How the Dreamliner is Killing Tanzanians dream?

How the Dreamliner is Killing Tanzanians dream?

Ni sawa na mtu anaenunua tv la million 3 ili aende sawa na jirani yake badala ya kuanza kwa kufungua kitega uchumi ambacho kingeingiza pesa kila siku kwa kutumia gharama hio hio ya 3m kisha angeweza nunua tv kwa faida inayopatikana.
Hii biashara ya ndege kuongozwa kisiasa itatuletea matokeo kati ya haya.

1. Shirika kupata hasara na serikali kukubali kushindwa.

2. Shirika kupata hasara na serikali kufunika hasara kwa kukataza ukaguzi wa CAG na ku pump hela zaidi ili kisiasa serikali isiadhirike.

Time will tell.
 
Kupanga ni kuchagua, tumeamua kuchagua kufanya maendeleo ya vitu kwanza, kama ndege, miundombinu, SGR, Stigler, flyover, na kujenga Tanzania ya Viwanda. Miradi hii mikubwa ikikamilika, ndipo tutageukia maendeleo ya watu.
P

Pascal Mayalla,
Post zako nyingi sana zina support Utawala wa Magufuli, your homeboy lakini the same Magufuli is not supporting you as an individual...!!!Swali ni Je, wewe kama Pascal unafaidikaje na hii midege ya Bombadier, Dreamliner na Airbus?
Hivi Mtanzania wa kule kijijini kwenu Chato hii midege inamsaidiaje au kuinua uchumi wake kama mtu binafsi?
Mfano rahisi kabisa kwa layman: Wewe ni baba nyumbani kwako una watoto 5 au 10(Wasukuma kwa kuzaa hamjambo) unakuta kwamba kipato chako nyumbani ni kununua magari say ma-bus au maroli ya mizigo kwa ajili ya biashara. Fedha ikiingia unaongeza maroli na mabus, unajenga majumba ya kupangisha n.k. Mtu akifika nyumbani kwako anakuta hali ya sintofahamu:
  1. Watoto hawana Chakula cha kutosha wamejaa Kwarshakor(Utapiamlo).
  2. Watoto hawasomi shule ubora kulingana na kipato chako matokeo yake wanaishia la saba au Kidato cha 4 basi.
  3. Mkeo hapendezi amechokeana mbaya. Hana mavazi ya maana na hajawahi kuingia salon.
  4. Kazi yako ni kugombana na majirani kutwa kucha ni kufoka, kutukana na kuwasimanga kuwa hawana akili ndio maana wanazidi kuwa maskini.
  5. Maiirani wakija wanalia njaa wewe ndo unakuwa kimbelembele kuwapa fedha au Chakula ilhali wanao wanalia njaa nyumbani.
Kwa akili ya kawaida tu baba mwenye hekima na busara atataka kwanza ainue hali ya familia yake kwa kuhakikisha watoto wanasoma shule nzuri wafike hadi Chuo Kikuu baadaye waje kuwa wabobezi katika maeneo na nyaja za biashara anazofanya baba yao hatimaye kuja kuinua Uchumi wa Familia nzima. Baba mwenye busara atahakikisha mke wake siku zote anapendeza na presentable kwa jamii ili watu wakimwona wanajua huyu ni hakika ni mke wa Mayalla!

Rais Magufuli anaonekana ni baba asiye na busara. Badala ya kuwekeza Fedha inayopatikana kwenye elimu, elimu, elimu na afya, afya, afya na siyo kununua midege ambayo nina hakika fedha inayopatikana haitagusa maisha ya Mtanzania mmoja mmoja. Bado hii midege wanaoweza kuipanda ni kwa wale tu wenye uwezo. Dege kama Dreamliner haitawahi fanya safari za ndani(Local Flight) kwa vile imeundwa maalumu kwa masafa marefu. Usitegemee kuna siku utapanda Dreamliner from DAR to Chato wakifanya hivo wanaiua sasa hivi...!! Biashara ya Midege ni ngumu. Ukitaka kujua hivo angalia Mataifa yenye National Carriers kama Ethiopia Airliners, Kenya Airways, SA Airliners...hali zao ni tete kibiashara lakini pia Wananchi wao hawana hali nzuri kiuchumi eti kwa vile wana midege.....!!!

