Je, maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au vitu? Wachumi tusaidieni, uchumi wa Awamu ya 5, unalisaidia Taifa au utaliangamiza?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,601
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali, ambalo linatakiwa kujibiwa na wachumi wetu, kuhusiana na dhana ya maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu au ni maendeleo ya vitu?, na Je, sera za uchumi za serikali ya awamu ya Tano, ambazo zimejikita kwenye maendeleo ya vitu, badala ya maendeleo ya watu, zitalisaidia taifa kupata maendeleo ya kweli, au zitalisaidia taifa kupata maendeleo ya vitu, huku ukiliangamiza taifa katika maendeleo ya watu, na mwisho wa siku, Tanzania iwe ni nchi ya maendeleo makubwa ya vitu na miundombinu lakini watu wake wakaendelea kubaki kuwa masikini wa kutupwa kama Ethiopia?

Baba wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere alikuwa ni muumini wa falsafa ya "Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu na Sio Maendeleo ya Vitu" , falsafa ya Uchumi wa serikali ya awamu ya Tano chini ya Jemedari wake, Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, imejikita kwenye maendeleo ya vitu kwanza, kama kununua midege na kujenga miundombinu kwanza, halafu ndipo uje kwenye maendeleo ya watu, hivyo wachumi wetu, tusaidieni kutuelimisha, jee mfumo huu, wa kuanza na maendeleo ya vitu kwanza ndipo tuje kwenye maendeleo ya watu, utalisaidia taifa letu kuja kupata maendeleo ya kweli ambayo ni maendeleo ya watu, au na sisi Tanzania, baada ya kupata maendeleo ya vitu, ndege, reli, mabarabara mazuri, flyovers, etc, tutaishia kuwa kama Ethiopia ambayo ina miundombinu bora kabisa Barani Africa, huku ikiwa ndio nchi inayoongoza kukua kwa uchumi wa GDP ya zaidi ya 10% kwa mwaka, lakini uchumi wa mtu mmoja mmoja ukizidi kudidimia?

Kama kawaida yetu, maswali haya nayauliza genuinely kwa kutumia the right to expression provided na katiba yetu kwa kuuliza, jee awamu hii ya 5, inatumia falsafa gani ya kiuchumi?, jee uchumi huu wa kutanguliza kwanza vitu, unalisaidia taifa kwa kulipatia maendeleo ya kweli ya watu au unatupatia maendeleo ya vitu huku uchumi wa mtu mmoja mmoja ukizidi kudidimia, na kuangamia na mwisho wa siku tukajikuta uchumi, unalipaisha taifa kiuchumi, lakini kwa upande wa uchumi wa mtu mmoja mmoja, ukizidi kudidimia na kutufanya Watanzania tukaishia kuwa kama wa Ethiopians?

Kwa vile mimi sio mchumi, na tuna wachumi wetu lukiki humu mtandaoni, naombeni tusaidieni, tuelimisheni, kwa uchumi huu wa awamu ya 5, chini ya rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, Tanzania hapa tulipo, tumetoka wapi?, tuko wapi? na tunakwenda wapi?, are we realy heading to the right direction?
Declaration of interest Mimi sio mchumi, bali ni mwandishi wa habari wa kujitegemea nikijikita kwenye kuandika habari za kimaendeleo, developmental news, hivyo kama walivyo Watanzania wengi ambao sio wachumi, naona kama huu uchumi wa rais Magufuli, uchumi wa maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu kama ni kweli unalipatia taifa letu maendeleo makubwa na kulipaisha taifa letu kwenye kukua kwa uchumi, lakini at the same time, kwa upande wa uchumi binafsi, au uchumi wa mtu mmoja mmoja, sera hizi za uchumi wa viti, unatuzamisha kwenye lindi la umasikini zaidi uliotopea na kuwazamisha Watanzania wengi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja kwenye lindi la umasikini zaidi wa watu na utajiri wa vitu unless wachumi mtufafanulie huku tunakoona kama kuzama ni mtikisiko tuu kiuchumumi tukielekea kwenye stabilization, kama mtikisiko wa ndege kwenye runway inapotaka kupaa lakini iikiisha paa soon huwa ina stabilize na sisi hapa Tanzania, huku kukaza kwa vyuma na mdororo wa uchumi kwa biashara kufungwa, huu mtikisiko wa ujenzi wa uchumi wa vitu, huo ujenzi wa miundombinu, mabarabara, madege, SGR, Stigler na miundombinu mingine wezeshi ikikamilika, utausisimua uchumi wa mmoja mmoja na Tanzania na Watanzania kupata maendeleo makubwa ya kiukweli ya watu na kupaa kwa kiuchumi kutakako ipeleka Tanzania soon kuwa ni nchi ya uchumi wa kati tukielekea uchumi wa kwanza nasi kugeuka a donor country.

