Zitaje hizo nchi, tuangalie average GDP Per capita ya wananchi wa hizo nchi, halafu tulinganishe na GDP Per Capita ya Tanzania.
Nilikuwa nasikiliza interview moja ya Ethiopian Airlines CEO, alikuwa anahojiwa BBC kipindi cha "Business Daily".
Akaulizwa, mmefanikiwa sana hapa nyuma, katika biashara ambayo ina ushindani sana, nini siri ya mafanikio yenu?
Akajibu kuna mengi, lakini kikubwa kabisa ni jinsi serikali ilivyoachia shirika liendeshwe kitaalamu, na wataalamu, si kisiasa, na wanasiasa.
Nikaona kwa kanuni hii, shirika letu la ndege linavyoendeshwa kisiasa na wanasiasa, tuna safari ndefu sana.