How the Dreamliner is Killing Tanzanians dream?

Nilivyo elewa mimi, anavyofanya jiwe ni sawa na kununua TV huku watoto wako wakilala njaa.
Kununua TV ya inchi 75 na huku hana hela ya kulipa ada ili watoto wasome shule zenye kiwango cha juu.
 
Wengi wetu hatujui kwamba bei ya 787-8 Dreamliner moja inakwenda kwa $224.6 million ambayo ni Karibia Tshs. 517billion, Sasa piga kwa hizo mbili karibia 1 Trillion tumelipa -- achilia mbali zile PangaBoy zetu sijui 4 hivi..

Kama hizi hela zingekwenda kwenye Elimu na Kilimo nawaambia mngeishangaa Tanzania Mpya tungeuza Mpunga na Mahindi China na huko nchi za kiarabu kama hatuna akili nzuri.vile. Kila mtanzania angecheka maana mtoto wake angepata Elimu nzuri, Waalimu wetu wangefundisha huku wanachekelea, Sisi wazazi tungelima kilimo cha kisasa huku tukiwa na Uhakika kwa soko la nje. Kifupi watanzania wengi msingekuwa mnatembea na sura za kukata tamaa, mngetembea huku mnachekelea maana kila mmoja angekuwa na hela mfukoni na ana uhakika wa milo 2.
 

That is the way common idiotic thinking would react. Nimekuuliza nchi gani ya afrika ambayo iko tofauti na Tanzania?
Cut long short ,have a look of top 10 robust economies in Africa. Just for your clue in link here below, you could very much start updating your patches and fix some bugs which would be having.
 
Acheni siasa nyepesi, hizo sekta za elimu na kilimo zimeshakula hela nyingi sana tangu tupate uhuru, na mpaka kesho zinaendelea kutengewa hela.

Kuna kikubwa zaidi kinachoangaliwa kimataifa, na kwa njia moja au nyingine kinalenga hata kuboresha zaidi elimu na kilimo.

Ukitaka kilicho bora ukubali kuingia gharama ili ukipate, kusingizia kwamba kipaumbele kikubwa kipo kwenye sekta ya anga ni kujaribu kujidanganya, kila sekta ina umuhimu wake, na hizi pesa zinazonunua ndege miaka ya nyuma zilikuwa zikifadhili maisha ya matanuzi ya wachache wanaoishi mijini.
 
Mkuu nisaidie kitu kimoja, wakati wa JK hazikumunuliwa ndege. Je waliwekeza kwenye hayo usemayo? Au hela hizi kipindi hili ndio zinapatikana? Hizi hela ambazo JPM ananunulia ndege,SGR,Stiglers hapo nyuma ziliwekezwa kwenye hayo unayoyasema? Mbona hakuna jipya?
 

Quoting Wikipedia now. Some academicians we are! Even your own source (which clearly admits it is subject to being corrected) shows differences between countries.
Am sorry; am wasting my time trying to make an incorrigible learn something.
Endelea kuimba mapambio Mkuu.
 
Mimi sina tatizo na kununuliwa ndege.

Nina tatizo na.

1. Serikali kuwa kigeugeu, mara inajiondoa kwenye biashara na kuuza mashirika ya umma, mara inajirudisha katika biashara. Kwa mwendo huu hatuendelei.

2. Serikali kujiingiza katika sekta yenye high risk kama usafiri wa anga. Huku ilitakiwa serikali iweke mazingira ya kufanya kazi mazuri tu na wawekezaji wawekeze. Marekani wanaounda hizo ndege hakuna shirika la ndege la serikali. Unafikiri wao wajinga? Kama biashara ya dege ina faida sana unafikiri wao nchi waliotengeneza hizo Boeing hawataki faida?

3. Serikali kuingilia biashara kwa namna ambayo imebana wafanyabiashara wengine. Serikali imeminya wazi fursa kwa wawekezaji wengine sekta ya usafiri wa anga ili kuifanya ATCL ing'are. Kimsingi imetengeneza monopoly ambayo itapandisha bei.

4. Serikali kukataza transparency kwenye sekta ya usafiri wa dege. Kuanzia ndege kununuliwa bila open tender mpaka CAG kukatazwa kukagua mahesabu ya ATCL. Kama kila kitu kiko sawa, kwa nini kuna usiri hivi?

5. Serikali kufanya biashara hii ni jambo la kisiasa. Jinsi rais anavyozidi kuhusishwa na ATCL na kuingilia biashara, ndivyo hata siku ATCL ikipata hasara watu watafanya mbinu za kihasibu za uongo na kweli kuonesha ATCL imepata faida, mradi tu rais asiadhirike.
 