Tanzania Inayotegemea Kilimo
Tanzania ni nchi iliyokuwa ikitegemea kilimo kwa asilimia 80% lakini sasa kutokana na vijana wengi kukimbilia mijini, bado tunategemea kilimo kwa asilimia 67% yaani ni zaidi ya nusu ya Watanzania wanategemea kilimo. Jee kwenye falsafa ya Uchumi wa awamu ya tano wamefanya nini kuinua sekta ya kilimo ambayo ndio sekta tegemeo kwa uchumi wa walio wengi?.

Kukua kwa Uchumi kwa Asilia 7.2%
Uchumi wa Tanzania unakuwa kwa asilimia 7.2%, kuna watu wanashangilia sana ukuaji huu as if hii ndio mara ya kwanza kwa uchumi wa Tanzania kukua kwa zaidi ya asilimia 7%.
Hebu angalia hii taarifa GDP ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 10

2006-4.7%, 2007-5.5%, 2008 5.6%, 2009-5.4%, 2010- 6.4%, 2011- 7.9%, 2012- 5.1%, 2013- 7.3%, 2014- 7% 2015-7%, 2016- 7.2%, 2017-7.2%

Kikwete alipoingia alikuta GDP ya 4.7% na akainua hadi tukafikia GDP ya 7.9!. Magufuli kaingia kaikuta GDP ni 7.2% na sasa bado tuko 7.2%, hivyo katika ukuaji wa GDP ya taifa, kama rais Magufuli alikuta tuko 7.2%na sasa tuko 7.2% ameongeza nini?!, maana kwenye kusifia kukua kwa uchumi, kuna watu wanaimba tuu kama kasuku kuhusu huku kukua na kupaa kwa uchumi kuwa jamaa ameipaisha Tanzania, ameipaisha kutoka wapi alipoikuta na sasa tuko wapi?, na hapa sizungumzii kabisa deni la taifa!.

Jee Ukuaji Huu wa Uchumi wa asilimia 7.2% Umechagiwa na Sekta Zipi? na Unamfaidia Nani?.
Kwanza ni kweli uchumi wa taifa letu unakuwa kwa kasi ya 7.2%. Sasa twende kwenye sekta zinazochangia ukuaji huu wa uchumi ni madini, mawasiliano, utalii na fedha ambazo zimeajiri just 10% ya Watanzania wote. Sekta ya kilimo inayotegemewa, inakuwa kwa asilimia 1.3%, hii maana yake huu ukuaji wa uchumi wa asilimia 7.2%, unawafaidisha asilimia 10% ya Watanzania, lakini majority ya Watanzania wanaotegemea kilimo wakiendelea kupigika kwenye vyuma vilivyokaza hakuna mfano.

Tuangalie ni sekta zipi zinazochangia huu ukuaji huu wa GDP yetu ya 7.2%
  • agriculture: 25.1%
  • industry: 27.6%
  • services: 47.3%
Hii maana yake ni nini?. Kwa nchi ambayo uchumi wake unategemea kilimo kwa 67% ya watu wake, lakini mchango wa sekta ya kilimo ni 25.1% tuu kwenye ukuaji wa uchumi, unamaanisha wakulima ambao ndio wengi zaidi, hawa 67% wanagawana just 25.1 ya ukuaji wa uchumi, halafu hao wengine 23% wanagawana asilimia 74.9% ya uchumia wa taifa, hivyo walio wengi ni masikini wa kutupwa huku just 23% wakifaidi pande kubwa la keki ya taifa. Kama akitokea mtu atawaita hawa 67% wanaotegemea kilimo huku wanapigika kuwa hawa ni wapiga dili, mtu huyu atakuwa sii mzima and for sure, need his head be examined, asije akawa ni kichaa!.

