Housigeli anataka kuniharibia ndoa yangu jamani

kuna mahali wamama tunajisahau sana napo ni hapo kwa kumuachia h'gal kila kitu akifanye, mpaka kutandikiwa kitanda jamani, hapana!, QUOTE]

Na je,
ukiwa na h'boy..inakuwaje? Huyo baba bado atamchukua? ( im playing the devil's advocate)
 
kwa nilivyofahamu ni kuwa mama mkwe ndio ameyasema hayo, sio baba ndio kamzimia Hg kama ndio hivyo hiyo mbona kazi rahisi, ila kama ni baba anafikisha ujumbe kiaina then mama inabidi ukae mkao mzuri, inawezekana umejisahau kweli kwahiyo anakushtua basi ni vema ulijue na uanze kulifanyia kazi, punguza mizunguko baada ya kazi ili uwahi kurudi home angalau uandae chakula cha jioni na kusafisha chumba chako, pia jitahidi asubuhi uwahi kuamka mapema na kuandaa kifungua kinywa chako na cha mzee, weekend na holiday mama punguza mitoko ya kwenda kwa mashoga, kitchen party, send off, nk

huwa tunakimbilia kuwalaumu Hg's lakini pia akina mama tunamapungufu, hiyo ni alarm huna haja ya kupanik tulia angalia makosa yako na fanya uchunguzi kama ni kweli yametoka kwa mama mkwe au mzee anawakilisha indirect

kama ni suala la mama si tatizo unajua akina mama wanahitaji kueleimshwa maana zama zao ilikuwa mama ni wa nyumbani sio barabarani, tofauti na sasa, na pia lazima ujue kuwa kadri umri unavyoenda na uwezo wa kufikiri unakuwa mdogo na ndio maana tunaambiwa kuwalea wazazi ni kazi, inabidi ukae na mumeo, muelimishane juu ya hili, ili asilichukulie kama ni point na kama kweli unajitahidi yeye anajua zaidi, na faida ya kutoka kwako atakuwa anaijua ila saasa kama ni barabarani for nothing then mamaaa take care!!!
 
labda nikushtue tu, mama mkwe wangu ni watype hiyo, nilivyoona ameanza longolongo nimefanya kazi ndogo tu kumuweka sawa kwa vizawadi, leo - kanga, kesho - kitenge, nk mwenyewe kanyamaza maana kaona umuhimu wa mimi kuwa barabarani.
sasa dada kama mkono wako mfupi, hata mumeo haoni kinachokutoa nyumbani hapo jiandae kuuza nyumba!!!
 
nakushauri mfukuze mara moja. kuna ndugu yangu alikuwa na hausi geli toka iringa, alikuwa mdada. akapata safari, akamwacha na mmewe na watoto. housegirl alianza kumwekea dawa yule mbaaba, dingi likaanza kumchukia mkewe aliyemzalia watoto bila kupenda, siku wakamkamata housegirl akiletewa dawa na rafiki yake toka iringa ili ammalize kabisa yule mama mwenye nyumba achukue ndoa. baba likuwa anafanya mapenzi nae kwa nguvu za dawa, akampenda housegirl kuliko mkewe. alipokuja kugundua na dawa imeisha nguvu, alimpeleka hadi polisi, dingi lilitaka kumkatakata vipande kwasababu alikuwa ameshaitesa sana ndoa, ndani kulikuwa kama jehanamu kwa muda mrefu katika ndoa. msichana alifukuzwa kama mbwa, sasa hivi anafanya kazi kwenye mgahawa fulani hapa mtaani. watu hawana hata hamu nae, wanajuta kumfahamu. ukitaka kuwa na house girl, chukua kale kanakomaliza tu shule kule iringa au mikoa mingine,kakianza kuwashwa kidogo tu, mpe zawadi na nauli aende nyumbani akasalimie wazazi moja kwa moja.
 
nakushauri mfukuze mara moja. kuna ndugu yangu alikuwa na hausi geli toka iringa, alikuwa mdada. akapata safari, akamwacha na mmewe na watoto. housegirl alianza kumwekea dawa yule mbaaba, dingi likaanza kumchukia mkewe aliyemzalia watoto bila kupenda, siku wakamkamata housegirl akiletewa dawa na rafiki yake toka iringa ili ammalize kabisa yule mama mwenye nyumba achukue ndoa. baba likuwa anafanya mapenzi nae kwa nguvu za dawa, akampenda housegirl kuliko mkewe. alipokuja kugundua na dawa imeisha nguvu, alimpeleka hadi polisi, dingi lilitaka kumkatakata vipande kwasababu alikuwa ameshaitesa sana ndoa, ndani kulikuwa kama jehanamu kwa muda mrefu katika ndoa. msichana alifukuzwa kama mbwa, sasa hivi anafanya kazi kwenye mgahawa fulani hapa mtaani. watu hawana hata hamu nae, wanajuta kumfahamu. ukitaka kuwa na house girl, chukua kale kanakomaliza tu shule kule iringa au mikoa mingine,kakianza kuwashwa kidogo tu, mpe zawadi na nauli aende nyumbani akasalimie wazazi moja kwa moja.