Kwenye Ilani ya Uchaguzi kulikuwa na Ahadi ya milioni 50 kwa kila Kijiji....ziko wapi? Nina hakika hii Fedha anayonunulia midege ingelipelekwa kwa wanakijiji...wakafundishwa Ujasirimali,wakaanzisa Biashara ya Viwanda vidogovidogo kwa njia ya mikopo(Vicoba, Saccos au any SMEs) nchi ingelikuwa iko mbali. Kumbuka Wachina wamejengwa Uchumi wao kwa kutegemea Wananchi wenye Uchumi wa chini kujenga Uchumi mkubwa.

Hii midege haitakaa hata siku moja ibadilishe maisha ya Watanzania. Tuesikia ATCL mpaka sasa wana Dola milioni 14 sawa na Tshs. Trilioni 30. Sina hakika kama hii fedha iko Benki na kama ipo sina hakika kama ATCL hawadaiwi na Taasisi au Wazabuni wao. Sina hakika kama ATCL wameshatengeneza Faida maana huu mwaka 3 sijasikia wakitoa Public Financial statement kuonesha performance yao. Lakini pia sijasikia wametowa gawio kwa Serikali ya Magufuli....!!
 
Kiswahili "tumemamua" au "ameamua" sidhani kama tulishirikishwa
Kupanga ni kuchagua, tumeamua kuchagua kufanya maendeleo ya vitu kwanza, kama ndege, miundombinu, SGR, Stigler, flyover, na kujenga Tanzania ya Viwanda. Miradi hii mikubwa ikikamilika, ndipo tutageukia maendeleo ya watu.
P
 
Kiswahili "tumemamua" au "ameamua" sidhani kama tulishirikishwa

Hii Serikali siyo Shirikishi hata kidogo na MAAMUZI YOTE ANAFANYA JIWE akiwa na mkewe...!!Baba wa Taifa aliwahi kusema tusichague Rais ambaye HATUJUI KESHO AKIAMUKA ATASEMA NINI maana kazi yake ni kusikiliza ushauri na majungu ya mkewe...!!! Magufuli ndiyo Waziri wa Fedha, ndiyo BOT Governor, ndiye Bunge linalopanga Bajeti...!!!

Sijawahi ona Rais anatembea na lundo la mailioni ya Fedha kwenye ziara halafu akifika sehemu anatoa maburungutu ya mamilioni kuchangia miradi....!!!Hii fedha nani anakuja kui-account for? Je, kwanini hatumii ku-issue Cheque badala ya Cash?
Je, ina maana Rais au Ikulu haina Account ya matumizi? Kama hakuna Rais Magufuli mwenyewe hana Account yake binafsi ili akiwapa watu Cheque waka deposit bank na kufuata taratibu za malipo? Iko kitu haiko sawa hapa...!!!
 
..ndege zimeanza lini safari?

..na msimu wa watalii ni lini?

..na watalii wengi wanatokea nchi gani?

..Kagame ambaye amemshauri Jpm kununua ndege ameshasalimu amri baada ya kuingia hasara mwaka hadi mwaka. Sasa ameamua kuuza hisa za Rwanda Air kwa Qatar.

..South Africa wanapokea abiria wengi, na watalii wengi kuliko Tz, lakini shirika lao la ndege linaendeshwa kwa hasara.

..Ni makosa kwa Tz kujiingiza ktk biashara kichaa ya usafiri wa anga.

..Biashara ya mashirika ya ndege inazifaa nchi zenye fedha za kuchezea kama Qatar, na UAE. Wenzetu wana mapesa ya kununua dreamliners 40 kwa mara moja.

