Sina tatizo na hayo mengine uliyoyaainisha.
Nami kimsingi mtazamo wangu ni kama huo wako.
Hapo kuhusu Marekani nilitaka tu kuonyesha kuwa zipo nchi ambazo zina National carriers na hizo carriers zinafanya vizuri kuliko hata mashirika binafsi ya Marekani kama Delta, American, United, nk.
Ushawahi kupanda Delta?
Binafsi huwa naona ukipanda Qatar, Emirates, au Hata Lufthansa tu halafu uje upande Delta, ni kama una downgrade.
Hizo nchi za ndege ulizozitaja, Qatara, Emirates, Germany, kugeza mambo yao ni kugeza tembo kunya, tutapasuka msamba.
Mimi kiujumla napendelea maendeleo yanayowagusa watu wengi, tena wengi wa hali ya chini, kwa mpigo.
Kiuchumi, unaweza kutengeneza mzunguko wa hela vizuri zaidi kwa kuongeza purchasing power ya watu wa chini, halafu watu wa chini wakaongeza consumption, halafu enterpreneurs wakaongezeka, halafu wakajikusanya nguvu mpaka kuanzisha mashirika ya ndege yao, bila kuhitaji serikali ichukue risk kubwa.
Serikali inakuwa na jukumu la kuweka legal framework nzuri tu, kuweka amzingira ya biashara mazuri tu, kuweka level playing field, kuweka misingi ya free trade inayoendana na no barrier to entry or exit the market etc.
Sasa hivi serikali imejiingiza kwenye biashara kwa mabavu, imefanyia mpaka fitina mashirika binafsi. Hili linasababisha monopoly. Monopoly itapandisha bei halafu biashara ikose innovation.
Pia, hata shirika likipata hasara, vitabu vitapikwa, CAG atakatazwa asikague vitabu, zitaletwa figisu kibao. Kwa sababu shirika lishakuwa project ya kisiasa ya rais, na rais akitaka kuadhirika lazima asitiriwe by hooks or crooks.
Ndiko tunakoelekea.