How the Dreamliner is Killing Tanzanians dream?

Ni sawa na mtu anaenunua tv la million 3 ili aende sawa na jirani yake badala ya kuanza kwa kufungua kitega uchumi ambacho kingeingiza pesa kila siku kwa kutumia gharama hio hio ya 3m kisha angeweza nunua tv kwa faida inayopatikana.
Hii biashara ya ndege kuongozwa kisiasa itatuletea matokeo kati ya haya.

1. Shirika kupata hasara na serikali kukubali kushindwa.

2. Shirika kupata hasara na serikali kufunika hasara kwa kukataza ukaguzi wa CAG na ku pump hela zaidi ili kisiasa serikali isiadhirike.

Time will tell.
 

Pascal Mayalla,
Post zako nyingi sana zina support Utawala wa Magufuli, your homeboy lakini the same Magufuli is not supporting you as an individual...!!!Swali ni Je, wewe kama Pascal unafaidikaje na hii midege ya Bombadier, Dreamliner na Airbus?
Hivi Mtanzania wa kule kijijini kwenu Chato hii midege inamsaidiaje au kuinua uchumi wake kama mtu binafsi?
Mfano rahisi kabisa kwa layman: Wewe ni baba nyumbani kwako una watoto 5 au 10(Wasukuma kwa kuzaa hamjambo) unakuta kwamba kipato chako nyumbani ni kununua magari say ma-bus au maroli ya mizigo kwa ajili ya biashara. Fedha ikiingia unaongeza maroli na mabus, unajenga majumba ya kupangisha n.k. Mtu akifika nyumbani kwako anakuta hali ya sintofahamu:
  1. Watoto hawana Chakula cha kutosha wamejaa Kwarshakor(Utapiamlo).
  2. Watoto hawasomi shule ubora kulingana na kipato chako matokeo yake wanaishia la saba au Kidato cha 4 basi.
  3. Mkeo hapendezi amechokeana mbaya. Hana mavazi ya maana na hajawahi kuingia salon.
  4. Kazi yako ni kugombana na majirani kutwa kucha ni kufoka, kutukana na kuwasimanga kuwa hawana akili ndio maana wanazidi kuwa maskini.
  5. Maiirani wakija wanalia njaa wewe ndo unakuwa kimbelembele kuwapa fedha au Chakula ilhali wanao wanalia njaa nyumbani.
Kwa akili ya kawaida tu baba mwenye hekima na busara atataka kwanza ainue hali ya familia yake kwa kuhakikisha watoto wanasoma shule nzuri wafike hadi Chuo Kikuu baadaye waje kuwa wabobezi katika maeneo na nyaja za biashara anazofanya baba yao hatimaye kuja kuinua Uchumi wa Familia nzima. Baba mwenye busara atahakikisha mke wake siku zote anapendeza na presentable kwa jamii ili watu wakimwona wanajua huyu ni hakika ni mke wa Mayalla!

Rais Magufuli anaonekana ni baba asiye na busara. Badala ya kuwekeza Fedha inayopatikana kwenye elimu, elimu, elimu na afya, afya, afya na siyo kununua midege ambayo nina hakika fedha inayopatikana haitagusa maisha ya Mtanzania mmoja mmoja. Bado hii midege wanaoweza kuipanda ni kwa wale tu wenye uwezo. Dege kama Dreamliner haitawahi fanya safari za ndani(Local Flight) kwa vile imeundwa maalumu kwa masafa marefu. Usitegemee kuna siku utapanda Dreamliner from DAR to Chato wakifanya hivo wanaiua sasa hivi...!! Biashara ya Midege ni ngumu. Ukitaka kujua hivo angalia Mataifa yenye National Carriers kama Ethiopia Airliners, Kenya Airways, SA Airliners...hali zao ni tete kibiashara lakini pia Wananchi wao hawana hali nzuri kiuchumi eti kwa vile wana midege.....!!!

Kwenye Ilani ya Uchaguzi kulikuwa na Ahadi ya milioni 50 kwa kila Kijiji....ziko wapi? Nina hakika hii Fedha anayonunulia midege ingelipelekwa kwa wanakijiji...wakafundishwa Ujasirimali,wakaanzisa Biashara ya Viwanda vidogovidogo kwa njia ya mikopo(Vicoba, Saccos au any SMEs) nchi ingelikuwa iko mbali. Kumbuka Wachina wamejengwa Uchumi wao kwa kutegemea Wananchi wenye Uchumi wa chini kujenga Uchumi mkubwa.

Hii midege haitakaa hata siku moja ibadilishe maisha ya Watanzania. Tuesikia ATCL mpaka sasa wana Dola milioni 14 sawa na Tshs. Trilioni 30. Sina hakika kama hii fedha iko Benki na kama ipo sina hakika kama ATCL hawadaiwi na Taasisi au Wazabuni wao. Sina hakika kama ATCL wameshatengeneza Faida maana huu mwaka 3 sijasikia wakitoa Public Financial statement kuonesha performance yao. Lakini pia sijasikia wametowa gawio kwa Serikali ya Magufuli....!!
 