Hii nina copy na ku-paste ili Magufuli na Timu yake ya Lumumba waisome na kuitafakari.....This is big....!!!Kama hawawezi kuchukua ushauri huu tunakokwenda watalia kilio cha mbwa...mdomo juu....Time gonna tell!

..;ndege zimeanza lini safari?

..na msimu wa watalii ni lini?

..na watalii wengi wanatokea nchi gani?

..Kagame ambaye amemshauri Jpm kununua ndege ameshasalimu amri baada ya kuingia hasara mwaka hadi mwaka. Sasa ameamua kuuza hisa za Rwanda Air kwa Qatar.

..South Africa wanapokea abiria wengi, na watalii wengi kuliko Tz, lakini shirika lao la ndege linaendeshwa kwa hasara.

..Ni makosa kwa Tz kujiingiza ktk biashara kichaa ya usafiri wa anga.

..Biashara ya mashirika ya ndege inazifaa nchi zenye fedha za kuchezea kama Qatar, na UAE. Wenzetu wana mapesa ya kununua dreamliners 40 kwa mara moja.
 
Tanzania is a country in East Africa with a population of over 50 million people and per capita income of just about 1000 USD. The country has one of the fastest growing graduates unemployment in the region with a very high dependent ratio and rapid population increase.

For the past few years the country has undergone tremendous change in the areas of infrastructure,human rights democracy,freedom as well as inflation.The inflation especially in food crops is rising steadily while the incomes of majority of the population is shrinking due to unemployment and low wages.

Despite all these Tanzania has invested heavily in infrastructure projects including the construction of the SGR, A Hydro Power Project as well the purchase of brand new aircraft to revamp the national career Air Tanzania.

The recent purchase of aircrafts which included a dream liner (Boeing 787-800) comes amidst divided opinion among the majority of the people in the country with some criticizing and others supporting the move.

Analyst have looked at the decision to purchase aircrafts amidst tight resources and majority of them are against the move due to the fact that resources a limited and an aircraft carries with it costs to maintain it and the current aviation market in the country cannot support the operations of a Dreamliner or Air crafts in general.

Some analyst believe that the next president will have to make tough decisions to dispose of the aircrafts and invest the monies where they will have major impacts such as in health,education,water and sanitation as well as in improving the business environment and youth empowerment .

Do you think the Dreamliner will take aways Tanzanians dreams?Let us discuss on other productive use to which the money used to pay for the dreamlines could have been used and the impact that would have.
Nimeona nikujibu kizungu.

You are indeed very stupid!!!!

Writing this article in English does not give it an academic or any intellectual edge. It's just horrendous!!!!
 
Pascal Mayalla,
Post zako nyingi sana zina support Utawala wa Magufuli, your homeboy lakini the same Magufuli is not supporting you as an individual...!!!Swali ni Je, wewe kama Pascal unafaidikaje na hii midege ya Bombadier, Dreamliner na Airbus?
Mkuu Mzalendo2015, kwanza namsupport rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, sio kwasababu ni homeboy wangu, bali namsupport kwenye yale mema na mazuri, lakini kwenye mabaya namkosoa sana tuu.

Watanzania tuko zaidi ya million 50, kati ya hao wanaomsuport Magufuli ni over 20 millions, Magufuli atahitaji kuwasupport individual wangapi?.

Support yangu kwa Magufuli sio ya kujikomba komba kutafuta uteuzi ndio maana kwenye mazuri ndio napongeza lakini kwenye mabaya, nakosoa.

Kwenye hili la ndege, nimechangia vya kutosha. Karibu pande hizi




P
 
Yani mimi sielewi, watu wananalalamika kuhusu ununuzi wa hizi ndege eti ni kupoteza muda na manufaa yake ni si kwa watanzania wote na pia si ya moja kwa moja kwa wanananchi.

Sasa basi humu hebu tuambieni humu ndani nyie hizo dola millioni 200 mzifanyiaje ili kuanzia Kesho kipato cha kila mtanzania kukue kutoka hii dola 2 kwa siku hadi huko kwenye dola zaidi ya 20 kwa siku mnapotaka nyie.