Ukuaji Sekta ya Kilimo.
Angaliaji ukuaji wa sekta ya kilimo katika kipindi cha miaka 10
tanzania-agriculture-growth-q2-2016.jpg


Hivyo enzi za Kikwete kuna wakati kilimo kilichangia kupaisha GDP ya Tanzania kwa 7.6%, lakini ndani ya ukuaji huu wa GDP ya 7.2%, mchango wa kilimo ni 3.2%, japo ukuaji huu ni mdogo, lakini tumshukuru Magufuli, kwa sababu ilipoingia iliikuta sekta ya kilimo dholfu bin taaban.

Miradi Mikubwa ya Magufuli Ambako Mabilioni ya Fedha Yameelekezwa, Itasaidia Nini Watanzania?
Kwa vile asilimia 67% ya Watanzania wanategemea kilimo, na rais Magufuli kaja na falsafa ya Tanzania ya viwanda, ili hii Tanzania ya viwanda iwafaidie Watanzania walio wengi, then, Tanzania ya viwanda vya kweli ni Tanzania ya viwanda vya bidhaa za kilimo, Agro Processing Industries, jee serikali ya Magufuli, imefanya nini kuwekeza kwenye kilimo, ili kizalishe malighafi ya Tanzania ya viwanda?. Wachumi tusaidiane hapa!.

Where is The Blue Print, Mission, Vision na SMART Objectives za Tanzania ya Viwanda?
Tanzania ya Magufuli ni Tanzania ya viwanda, lakini where is the blue print ya hii Tanzania ya viwanda?, tunataka kujenga viwanda gani, vya kuzalisha nini, kwa kutumia malighafi gani, na nguvu kazi gani na vitajengwa wapi?. Mision na vision ya Tanzania ya viwanda ni ipi, na jee hii Tanzania ya viwanda inazo SMART Objectives?. Wachumi tusaidieni hapa ili tuielewe hii Tanzania ya viwanda tunayotaka kuijenga.

Tanzania ya Viwanda Itatumia Malighafi Gani?
Kupitia kazi zangu za uandishi wa habari, nimetembelea viwanda vingi vikiwomo viwanda vya Bakhresa vinavyozalisha unga wa ngano na vile vya vinywaji. Kwenye unga wa ngano, kuna wakati Tanzania tulizalisha ngano nyingi hadi kuuza nje kwenye yale mashamba ya Nafco kule Yaeda Chini. Lakini sasa asilimia 100% ngano yote inayozalishwa Bakhresa, Azania, inaagizwa kutoka nje na kwenye vinywaji, 90% ya pulp inaagizwa, only 10% ndio matunda ya ndani!. Kile kiwanda cha matrekta pale Kibaha ni assembly plant only!, everything is imported!, tunachofaidika labda ni ajira na wale kina mama ntilie kuuza chakula kwa wafanyakazi!. Sii wengi mnajua kuwa hadi toochpicks, Tanzania tunaagiza!, hivyo hii Tanzania ya viwanda, kama sio Tanzania ya viwanda vya bidhaa za kilimo, then tutajikuta tunajenga a China Town yenye assembly plants kutumia cheap labor, at the end of the day, everything goes back to kule mitaji ilikotoka, tukiachiwa Watanzania wachovu waliotumikishwa na wakatumikishika!.

Miradi Mikubwa ya Bombadia, Flyover, Reli ya SGR, Uwanja wa Chato Ina Faida Gani Kwa Taifa ?
Miradi mikubwa ya Bombadia, Flyover, Reli ya SGR, Uwanja wa Chato, Ujenzi wa Miundombinu mbalimbali, jee unasaidiaje hawa asilimia 67% wanaopiga kwa kilimo?!. Just imagine kama fedha hizo zingepampiwa kuboresha sekta ya kilimo ambayo ingewainua asilimia 67% ya Watanzania,
lakini miradi yote hii, itawafaidia zaidi wale wale asilimia 23%, wanaofaidika na asilimia 75% ya pato la taifa, au ni utekelezaji wa ule msemo " mwenye nacho, ataongezewa, na asiye nacho, atanyang'anywa hata kile kidogo alichonacho?!".