Kiswahili "tumemamua" au "ameamua" sidhani kama tulishirikishwa
 
Kiswahili "tumemamua" au "ameamua" sidhani kama tulishirikishwa

Hii Serikali siyo Shirikishi hata kidogo na MAAMUZI YOTE ANAFANYA JIWE akiwa na mkewe...!!Baba wa Taifa aliwahi kusema tusichague Rais ambaye HATUJUI KESHO AKIAMUKA ATASEMA NINI maana kazi yake ni kusikiliza ushauri na majungu ya mkewe...!!! Magufuli ndiyo Waziri wa Fedha, ndiyo BOT Governor, ndiye Bunge linalopanga Bajeti...!!!

Sijawahi ona Rais anatembea na lundo la mailioni ya Fedha kwenye ziara halafu akifika sehemu anatoa maburungutu ya mamilioni kuchangia miradi....!!!Hii fedha nani anakuja kui-account for? Je, kwanini hatumii ku-issue Cheque badala ya Cash?
Je, ina maana Rais au Ikulu haina Account ya matumizi? Kama hakuna Rais Magufuli mwenyewe hana Account yake binafsi ili akiwapa watu Cheque waka deposit bank na kufuata taratibu za malipo? Iko kitu haiko sawa hapa...!!!
 

Hii nina copy na ku-paste ili Magufuli na Timu yake ya Lumumba waisome na kuitafakari.....This is big....!!!Kama hawawezi kuchukua ushauri huu tunakokwenda watalia kilio cha mbwa...mdomo juu....Time gonna tell!

..;ndege zimeanza lini safari?

..na msimu wa watalii ni lini?

..na watalii wengi wanatokea nchi gani?

..Kagame ambaye amemshauri Jpm kununua ndege ameshasalimu amri baada ya kuingia hasara mwaka hadi mwaka. Sasa ameamua kuuza hisa za Rwanda Air kwa Qatar.

..South Africa wanapokea abiria wengi, na watalii wengi kuliko Tz, lakini shirika lao la ndege linaendeshwa kwa hasara.

..Ni makosa kwa Tz kujiingiza ktk biashara kichaa ya usafiri wa anga.

..Biashara ya mashirika ya ndege inazifaa nchi zenye fedha za kuchezea kama Qatar, na UAE. Wenzetu wana mapesa ya kununua dreamliners 40 kwa mara moja.
 
Nimeona nikujibu kizungu.

You are indeed very stupid!!!!

Writing this article in English does not give it an academic or any intellectual edge. It's just horrendous!!!!
 
Pascal Mayalla,
Post zako nyingi sana zina support Utawala wa Magufuli, your homeboy lakini the same Magufuli is not supporting you as an individual...!!!Swali ni Je, wewe kama Pascal unafaidikaje na hii midege ya Bombadier, Dreamliner na Airbus?
Mkuu Mzalendo2015, kwanza namsupport rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, sio kwasababu ni homeboy wangu, bali namsupport kwenye yale mema na mazuri, lakini kwenye mabaya namkosoa sana tuu.

Watanzania tuko zaidi ya million 50, kati ya hao wanaomsuport Magufuli ni over 20 millions, Magufuli atahitaji kuwasupport individual wangapi?.

Support yangu kwa Magufuli sio ya kujikomba komba kutafuta uteuzi ndio maana kwenye mazuri ndio napongeza lakini kwenye mabaya, nakosoa.

Kwenye hili la ndege, nimechangia vya kutosha. Karibu pande hizi




P
 
Yani mimi sielewi, watu wananalalamika kuhusu ununuzi wa hizi ndege eti ni kupoteza muda na manufaa yake ni si kwa watanzania wote na pia si ya moja kwa moja kwa wanananchi.

Sasa basi humu hebu tuambieni humu ndani nyie hizo dola millioni 200 mzifanyiaje ili kuanzia Kesho kipato cha kila mtanzania kukue kutoka hii dola 2 kwa siku hadi huko kwenye dola zaidi ya 20 kwa siku mnapotaka nyie.

Tusaidiane basi maana nchi si yetu sote!!! Tupeni mawazo basi!!!
 
If it was my decision I would rather leave airline business to private sector and the concentrate on policy issues Airline is a business that require an Investor to be very dynamic, with the government system of delaying decision making I do not see how this airline is going to compete in this very saturated market. We do not need a rocket science to know that airline business is too risk for a country like Tanzania. Every one would expect that the little resources that we have would be used with highest care but the opposite is the reality. As a transport professional I do not see any good future for ATCL, except political mileage.
 
