wa 2022

Katika mazungumzo hayo Otárola anasikika akikiri mapenzi yake kwa Mwanamke huyo na kumwomba atume CV yake, ambapo Wote wawili wamesema mazungumzo hayo ni ya tokea 2021 (kabla Otárola hajawa Waziri) huku Uchunguzi zaidi wa tuhuma hizo ukianza mara moja

...........

Peru's Prime Minister Alberto Otárola has resigned over allegations he attempted to use his influence to help a woman gain lucrative government contracts.

The scandal escalated last week when a Peruvian TV broadcaster aired audio clips of what it said were conversations between the two.

Mr Otárola, 57, has denied any wrongdoing.

A formal investigation has been launched into the allegations.

According to the Panorama programme, which first aired the clips over the weekend, the woman Mr Otárola can be heard speaking to is Yaziré Pinedo, 25.

Ms Pinedo was reportedly awarded two contracts for work in the defence ministry in 2023 that earned her a total of 53,000 sol ($14,000; £11,000).

Mr Otárola was Peru's defence minister until the end of 2022, when President Dina Boluarte took office and he was promoted.

In the audio clips, Mr Otárola can be heard declaring his love for the woman and asking her to send him her CV.
The remarks appear to contradict a statement he made prior to their release, that he had only met Ms Pinedo once at a meeting.

She told Peruvian broadcaster Canal N on Tuesday that she had previously had a brief relationship with him.

Both have said the audio recordings were from conversations in 2021 - before Mr Otárola became a cabinet minister.

Nevertheless, President Boluarte demanded he return early from an official visit to Canada, and his resignation followed.

"Those who have always wanted me out of the government... have not even hesitated to edit an audio with the veiled purpose of tarnishing my image," Mr Otárola said in his resignation speech.

Among those he has accused of being part of a plot to disgrace him is former Prime Minister Martín Vizcarra, who said on social media that he "strongly rejected" the "delusional accusations".

According to Peruvian law, all 18 members of Peru's cabinet must follow Mr Otárola and hand in their resignations - but the president has the choice to reselect them again if she wishes.

Peru's government is no stranger to shake-ups - Ms Boluarte has ordered several cabinet reshuffles since taking power as she attempts to quell opposition to her leadership.

Source: BBC
 
Una ona nchi za wenzetu walivyokuwa wako serious kwenye masuala ya serikali, cv tuu ina mfanya mtu ana jivua madaraka mwenyewe bila kulazimishwa, hapa kwetu waziri ana ingia mikataba mibovu ana uza rasilimali za nchi kwa mikataba ya kijinga, ana iingiza nchi kwenye hasara ya trilioni za pesa alafu bado yupo ofisini hataki kusikia mambo ya kujiuzulu...
Hapo bado hujaweka ubabe wa viongozi wengine kudhulumu mali za wananchi kwa kisingizio una nijua mimi nani.
Afrika hasa Tanzania sisi hatupaswi hata kuwa nchi ya dunia ya 3, sisi ustaarabu bado sanaaaa. Ni kama wale watu ambao wanaishi misituni huko mpaka karne hii hawataki kuona hata ndege inapita angani wala kukutana na binadamu wengine.

Sisi bado sanaaa tunacheza cheza makida makida tuu suala la uongozi sisi tupo nyuma miaka 💯
 
Back
Top Bottom