Jee Tanzania Tunataka Kupaa Kimaendeleo Kuifikia Ethiopia?.
Kati ya nchi 6 ambazo ni fastest growing economies ni Africa, Tanzania ni nchi ya 5, tumeipita Rwanda.
6. Rwanda
5. Tanzania
4. Mozambique
3. Cote d’Ivoire
2. DRC
1. Ethiopia.

Ethiopia ndio inayoongoza kwa ukuaji wana shirika kubwa la ndege, wana miundombinu ya majengo na mabarabara mazuri, wana treni ya umeme, uchumi wake unakuwa kwa zaidi ya asilimia 10% kwa mwaka, lakini angalia kiwango cha umasikini wa watu wake!, ile miili inayookotwa baharini na maporini kila uchwao, ni ya Waethiopia!. Jee Tanzania tunataka kuwa kama Ethiopia?.

Mwalimu aliusia kuwa "Maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu na sio maendeleo ya vitu", wachumi kwenye hili pia tusaidieni, ni miradi gani mikubwa ya awamu ya Magufuli ambayo imelenga kwenye maendeleo ya watu?. Are we really heading to the right direction economically?.
Ili Tuendelee Tuendelee, Jee Tunahitaji Nini Haswa, Kuwaendeleza Watu au Vitu?
Hili ni swali la msingi sana, ili taifa letu liendelee, jee tunahitaji maendeleo gani kwanza, tuanze kuendeleza watu kwa kuweka mazingira wezeshi ili watu wapate maendeleo, wajenge uchumi imara, wachangie kodi na wachangie uchumi wa taifa ndipo tutumie fedha za ndani kuleta maendeleo ya vitu, au tuanze kwa kukopa ili kujenga maendeleo ya vitu kwanza, hata kama ni kwa kukopa, tukiishapata vitu, ndipo tuje maendeleo ya watu?. What are our priorities?

Naomba kutumia falsafa mbili kutolea mifano Falsafa ya Mwalimu Nyerere, na Falsafa ya Adam Smith.

Falsafa ya Mwalimu Nyerere: Ili Tuendelee Tunahitaji Vitu Vinne,
  1. Watu-tunao
  2. Ardhi- tunayo
  3. Siasa Safi- tunayo?
  4. Uongozi bora-?
Kama vitu hivi vyote vinne tunavyo, sasa sisi Tanzania tumekosa nini?, kwa nini bado ni masikini?. Kati ya watu milioni 55 wa Tanzania, watu milioni 15 wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku.

Nyerere alipotangaza Azimio la Arusha la siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, alisema kazi ya kujenga ujamaa ingechukua miaka 30. Lakini siku anatangaza kung'atuka alikiri kuwa tumekosea!, akakiri kwa kusema "kufanya kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa"

Je, mnajua tulikosea wapi?. Tumsikilize mwanauchumi Adam Smith kwenye theory yake ambayo itaonyesha kosa la Nyerere.

Economic Theory Ya Adam Smith-Land, Labor, Capital & Entrepreneurship
Katika theory hii ya Adam Smith, inashabihiana na theory ya Nyerere kwenye watu na ardhi, na itatofautiana na Nyerere kwenye Siasa Safi na Uongozi Bora, Adam Smith anasema tunahitaji Capital na Entrepreneurship. Hivyo theory ya Nyerere kuweka siasa safi na uongozi bora ni kitu kile kile, kwenye theory ya Nyerere kulikosekana Capital, Nyerere alifanya kosa kubwa kwa kuamini fedha sii msingi bali ni matokeo, but in reality, pesa ni msingi sana wa kupata mitaji. Kama una watu, na ardhi, na una siasa safi, na uongozi bora, bila mitaji ya kuwawezesha hao watu kuitumia ardhi kuzalisha mali, tulitanga maji kwenye kinu kutegemea kilimo cha jembe la mkono, kutokuwa na mitaji ya kuchimba madini, mitaji ya kujenga viwanda. Mwinyi alipoingia, alifanya sera ya ubinafsishaji kwa uongo kuwa fedha za ubinafsishaji zitawekwa kwenye mfuko maalum wa mitaji kuwawezesha Watanzania ili waje kuwa wamiliki wa uchumi wao!, it was all a lie na hapa ndipo matabaka ya wenye nacho na wasionacho yalipoanzia!.