Hayo uliyoyasema siyafahamu vizuri hivyo sina cha kuchangia
 
Hoja hapa si suala la ukusanyaji wa pesa hoja hapa ni suala la ipi iwe ni priority kwa Taifa.... kwa nini iwe ndege na isiwe kilimo na elimu? Je ni kipi kinachogusa watanzania wengi kwa mtazamo wako?
 
tutageukia
Hii ni ajabu sana, hivi inamaana hamuoni kabisa miradi ya maji ilivotapakaa nchi nzima? Hamuoni vituo vya afya vinavojengwa kwa kasi nchi nzima, hamuamini kuwa elim ni bure darasa la kwanza mpaka sekondari? Hamuoni wanafunzi wetu wakipokea mikopo kwa ajili ya elim ya juu? Hamauoni huduma za mama na mtoto? Hivi vyote mbn vinaenda sambamba na hayo maendeleo uliyoyataja ya watu? Kipi hivi leo kikichobaki nyuma? Eti baadae tutarudi kwny maendeleo ya watu, kweli??????
 

Lakini zipo nchi nyingi tu zenye mashirika ya ndege yanayomilikiwa na serikali na mashirika hayo yanafanya vizuri tu kibiashara.

Hata ukiangalia orodha ya mashirika bora ya ndege duniani, kwa mwaka huu wa 2029, 10 bora imetawaliwa na national carriers.

Hata ukiangalia orodha za 10 bora za miaka iliyopita, hali ni ile ile.
 
P
 
Zitaje hizo nchi, tuangalie average GDP Per capita ya wananchi wa hizo nchi, halafu tulinganishe na GDP Per Capita ya Tanzania.

Nilikuwa nasikiliza interview moja ya Ethiopian Airlines CEO, alikuwa anahojiwa BBC kipindi cha "Business Daily".

Akaulizwa, mmefanikiwa sana hapa nyuma, katika biashara ambayo ina ushindani sana, nini siri ya mafanikio yenu?

Akajibu kuna mengi, lakini kikubwa kabisa ni jinsi serikali ilivyoachia shirika liendeshwe kitaalamu, na wataalamu, si kisiasa, na wanasiasa.

Nikaona kwa kanuni hii, shirika letu la ndege linavyoendeshwa kisiasa na wanasiasa, tuna safari ndefu sana.
 

Your writing as per above tells the volume. Some would even wonder whether you are real academician or rogue one. And if happens that you are one them, then I pity your products.

Leave alone the writing. I was of the view that probably you would go further down the road in details arguing using data available, instead however, you keep tweaking the words and phrases.

If you are manned up, click the link below and then hover over the countries, you would probably get the bugs fixed.

 
Hoja hapa si suala la ukusanyaji wa pesa hoja hapa ni suala la ipi iwe ni priority kwa Taifa.... kwa nini iwe ndege na isiwe kilimo na elimu? Je ni kipi kinachogusa watanzania wengi kwa mtazamo wako?
Anyway,kwahio kwenye kilimo na elimu hela haziendi?
 
Umejibu jambo moja tu kati ya matano. Ina maana manne mengine unakubaliana nami?
 

Actually hoja yangu ilikuwa ni kwamba, hakuna ubaya nchi kuwa na national carrier.

Nchi nyingi tu zina national carriers na hayo mashirika yanafanya vizuri tu [hata kama Marekani wao hawana national carrier].

La msingi ni jinsi na namna ambavyo shirika linaendeshwa.

Likiendeshwa kitaalamu bila uingizwaji wa siasa, shirika linaweza kufanya vizuri kabisa na mifano hai ipo.
 
Hebu tuwekee hapa hiyo ilani tuone kama kweli ilikuwa ni sehemu ya ilani yenu
 
Umejibu jambo moja tu kati ya matano. Ina maana manne mengine unakubaliana nami?

Sina tatizo na hayo mengine uliyoyaainisha.

Nami kimsingi mtazamo wangu ni kama huo wako.

Hapo kuhusu Marekani nilitaka tu kuonyesha kuwa zipo nchi ambazo zina National carriers na hizo carriers zinafanya vizuri kuliko hata mashirika binafsi ya Marekani kama Delta, American, United, nk.

Ushawahi kupanda Delta?

Binafsi huwa naona ukipanda Qatar, Emirates, au Hata Lufthansa tu halafu uje upande Delta, ni kama una downgrade.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…