Tusaidiane basi maana nchi si yetu sote!!! Tupeni mawazo basi!!!
 
1572189392725.png
 
If it was my decision I would rather leave airline business to private sector and the concentrate on policy issues Airline is a business that require an Investor to be very dynamic, with the government system of delaying decision making I do not see how this airline is going to compete in this very saturated market. We do not need a rocket science to know that airline business is too risk for a country like Tanzania. Every one would expect that the little resources that we have would be used with highest care but the opposite is the reality. As a transport professional I do not see any good future for ATCL, except political mileage.
 
Kiuchumi, nchi zenye umasikini na kipato cha chini zinatakiwa kujikita kuwekeza katika vitu vitakavyoleta "multiplier effect".

Mradi utakaomuongezea kila Mtanzania mtu mzima kipato kwa shilingi 10 kwa siku ni wa muhimu kiuchumi kuliko a big white elephant project.

Mchumi kila mara anatakiwa aangalie value for money, bang for buck.

Kwenye kununua midege, kwa mfano, hatujapata value for money. Tena kuna uwezekano mkubwa midege ikatutia hasara kubwa sana.

Ni kama vile tumenunua kitu kwa kuangalia ujiko zaidi ya uchumi.
Mkuu uko vizuri. Idea yako iko sawa. Lakin kwenye kuchagua mradi gan mkubwa unaweza kuleta mult plier effect ni tatizo kwako. Unajua ukiangalia kwa mapana, mtanzania anahitaji kwanza kabisa umeme. Umeme ni kitu cha kwanza kabisa. Ni muhimu tukawa na umeme kila kona ya nchi ili kuwezesha shughuli ndogo ndogo za kiuchumi kwa kila mtanzania ikiwemo kilimo cha kisasa. Kwa maana hiyo mradi wa stigler gorge ni muhim sana. Unahitajika sana. Pamoja na mradi wa umeme vijijin - rea. Nategemea watanzania wapige kelele utekelezaji wa miradi hii uende kwa kasi sana.

Lakin watanzania hawa wanahitaji masoko ya bidhaa zako. Masoko ya mazao na kazi za mikono. Masoko ya vivutio vya utalii. Kwa maana hiyo miradi yoyote yenye kuleta au ku saidia hayo mambo ni muhimu sana. Mfano ni mradi wa miundo mbinu. Bara baara, madaraja, viwanja vya ndege na ndege zenyewe. Ni muhimu sana. Miradi hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi wetu. Mtanzania mwenye akili timamu ata suport miradi ya aina hii kwa nguvu zake zote.

Lakin pia tunahitaji miradi ya kubadilisha afya zetu na maisha yetu. Miradi kama ya elimu bure kwa watoto wetu, miradi ya maji vijijin, na miradi ya hospitali au dispensary kwa kila kata.

Ni muhimu kwa ajili ya kubadili maisha ya mtanzania.

Sielewi kwann mtanzania wa kawaida haelewi maana ya investment kubwa zinazofanyika nchin.

Lakin pia ni vizuri kutambua kuwa kila sehem, kila mahali pakiweza kufikika then inakuwa rahisi kufanya shughuli yoyote ya kiuchumi kwa kila mwananchi wa kawaida.

Pia ni vizuri ikawa wazi kuwa labda awamu zijazo zinaweza kuwa na program ya kugawa hela au ajira kwa kila mtanzania. Lakin kwa sasa tunaomba haya niliyoyataja yafanyike kwa faida ya kila raia wa tanzania.
 