Magufuli Anafuata Sera Gani ya Kiuchumi na Anatupeleka Wapi?
Hapa ndipo mimi na akina sisi tusiojua uchumi, tunahitaji kuelimishwa na kueleweshwa, Magufuli anafuata mfumo gani wa kiuchumi na utatupekeka wapi?. Hili la kukopa dola milioni 500 kutoka Credit Suisse kwa ajili ya kujengea miundombinu, kwa riba ya asilimia 80% interest, ndani ya miaka 5! Hivyo tutalipa dola milioni 900!, kiukweli kabisa, mimi hili limenishtua na kuniogopesha!. Kama hili ni kweli tunakopa hivi, kwa mwendo huu, Magufuli atalikomboa taifa letu, au atalizamisha ndani ya mzigo wa madeni?. Kama fedha za bombadia, SGR, flyover, uwanja wa Chato, tunaelezwa ni fedha za ndani, lakini ukweli halisi ni fedha za mikopo ya miundondominu, tungeitumia kama capital ya kuwawezesha Watanzania kuinua sekta ya kilimo, tuzalishe zaidi, na kuwakopesha mitaji ya kumiliki viwanda vya aggro processing industries, tusiuze tena mazao ghafi, bali tuuze processed products ambazo zimekuwa na added value, kisha fedha zinazotokana na uzalishaji ndizo tukazitumia kujengea huu ufahari wa barabara na reli za kupaa, na kununua ndege taratibu, kuna tofauti gani?. Wachumi tuelimisheni nasi tuelewe, faida za bombadia, SGR, flyover, uwanja wa Chato na miundombinu mingine inayowafaidia only 10% ya Watanzania, ukilinganisha na kuwajengea uwezo wakulima asilimia 67% wanaotegemea kilimo?!. Wachumi wetu jamani tufafanulieni tuwaelewe, mnalipeleka wapi taifa letu hili changa lenye umri wa zaidi miaka 55!.

Nadhani ili tusiingizane kwenye mikopo chechefu ya deni la taifa, tufike mahali Tanzania tukitaka kukopa kuingiza kwenye deni la taifa, Bunge lielezwe tunakopa fedha za nini, kiasi gani kwa riba gani ili Bunge ndilo liidhinishe mikopo ya deni la taifa, tusije kujikuta taifa linabebeshwa mzigo mkubwa wa madeni, kumbe tumejengea white elephants na matumbo ya watu!

Kupanga ni kuchagua.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea.
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas.
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza ...
 
Wanabodi,

Hii ni thread ya swali, ambalo linatakiwa kujibiwa na wachumi wetu, Mwalimu Nyerere alituhusia "Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu na Sio Maendeleo ya Vitu". Wachumi wetu tusaidieni kutuelimisha, huu Uchumi wa Magufuli, Unalisaidia Taifa Kupata Maendeleo ya Watu, au Utatupatia Maendeleo ya Vitu Huku Uchumi wa Mtu Mmoja Mmoja Ukiangamia?.

Kama kawaida yetu kutumia the right to expression kuuliza, Jee awamu hii ya 5 ya rais Magufuli, inatumia falsafa gani ya kiuchumi?, jee uchumi huu wa Magufuli, unalisaidia taifa au unaliangamiza?. Kwa vile mimi sio mchumi, wachumi wetu, tusaidieni, tuelimisheni tunakwenda wapi?, are we heading to the right direction?.

Declaration of interest
:
Mimi sio mchumi, bali ni mwandishi wa habari wa kujitegemea nikijikita kwenye kuandika habari za kimaendeleo, developmental news, hivyo kama walivyo Watanzania wengi ambao sio wachumi, naona kama huu uchumi wa Magufuli, unatuzamiza na kulizamisha taifa, unless wachumi mtufafanulie huku kuzama ni mtikisiko tuu, lakini soo tutapaa!.

Tanzania Inayotegemea Kilimo
Tanzania ni nchi iliyokuwa ikitegemea kilimo kwa asilimia 80% lakini sasa kutokana na vijana wengi kukimbilia mijini, tunategemea kilimo kwa asilimia 67% yaani ni zaidi ya nusu ya Watanzania wanategemea kilimo. Jee kwenye falsafa ya Uchumi wa Magufuli, amefanya nini kuinua sekta ya kilimo ambayo ndio sekta tegemeo kwa uchumi wa walio wengi?.

