Serikali iache kujenga matundu ya vyoo/vyoo vya shimo, ijenge vyoo kamili vya kisasa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,634
46,277
Katika karne hii Huwa nasikia wanasiasa na viongozi wa serikali wakizungumzia ujenzi wa "matundu" ya vyoo katika shule kama mojawapo ya mafanikio yao nashangaa sana!

Matundu ya vyoo mara nyingi kama sio zote huwa ina maana ya vyoo vya shimo ambavyo vilikuwa ni hatua ya pili baada ya binadamu wa zamani sana kuacha kujisaidia hovyo nje katika mazingira yasiyo na choo.

Mfumo wa choo cha kuflashi uligunduliwa tangu mwaka 1596 au karne ya 16 na John Harrington huko Uingereza na karne ya 17 ukaboreshwa zaidi ambapo umeendelea kutumika mpaka leo kwa maboresho mbalimbali.

Mfumo wa vyoo vya matundu au vya shimo ni wa kale mno wa binadamu ambao walikuwa bado wanajitafuta katika ustaarabu.

Serikali sasa iongeze njia kwa raia wake, ni wakati wa kujenga vyoo kamili katika shule na taasisi zake zote na iachane na matundu ya vyoo au vyoo vya shimo.
 
Wana pesa za V8 tu
 
Back
Top Bottom