Hata uchambuzi wake hauna mantiki kwa sababu hakuna sekta iliyowekwa pembeni na serikali hii. Tofauti ni kiasi cha pesa tu. Lakini pia wasisahau kwamba kuna wakati nchi hii ilitenga bajeti kubwa kwenye sekta za elimu na afya kuliko sekta zingine.
Elimu(2005-2007); Afya(2007-2010); nishati mafuta, gesi na umeme(2011-2015); infrastructure(2015-present).
Sasa ubaya nini tukijipangilia mambo yetu? Serikali itawezaje kuajiri bila kuimarisha Macro-economy?
Chief kuajiri ni kazi ya sekta binafsi na sio serikali.

Kazi ya serikali ni kuweka mazingira bora kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi
 
Hivi ni kweli watanzania hatuelewi umuhimu wa hizi ndege kweli?

Hivi ni kweli kuna mtoto asielewa sababu ya kwanini baba yake amenunua lory la mizigo au basi la abiria badala ya kumfungulia duka kwanza.

Hivi ni kweli kuna mpangaji asie elewa umuhimu na faida ya kujenga nyumba yake.

Au mpaka leo kuna mtanzania ambae haelewi faida ya kujenga shule za sekondati kila kata nchi nzima badala ya kuboresha kwanza zile zilizo itwa shule za vipaji maalumu.

Hivi kuna mtanzania wa kawaida anae elewa hela za kuendesha elimu bila malipo na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu zinatoka wapi.

Inamana tunaka kusema kwamba ni afadhali hizo hela zilizonunua ndege zingegawanywa katika wizara mbali mbali zikatekeleze miradi ya maendeleo kuliko kunua ndege zitakazo leta faida zaidi hata kwa miaka kadhaa ijayo kisha faida ndo itumike.

Hivi kweli kuna mtu anaogopa kuanzisha mradi flani kwa kumuangalia flani anaelega lega kisha mtaji aliokua nao anakula wote?

Hivi kweli kuna mtu asiefahamu kwamba kuyumba kwa biashara kuna changizwa na vitu vingi ikiwemo poor managment

Hivi kweli tuache kununua ndege eti kwakua ethiopia shirika lao limeyumba basi nalakwetu litayumba bila kujiuliza sababu za kwanini limeyumba pengine ni poor managment je sisi tuki improve managment hatuwezi kufanya vizuri?

Mambo ni mengi sana ngoja niishie hapo kwanza.
Mifano yako yote haiko relevant na mada iliopo mezani
 
Hayo maneno hapo juu mabeberu wana andaa namna ya kuja kupiga hela. Yaani ikitokea kaja rais mwingine 2025 basi cha kwanza mafisadi na mabeberu watataka kuliua shirika la ndege kwa kujiuzia bei ya kutupwa kwa kisingizio cha eti kwenda kuzizika hizo hela kwenye non-income generating activities. Nadhani uchaguzi wa rais 2025 kigezo kimojawapo ni rais atakaye linda yale yote yaliyo asisiwa na Dkt Magufuli, iwapo mgombea urais akionekana ni mtaka kuuza ndege (mfano), basi huyo hafai. Na hapo historia inaweza kujirudia kwa sababu Mzee Mwinyi na Mkapa waliondoa misingi ya Mwl Nyerere, akaja Mzee Kikwete akajaribu kurudisha ila ilikuwa ilishaharibiwa kabisa, sasa Dkt Magufuli anarejesha tena. Iwapo hiyo misingi itavurugwa 2025-2030 itatuchukua marais watatu kumpata rais kama Dkt Magufuli, yaani mpaka 2050 ndiyo tena tunaweza pata rais mchapa kazi.
Ukweli ni kuwa hya mandege yanatutia hasara, nasapoti rais ajaye ayauze yote
 
I don't see a clear point here. Should Magufuli invest in water was that development compared to flights which in return makes money and employment to the people?
By the way, don't you see water projects going on everywhere? Don't you see number health facilities being in various stages of construction?

I guess this is not a Tanzanian post, a Tanzanian should have the answers to the doughts indicated in the post.

We Tanzania have decided to accept what Magufuli is doing. He is right by more than 80%.
We nae hutumii hta akili kufikiri

Hujui kuwa wananchi kupata maji safi ni advantage kwao kwani watatumia muda mwingi kwenye shughuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda huo kwenda kutafuta maji!