Kukua kwa Uchumi kwa Asilia 7.2%
Uchumi wa Tanzania unakuwa kwa asilimia 7.2%, kuna watu wanashangilia sana ukuaji huu as if hii ndio mara ya kwanza kwa uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia 7%.
Hii ni taarifa GDP ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 10

2006 2007 2008 2009 2010 2011 2012 2013 2014 2015 2016 2017
4.7% 8.5% 5.6% 5.4% 6.4% 7.9% 5.1% 7.3% 7% 7% 7.2% 7.2%

Kikwete alipoingia alikuta GDP ya 4.7% na akainua hadi tukafikia GDP ya 7.9. Magufuli kaingia kaikuta GDP ni 7.2% na sasa bado tuko 7.2%, hivyo katika ukuaji wa GDP, Magufuli ameongeza nini?.

Ukuaji Huu wa asilimia 7.2% Umechagiwa na Sekta Zipi?.
Sasa twenda kwenye sekta zinazochangia ukuaji huu wa uchumi ni madini, mawasiliano, utalii na fedha ambazo zimeajiri just 10% ya Watanzania wote. Sekta ya kilimo inayotegemewa, inakuwa kwa asilimia 1.3%, hii maana yake huu ukuaji wa uchumi wa asilimia 7.2%, unawafaidisha asilimia 10% ya Watanzania, lakini majority ya Watanzania wanaotegemea kilimo.

Tuangalie ni sekta zipi zinazochangia huu ukuaji huu wa GDP yetu ya 7.2%
  • agriculture: 25.1%
  • industry: 27.6%
  • services: 47.3%
Hii maana yake ni nini?. Kwa nchi ambayo uchumi wake unategemea kilimo kwa 67% lakini mchango wa sekta ya kilimo ni 25.1% tuu kwenye ukuaji wa uchumi, unamaanisha wakulima ambao ndio wengi zaidi, hawa 67% wanagawana just 25.1 ya ukuaji wa uchumi, halafu hao wengine 23% wanagawana asilimia 74.9% ya uchumia wa taifa, hivyo walio wengi ni masikini wa kutupwa huku just 23% wakifaidi pande kubwa la keki ya taifa. Kama akitokea mtu atawaita hawa 67% wanaotegemea kilimo huku wanapigaka kuwa ni wapiga dili, mtu huyu atakuwa ni kichaa!.

Ukuaji Sekta ya Kilimo.
Angaliaji ukuaji wa sekta ya kilimo katika kipindi cha miaka 10
tanzania-agriculture-growth-q2-2016.jpg


Hivyo enzi za Kikwete kuna wakati kilimo kilichangia kupaisha GDP ya Tanzania kwa 7.6%, lakini ndani ya ukuaji huu wa GDP ya 7.2%, mchango wa kilimo ni 3.2%, japo ukuaji huu ni mdogo, lakini tumshukuru Magufuli, kwa sababu ilipoingia iliikuta sekta ya kilimo dholfu bin taaban.

Miradi Mikubwa ya Magufuli Ambako Mabilioni ya Fadha Yameelekezwa, Itasaidia Nini Watanzania?.
Kwa vile asilimia 67% ya Watanzania wanategemea kilimo, na Magufuli kaja na falsafa ya Tanzania ya viwanda, ili hii Tanzania ya viwanda iwafaidie Watanzania, then, Tanzania ya viwanda vya kweli ni Tanzania ya Agro Processing Industries, jee serikali ya Magufuli, imefanya nini kuwekeza kwenye kilimo, ili kizalishe malighafi ya Tanzania ya viwanda?. Wachumi tusaidiane hapa!.

Where is The Blue Print, Mission, Vission na SMART Objectives za Tanzania ya Viwanda?.
Tanzania ya Magufuli ni Tanzania ya viwanda, lakini where is the blue print ya hii Tanzania ya viwanda?, tunataka kujanga viwanda gani, vya kuzalisha nini, kwa kutumia malighafi gani, na nguvu kazi gani na vitajengwa wapi?. Mission na vission ya Tanzania ya viwanda ni ipi, na jee hii Tanzania ya viwanda inazo SMART Objectives?. Wachumi tusaidieni hapa ili tuielewe Tanzania ya viwanda tunayotaka kuijenga.

