SoC02 Huduma ya vyoo vya kulipia kwenye vituo vya daladala

Stories of Change - 2022 Competition

pbwmasanja

Member
Mar 20, 2013
5
7
HUDUMA YA VYOO VYA KULIPIA KWENYE VITUO VYA DALADALA
UTANGULIZI:

Tukichukulia maisha ya mjini hasa miji mikubwa kama Dar es Salaam suala zima la mahitaji ya choo ni muhimu kwa jamii. Na karibu asilimia kubwa ya jamii ya wakazi wa mjini hasa miji mikubwa wanapata huduma ya choo.

Hata hivyo mimi katika mazingira magumu sana siku moja nikiwa katika harakati zangu za kawaida nilikuja kugundua kuwa wasafiri wanaotegemea usafiri wa umma mjini (daladala) hii huduma ya vyoo haiwazingatii na haiwajali na niseme kwa asilimia kubwa haipo.

Siku moja nilisafiri kutoka Kibamba Shule Manispaa ya Ubungo katika jiji la Dar es Salaam kwa njia ya daladala ya kawaida inayoenda moja kwa moja Mawasiliano (Simu 2000) kupitia Ubungo. Kwa bahati mbaya tumbo langu lilivurugika na nilihitaji kupata huduma ya choo kwa haraka kabla sijaharibikiwa na pengine kuchafua mazingira. Wakati huo pesa niliyokuwa nayo mfukoni ilikuwa inatosha nauli moja tu ya kunifikisha katika kituo cha Mawasiliano bila kubadilisha gari.

Kwa hali niliyokuwa nayo ya mvurugiko wa tumbo nilifikiria sana kushuke kituo chochote njiani kabla ya kufika ii nikatafute huduma ya choo cha kulipia huduma ambazo kwa kawaida hazipo kwenye vituo vya daladala. Lakini changamoto niliyokuwanayo ilikuwa je nikishuka kabla sijafika suala la nauli ya kupanda gari nyingine ya kumalizia safari yangu baada ya kupata hiyo huduma ya choo litakuwaje. Ile hali ya bana nikubane tumbo kuvurugika ilizidi nikaona bora tu nilipe ile nauli yangu kisha nishuke pale Kimara Suka na nitajua la kufanya baada ya hapo. Nilifanikiwa kwenda kwa mwendo wa kasi ya mwanga hadi kwenye choo cha kanisa (Bahati nzuri katika eneo hilo nilijua kuna kanisa lipo jirani na kituo cha daladala) bila ruhusa ya wahusika na niliharisha ipasavyo. Baada ya shughuli yangu ya chooni niitoka na kujijieleza kwa muhusika aliyekuwa pale nje ya choo akisubiri ajue kulikoni niliingia chooni bila ruhusa, lakini nilijieleza nikaeleweka akaniruhusu nikaondoka. Hatua chache tu baada ya kuachana na mhusika wa kile choo mara nilianza kufikiria jinsi ya kufika Mawasiliano bila kuwa na pesa yoyote ya nauli.

Kwa kifupi siku hiyo nilipata taabu sana, taabu iiyotokana na tatizo la ukosefu wa huduma ya choo kwenye vituo vya daladala. Naamini tatizo au changamoto hii inawakumba na inawasumbua sana watu wengi itokeapo dharura kama iliyonipata mimi au mtu anapokuwa yupo kituoni na akabanwa na haja ndogo au kubwa.

PENDEKEZO
Baada ya utangulizi kwa kutumia simulizi ya changamoto ya lililonikuta na ambalo nahisi wengi limekwishawakuta au litawakuta sasa tuongee nini cha kufanyka kutatua changamoto hii.

Pamoja na kwamba mamlaka husika hazijatafuta ufumbuzi wa suala hili kwa sababu yoyote ile iwe ama kwa kujua au kutokujua, mimi kwa upande wangu naliona hili kwa jicho la kama fursa ya kiuchumi kwa wadau mbali mbali katika kutoa huduma maalumu ya choo kwenye vituo vya daladala. Kwa upande mwingine ukiachiia mbali suala la ustaarabu na maadili, naliona jambo hili kimazingira na kiafya lina athari kubwa kwa maana vituo vingi vya daladala vimechafuliwa na vinaendelea kuchafuliwa sana na mkojo na vinyesi hasa nyakati za usiku.

Kwa upande wa wajasrliamali nafikiri jambo hili linatakiwa kama fursa kwa kufikiria kuanzisha huduma ya vyoo vya kulipia vinavyotembea (commercial mobile toilets) kwa kutumia magari yanayotembea (yaliyotengenezwa aalumu) yenye vyumba vya choo walau viwili na tanki la maji safi na taka. Magari haya yanaweza kuwa yanatembea kutoka kituo kimoja hadi kingine huku yakisimama walau kwa nusu saa kwene kila kituo ii kutoa nafasi na muda wa kutosha kwa watumiaji. Muda wa magari haya maalumu kupishana kufika kituoni isizidi dakika 15 baada ya gari lililotangulia kutoka kituoni. Magari haya yanaweza kusajiliwa na kupatiwa leseni ya biashara hii.

Kwa wale wenye magari ya huduma ya maji taka wanaweza kuboresha magari yao nakupata leseni au kibali maalumu cha kuweza kutoa huduma ya vyoo na maji taka kwenye vituo vya daladala badala ya kusubiri wateja wa maji taka wa majumbani. Kinachoweza kufanyika kwenye magari haya ni kuongeza vyumba vya kujisaidia ama kwenye gari hilo hilo au kuongeza trela maaumu kwa ajili hiyo na kugawanya tanki katika sehemu ya maji safi na taka ili kukidhi mahitaji.

Kama aina zote mbili za vifaa vya vyoo vilivyopendekezwa hapo juu zitaonekana zina changamoto ya utekelezaji, nafikiri wajasiriamali wafikirie au wathubutu kuwasiliana na mamlaka zinazohusika na masuala ya afya, mazingira na vituo vya daladala kuona namna bora ya kujenga na kutoa huduma ya choo ya kulipia katika vituo vyote vya daladala ama vituo vya muda au kudumu ilimradi tu hii huduma ipatikana.

Pamoja na kuimarisha afya ya abiria na jamii, huduma hii ya vyoo kwenye vituo vya daladala itadumisha usafi wa mazingira na kuwa chanzo cha mapato kwa watoa huduma na kodi kwa serikali.

Kwa kumalizia napenda kuziweka wazikwa ufupi faida za kijamii, kimazingira, kiutamaduni na kiuchumi kama ifuatavyo:
  • Kuzalisha fursa za ajira kwa wananchi;
  • Kuboresha afya ya jamii;
  • Kupunguza uchafuzi wamazingira;
  • Chanzo cha mapato kwa watoa huduma;
  • Kuboresha hali ya maisha ya wanajamii;
  • Kuongeza mapato kwa serikali kwa njia ya kodi;
  • Kupunguza watu kujisaidia ovyo kinyume na maadili ya watanzania, nk
Kwa wadau wowote watakaoona kuwa hii ni fursa kibiashara, taasisi yangu iitwayo TANZANIA BUSINESS AND SELF EMPLOYMENT CONSULTANTS kwa kutumia timu yake ya wataalamu ipo tayari kusaidia kwa gharama zinazowezekana kuandika mpango wa biashara au pendekezo la mradi huu na kuwaunganisha na taasisi za fedha, wawekezaji na wafadhii wataona kuwa mradi au biashara hii inafaa kufanyika.

tanbsec@gmail.com
 
Back
Top Bottom