By the way utatumia vipi billions of money kwenye sekta ambayo inawakilisha only 1% ya population na kuitekeleza sekta sekta ya kilimo inayowakilisha 80% ya population?

Hyo itakuwa akili au matope?
 
Mkuu Mzalendo2015, kwanza namsupport rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, sio kwasababu ni homeboy wangu, bali namsupport kwenye yale mema na mazuri, lakini kwenye mabaya namkosoa sana tuu.

Watanzania tuko zaidi ya million 50, kati ya hao wanaomsuport Magufuli ni over 20 millions, Magufuli atahitaji kuwasupport individual wangapi?.

Support yangu kwa Magufuli sio ya kujikomba komba kutafuta uteuzi ndio maana kwenye mazuri ndio napongeza lakini kwenye mabaya, nakosoa.

Kwenye hili la ndege, nimechangia vya kutosha. Karibu pande hizi




P

Pascal,
Sidhani kama kwenye nafsi yako unaamini unachokisema na kukisimamia....!
Kwamba unamkosoa Magufuli kwa mabaya anayowafanyia Watanzania......Kwamba hujikombi kwa homeboy wako kweli...!!I can't believe you!

Sijawahi kusikia kauli yako thabiti kuhusu kile kilichompata Tundu Lissu ikiwa ni katika mabaya Utawala wa Magufuli umewatendea baadhi ya Watu wakiwemo Ben Saanane na Azory Gwanda....!

Nina hakika moyoni mwako leo hii ukisikia Ikulu imetangaza jina lako katika uteuzi wa Ukuu wa Wilaya hakika utafanya sherehe na utakuwa wa kwanza kufika Ikulu kula kiapo...!!!

Mimi napenda kukushauri wewe na Watz wengine tusemeni ukweli tu badala ya unafiki na kujikomba komba ili kupata vyeo...!!Hi itamsaidia home boy wako badala ya kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa huku akizidi kuiharibu nchi...!!!
 
Mtoa hoja anasema Tz kuna shida kubwa mno ya ajira na hivyo utegemezi unaongezeka sana. Ni kweli kabisa lkn suluhu yake ni nini? Watu wengi tunafikiri ya kuwa sekta ya utalii ikiendelezwa inaweza kutusaidia mno katika kupunguza tatizo la ajira.Huwezi kuwa na sekta imara ya utalii kama huna shirika la ndege .na hii dhana ya kutegemea shirika la jirani , jirani ambaye ni mshindani wako ndicho kitu kilichodumaza sana sekta utalii.Hivi umewai jiuliza kwanini Tz ambayo ni ya pili Kwa wingi na ubora wa vivutio vya utalii duniani lkn tunapokea watalii wachache hata tukujilinganisha na jirani tu.

Pili mtoa mada anasema badala ya kujenga sekta ya usafirashaji wa anga tuwekeze kwenye sekta ya Elimu,Afya ,Maji na kuboresha mazingira ya biashara. Mimi naona ni busara kujenga sekta zote hizo Kwa wakati mmoja.na ndicho kitu kinachofanyika muda huu.
Km issue ni ajira kwanini hyo mapesa ya ndege tusiwekeze kwenye kilimo ambapo inaweza kuajiri hadi 80%ya population

Agribusiness ndyo sekta pekee itakayotutoa hpa tulipo. Na sio hyo mandege
 
Siku akiingia Rais aliechaguliwa na watu, hiyo midege itauzwa ama ikodishwe kwa mashirika ya ndege yanayofanya biashara, kuliko hii biashara yetu ya kisiasa!
Hizi akili za kikagame za serikali kulipa gharama za kuendesha shirika lao la ndege ni ushamba wa kiwango cha changarawe, kisa sifa tu kwamba serikali inamiliki ndege nyingi bila faida.
kama wanabisha waruhusu CAG akague hesabu zake tuone miujiza!
 
Back
Top Bottom