Tanzania ya Viwanda Itatumia Malighafi Gani?.
Kupitia kazi zangu za uandishi wa habari, nimetembelea viwanda vya Bakhresa vinavyozalisha unga wa ngano na vile vya vinywaji. Kwenye unga wa ngano, asilimia 100% ngano yote inaagizwa kutoka nje na kwenye vinywaji, 90% ya pulp inaagizwa, only 10% ndio matunda ya ndani!. Kile kiwanda cha matrekta pale Kibaha ni assembly plant, everything is imported, tunachofaidika labda ni ajira na wale kina mama ntilie kuuza chakula kwa wafanyakazi!. Sii wengi mnajua kuwa hadi toochpicks, Tanzania tunaagiza!, hivyo hii Tanzania ya viwanda, kama sio Tanzania ya viwanda vya bidhaa za kilimo, then tutajikuta tunajenga a China Town yenye assembly plants kutumia cheap labor, at the end of the day, everything goes back to kule mitaji ilikotoka, tukiachiwa Watanzania wachovu waliotumikishwa na wakatumikishika!.

Miradi Mikubwa ya Bombadia, Flyover, Reli ya SGR, Uwanja wa Chato Ina Faida Gani Kwa Taifa ?.
Miradi mikubwa ya Bombadia, Flyover, Reli ya SGR, Uwanja wa Chato, Ujenzi wa Miundombinu mbalimbali, jee unasaidiaje hawa asilimia 67% wanaopiga kwa kilimo?. Just imagine kama fedha hizo zingepumpiwa kuboresha sekta ya kilimo ambayo ingewainua asilimia 67% ya Watanzania,
lakini miradi yote hii, itawafaidia zaidi wale wale asilimia 23%, wanaofaidika na asilimia 75% ya pato la taifa, au ni utekelezaji wa ule msemo " mwenye nacho, ataongezewa, na asiye nacho, atanyang'anywa hata kile kidogo alichonacho?!".

Jee Tanzania Tunataka Kupaa Kimaendeleo Kuifikia Ethiopia?.
Kati ya nchi 6 ambazo ni fastest growing economies ni Africa, Tanzania ni nchi ya 5, tumeipita 6. 6. Rwanda
5. Tanzania
4. Mozambique
3. Cote d’Ivoire
2. DRC
1. Ethiopia.

Ethiopia wana shirika kubwa la ndege, wana miundombinu ya majengo na mabarabara mazuri, wana treni ya umeme, uchumi wake unakuwa kwa zaidi ya asilimia 10% kwa mwaka, lakini angalia kiwango cha umasikini wa watu wake!, ile miili inayookotwa baharini na maporini kila uchwao, ni ya Waethiopia!. Jee Tanzania tunataka kuwa kama Ethiopia?.

Mwalimu aliusia kuwa "Maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu na sio maendeleo ya vitu", wachumi kwenye hili pia tusaidieni, ni miradi gani mikubwa ya awamu ya Magufuli ambayo imelenga kwenye maendeleo ya watu?. Are we really heading to the right direction economically?.

Ili Tuendelee Tunahita Vitu Vinne, Vyote Tunavyo, Tumekwama Wapi?
Tulifunzwa, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne,
  1. Watu-tunao
  2. Ardhi- tunayo
  3. Siasa Safi- tunayo?
  4. Uongozi bora-?
Kama vitu hivi vyote vinne tunavyo, sasa sisi Tanzania tumekosa nini?, kwa nini bado ni masikini?.

Kupanga ni kuchagua.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea.
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...
Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed ...
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza ...
Paskali katika vitu hivyo vinne Tanzania inakosa kimoja, WATU. Ardhi tunayo, siasa safi tunayo, Uongozi bora tunao, Watu ndio hatuna!! Hili hata Rais Museveni aliwahi kutuambia.
 
Mimi si Mchumi ila nakubaliana kabisa na Baba wa Taifa kuwa Maendeleo yanapaswa kuwa ya Watu na sio vitu,Kuna faida gani ya kuwa na barabara nzuri, mandege mengi ili hali watu wako ni wajinga,maradhi yanawasumbua na mlo kwao shida?