Mkuu uko vizuri. Idea yako iko sawa. Lakin kwenye kuchagua mradi gan mkubwa unaweza kuleta mult plier effect ni tatizo kwako. Unajua ukiangalia kwa mapana, mtanzania anahitaji kwanza kabisa umeme. Umeme ni kitu cha kwanza kabisa. Ni muhimu tukawa na umeme kila kona ya nchi ili kuwezesha shughuli ndogo ndogo za kiuchumi kwa kila mtanzania ikiwemo kilimo cha kisasa. Kwa maana hiyo mradi wa stigler gorge ni muhim sana. Unahitajika sana. Pamoja na mradi wa umeme vijijin - rea. Nategemea watanzania wapige kelele utekelezaji wa miradi hii uende kwa kasi sana.

Lakin watanzania hawa wanahitaji masoko ya bidhaa zako. Masoko ya mazao na kazi za mikono. Masoko ya vivutio vya utalii. Kwa maana hiyo miradi yoyote yenye kuleta au ku saidia hayo mambo ni muhimu sana. Mfano ni mradi wa miundo mbinu. Bara baara, madaraja, viwanja vya ndege na ndege zenyewe. Ni muhimu sana. Miradi hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi wetu. Mtanzania mwenye akili timamu ata suport miradi ya aina hii kwa nguvu zake zote.

Lakin pia tunahitaji miradi ya kubadilisha afya zetu na maisha yetu. Miradi kama ya elimu bure kwa watoto wetu, miradi ya maji vijijin, na miradi ya hospitali au dispensary kwa kila kata.

Ni muhimu kwa ajili ya kubadili maisha ya mtanzania.

Sielewi kwann mtanzania wa kawaida haelewi maana ya investment kubwa zinazofanyika nchin.

Lakin pia ni vizuri kutambua kuwa kila sehem, kila mahali pakiweza kufikika then inakuwa rahisi kufanya shughuli yoyote ya kiuchumi kwa kila mwananchi wa kawaida.

Pia ni vizuri ikawa wazi kuwa labda awamu zijazo zinaweza kuwa na program ya kugawa hela au ajira kwa kila mtanzania. Lakin kwa sasa tunaomba haya niliyoyataja yafanyike kwa faida ya kila raia wa tanzania.
 
Chief kuajiri ni kazi ya sekta binafsi na sio serikali.

Kazi ya serikali ni kuweka mazingira bora kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi
 
Mifano yako yote haiko relevant na mada iliopo mezani
 
Ukweli ni kuwa hya mandege yanatutia hasara, nasapoti rais ajaye ayauze yote
 
We nae hutumii hta akili kufikiri

Hujui kuwa wananchi kupata maji safi ni advantage kwao kwani watatumia muda mwingi kwenye shughuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda huo kwenda kutafuta maji!

By the way utatumia vipi billions of money kwenye sekta ambayo inawakilisha only 1% ya population na kuitekeleza sekta sekta ya kilimo inayowakilisha 80% ya population?

Hyo itakuwa akili au matope?
 

Pascal,
Sidhani kama kwenye nafsi yako unaamini unachokisema na kukisimamia....!
Kwamba unamkosoa Magufuli kwa mabaya anayowafanyia Watanzania......Kwamba hujikombi kwa homeboy wako kweli...!!I can't believe you!

Sijawahi kusikia kauli yako thabiti kuhusu kile kilichompata Tundu Lissu ikiwa ni katika mabaya Utawala wa Magufuli umewatendea baadhi ya Watu wakiwemo Ben Saanane na Azory Gwanda....!

Nina hakika moyoni mwako leo hii ukisikia Ikulu imetangaza jina lako katika uteuzi wa Ukuu wa Wilaya hakika utafanya sherehe na utakuwa wa kwanza kufika Ikulu kula kiapo...!!!

Mimi napenda kukushauri wewe na Watz wengine tusemeni ukweli tu badala ya unafiki na kujikomba komba ili kupata vyeo...!!Hi itamsaidia home boy wako badala ya kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa huku akizidi kuiharibu nchi...!!!
 
Km issue ni ajira kwanini hyo mapesa ya ndege tusiwekeze kwenye kilimo ambapo inaweza kuajiri hadi 80%ya population

Agribusiness ndyo sekta pekee itakayotutoa hpa tulipo. Na sio hyo mandege
 
Siku akiingia Rais aliechaguliwa na watu, hiyo midege itauzwa ama ikodishwe kwa mashirika ya ndege yanayofanya biashara, kuliko hii biashara yetu ya kisiasa!
Hizi akili za kikagame za serikali kulipa gharama za kuendesha shirika lao la ndege ni ushamba wa kiwango cha changarawe, kisa sifa tu kwamba serikali inamiliki ndege nyingi bila faida.
kama wanabisha waruhusu CAG akague hesabu zake tuone miujiza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…