Human Nature

Haya leo ni mwendo wa masong tu

Welcome back mtoa mada
I'm back πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
Ma song ya motoooo
Halafu ngoma zote ni vitu vyangu kabisa πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
Say yeeeeeeeeee! Nice to hear that,karibu sana
Mimi bado nitakuwa na mtazamo tofauti na wewe

Bado nakuja pale pale kwenye ndani ya nafsi zetu,mfano binadamu wote tumeumbwa na nafsi ambayo inatuambia au kuhisi kuna nguvu zaidi yetu ambayo ndio kimbilio letu pale tunapotaka msaada au kutatua shida zetu

Wengine wanaita Mungu,wengine mizimu,wengine wanajua wanavyoita

Ndio maana kuna wanaobudu kwenye miti mikubwa,wengine kwenye mapango na wengine,jua na kadhalika,hii ni kuonyesha kwamba nafsi za binadamu zinatambua kuna nguvu ambayo ndio kimbilio lao

Sasa mazingira ndio huwa shape watu ama kubakia kwenye ile nafsi ya asili ambayo inatambua jema na baya au kuwapa kitu kipya ambacho kitawatoa kwenye uhasilia wao

Ndio ile mfano ulio toa sasa,binadamu sasa anatambulishwa kwenye system nyingine ya maisha ya kuwa na uhusiano wa jinsia moja,mazingira yana nafasi kubwa sana ya kubadilisha tabia na mienendo ya watu

Sasa kile ambacho ndio binadamu atakuwa anakutana nacho mara kwa mara ndio kitaamua awe ni mtu wa namna gani
 
Mdada to cut the story si unajua tuna vichwa viwili,sasa Saidi Kipara akifanya maamuzi ni ngumu kuyakwepa
 
Hakika hakika
 
Akili zetu huchagua zaidi yale yaliyo mepesi na haraka kwetu. Hii inaweza kuwa kwa ajili ya kujilinda ama kupata faida flani.

Hizo "kanuni" tulizitunga sisi wenyewe wakati tunaanza kuishi kimakundi enzi hizo ili tusifarakane hovyo.

Lengo la kanuni sio kutubadilisha, ni kutudhibiti. Hatuwezi kubadilika, ila kuna wale ambao hupoteza utimamu wao, ama hushawishika kufanya mambo hatarishi sana mfano kuua watu. Kanuni/sheria zinasaidia kuwakabili hawa.
 
Mkuu karibu tena na Asante kwa maada mujarabu.

Binafsi nitatumia mtazamo wa kiimani ili kujibu hii hoja.

Mungu alipoumba dunia aliumba mambo mema na mabaya lakini pia alimpa mwanadamu uhuru wa kuchagua kati ya mema na mabaya. Kumbukumbu ya torati 30:15,19

Tukiongelea mambo mema na mambo mabaya hii inakua ni jambo la asili. Lakini binadamu kufanya jambo jema au baya hiyo siyo asili bali ni chaguo ambalo mtu ameamua kulitenda kwa akili zake.

Hivyo nahitimisha kwa kusema matendo yote mabaya au mema ni matokeo ya mtu kuchagua kuyatenda hayo wala sio human nature au sijui bahati mbaya. Hayo yote ni machaguo ya mtu mwenyewe.
 
F
Finally, somebody has resurfaced after disappearing misteriously for a short while.
 
Shukran sana
Kanuni tulizipanga wenyewe kwa utashi na kwa kuzingatia asili ya mwanadamu

Tumetunga kanuni ya adhabu kwa mtu aliemuua mwingine ili iwe fundisho watu wasichukulie kawaida kuuana

Kwahiyo dunia bila kanuni
Ingekua mbaya zaidi

Kama ulivyosema awali kua mzazi kuiba kwa ajili ya mwanae ni kukosa option
Na ukajaribu kuhalalisha kua hakua na chaguo

Na kumbe wakati huo huo ameiba chakula kilichohifadhiwa kwa ajili ya mtoto mwingine kwahiyo amepeleka maumivu kwa mwingine

Kitu ambacho sio sawa
Kwa sababu kinaponya hapa kinajeruhi kule kwa mantiki hiyo akibainika atawajibishwa hata kama atajitetea mwanae alikua na njaa wala hakuna huruma juu yake

Kwa sababu bado angeweza kuomba kuliko kuiba
 
Mkuu karibu tena na Asante kwa maada mujarabu.
Shukran sana mkuu nimekaribia
Yaan huku ulipokuja tutahamisha mada mkuu yaani kulikua na mantiki ipi
Mungu aumbe mabaya?
Kwa faida ipi?
Kwa lengo gani?
 
Ukiweza hivi maisha yanakua matamuu mnoo
 
Homo Sapiens big 🧠
 
Ujue hapa wewe na mshamba_hachekwi hamtaelewana
Maana hapa umeshaingiza dini na yeye sidhani kama ni vitu vyake
 
Ukiweza hivi maisha yanakua matamuu mnoo
siku ukiacha kutafsiri mambo au vitu kwamba hili baya au nzuri unaweza kuishi maisha ya raha sana binafsi siamini kama kuna mtu anaweza kuniumiza au kunipa furaha tofauti na mim.
DUNIANI hakuna jambo baya wala nzuri ni mtazamo wako tu unaomuumiza mtu mfano mzuri unakuja kuabiwa fulani alikuwa anakuogea vibaya unaumia kabla hujajua why hukuumia lakn ukichukulia kawaida kama unavyolichukulia jiwe huwezi kuumia.
 
Duniani hakuna jambo baya au zuri?
Ukimuibia mtu ni nini inakua ?

Ukimkata mkono mtu mwingine ni nini hiyo inakua?

Dunia ipi hiyo haina baya wala zuri nikaishi?
 
Duniani hakuna jambo baya au zuri?
Ukimuibia mtu ni nini inakua ?

Ukimkata mkono mtu mwingine ni nini hiyo inakua?

Dunia ipi hiyo haina baya wala zuri nikaishi?
nikuulize swali jepesi tu kabla sijakujibu
Ni jambo lipi ambalo binadamu wote tunaamini ni nzuri au baya?.
Kwamba ili jambo ukifanya kila mtu anaamini ni nzuri?
 
nikuulize swali jepesi tu kabla sijakujibu
Ni jambo lipi ambalo binadamu wote tunaamini ni nzuri au baya?.
Kwamba ili jambo ukifanya kila mtu anaamini ni nzuri?
Jambo lolote lile linaloacha hisia za maumivu tunaliita baya

Labda kama wewe una jina lingine
Haya ni nijib na mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…