Tuanze kuinua hali za watu katika Elimu, Afya na huduma zote stahiki, Mtu akiendelea ni lazima maendeleo ya vitu yatafata!

Naomba Wachumi mjitokeze kama mlivyoombwa na mtoa Uzi ili nasi tuweze pata elewa kama tunaelekea njia sahihi.
 
Nunua boeing and airbus na zifike hadi vijijini

Jenga madaraja yanayounganisha Dar es salaam na Tokyo

Weka reli zinazotumia bluetooth na infrared

Hakikisha kila mtaa kunakuwa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa

Weka flyovers kiasi kwamba unaweza kusafiri Dar hadi Kigoma juu kwa juu

Weka daraja la chini ya habari litalowezesha watu kusafiri hadi Zanzibar bila kuona bahari

Weka hadi paa la vioo kufunika miji mikubwa ili isiathirike na mvua na kusimamisha shughuli za watu (enzi zetu tulikuwa tunadanganywa Paris imefunikwa na vioo)

Mengine ongeza mwenyewe lakini sisi watu wa welfare economy mwishoni tutaka kuona hayo yote yamemwezesha vipi mwanachi wa kawaida kupata huduma bora za elimu (access and availability), huduma bora za afya (access and availability), access and availability ya maji safi na salama, food security, stable income and many more or else, investments husika are just bullshit!
 
Hakuna siku taarifa ya habari itapita bila ya issue ya maji safi na salama. Maji ndio kila kitu, miundo mbinu haijengwi bila maji, gari, treni, ndege, n.k. haviendi bila maji.

Chakula hakipikiki bila maji, asilimia kubwa ya mwili wa binadamu ni maji na unahitaji maji. Maji ndio kila kitu hata sayari mpya zinazofikiriwa kuhamiwa na binadamu kwanza wanaangalia uwezekano wa kuwepo maji. Serikali itatue tatizo la maji vijijini as a first priority.
 
Paskali katika vitu hivyo vinne Tanzania inakosa kimoja, WATU. Ardhi tunayo, siasa safi tunayo, Uongozi bora tunao, Watu ndio hatuna!! Hili hata Rais Museveni aliwahi kutuambia.
Kweli tuna upungufu wa watu ikiwa mpo mnaoweza kuiita chupi kofia kwa kuwa tu imevaliwa kichwani na baba mkwe.

Uongozi bora ni upi? Huu wa 'Mwalimu wa Nidhamu' kukataza rasta shuleni Jumatatu halafu Alhamisi 'Mwalimu Mkuu' anamuumbua hadharani as if alishindwa kujadiliana naye ofisini?

Museven huyu wa Uganda? Huyu anayerudisha nyuma umri na kubadili katiba kila uchao ili aendelee kubakia madarakani?

Ashakhum si matusi, mjinga wewe! Uongozi bora hauhitaji nguvu kuumimina mioyoni mwa wananchi. Kiongozi bora hang'ang'anii madaraka. Kiongozi bora huacha nyuma yake ushawishi na sio hoja ya nguvu. Nyuma ya kiongozi bora kuna mamia ya wafuasi walio tayari kuliendeleza aliloliacha kiongozi wao.
 
Mimi sifahamu sana mambo haya,ila niulize kitu,hivi mwalimu Nyerere alikuwa mchumi?na kama alikuwa mchumi vipi alifanikiwa sana kutufanya tuige falsafa zake za kuongoza uchumi?pili,wakati wa utawala wake uchumi wa mtu mmoja mmmoja ulikuwa juu kuliko ulivyo sasa?tatu,nyanja kama za madini zilikuwa na udhibiti wa kutosha kuliko udhibiti huu anaoufanya Magufuli?Nne,Ningeomba ufafanuzi kidogo hapo penye maendeleo ya vitu,ni hayo tu,mnisaidie hapo.
 
Mimi pia sio mchumi, ila kwahali inavokwenda, hauhitaji kuwa mchumi ili kuelewa uchumi wa nchi yetu. Zaidi sana naona mkulu ndo anawapa ushauri wachumi wetu
 
Back
Top Bottom