kanaweza pia kakawa kajuzi ka mambo kupitiliza, na mpaka ushtukie utakuta walianza kitambo.
 
ujuzi huwa sio wajuzi, kwasababu wengine ni watoto hata hawana uzoefu.labda kama una lihousegirl likubwa sana ndo linaweza kuwa lilikubuhu. wengi wanakuwa walimaliza lasaba wakaja kuvunjia ungo ndani kwetu. hivyo sio wajuzi,ila wana dawa.
 
ujuzi huwa sio wajuzi, kwasababu wengine ni watoto hata hawana uzoefu.labda kama una lihousegirl likubwa sana ndo linaweza kuwa lilikubuhu. wengi wanakuwa walimaliza lasaba wakaja kuvunjia ungo ndani kwetu. hivyo sio wajuzi,ila wana dawa.

uoga bwana kitu cha ajabu sana.
mie nasema huyo mwalikibeto aletwe kwangu kwani nina upungufu wa hausigeli kiasi kwamba hata limbwata siku hizi siwekewe
 
ujuzi huwa sio wajuzi, kwasababu wengine ni watoto hata hawana uzoefu.labda kama una lihousegirl likubwa sana ndo linaweza kuwa lilikubuhu. wengi wanakuwa walimaliza lasaba wakaja kuvunjia ungo ndani kwetu. hivyo sio wajuzi,ila wana dawa.


kukubuhu kwa mtu hakuhitaji umri ndugu, unaweza kukuta hako ka darasa la saba kamekubuhi kuliko hilo limama unalolizungumzia.
 
Nzuri ngoja ninywe kiloba nikushauri.
Masanilo,Brenda,Mwanajamii,Nyamayao,WOS,Mbu,Msanii,Joyceline mnaweza mkaendelea na mjadala mwenzenu huyo jahazi linazama h/g katoa TG kwa baba mwenye nyumba.


Nani kakuambia kwamba laitoa Tig kwa baba mwenye nyumba,soma tena uelewe vizuri.

namshauri huyu mama punguze jazba amuite mama mkwe wake, mume wake na huyo dada wayaongee kwa uwazi bila kuuma uma maneno, halafu kama kuna sehemu alikuwa anakosea kama binadamu na mama mwenye nyumba ahakikishe anaparekebisha, akiona kuna uhusiano kati ya baba na binti amrudishe binti kwa wazazi wake amkabidhi na aeleze.
Kuna mtu niliona amemshauri aondoke aondoke aende wapi? yeye ni mwanamke anatakiwa awe strong apiganie nyumba yake na penzi lake, bora mume hana tatizo hao wengine wasikunyime usingizi
Ila ukumbuke responsibilities zako as a wife.
 
Mwaka huu 2009 tunakumbuka miaka karibu 205 ya kusimamishwa kwa
biashara ya utumwa iliyohusisha meli za kiingereza na nchi nyinginezo.
Ingawa miaka 200 imepita, je utumwa huo twauendeleza wenyewe?
Utumwa mfumo wa unyonyaji wa kutumia nguvu za watu bila malipo wala
hiyari yao wenyewe au kumiliki mtu/watu wengine kama bidhaa. Mara
nyingi tunapozungumzia utumwa tunafikiria kuhusu biashara ya pembe
tatu tuliyofundishwa na waalimu wetu wa siasa au historia shuleni.
Tulifundishwa kwamba watumwa walikamatwa kutoka vijijini mwao na
kuuzwa kwa wafanya biashara ambao waliwapiga mnada gulioni Bagamoyo,
Mombasa na Unguja. Pili tunaelezwa kuwa watumwa walisafirishwa kwenda
visiwa vya Shelisheli hadi Karibea na Amerika kwenye mashamba ya miwa
na kadhalika. Baada ya hapo waalimu wetu walitueleza jinsi watumwa
walivyoteseka huko mashambani na wanyapara wao walivyowapiga,
kuwafanyisha kazi na kuwavuna. Malipo yao yalikuwa sembe na maharage
kidogo ili kesho tena waje kulima.

WATUMWA TUNAO MAJUMBANI MWETU - Bidii - Karibu Tujenge Nchi | Google Groups
 
ahahahaa...ebwanaeheeee..duuuuuh...sasa mama kevini wa tabataaaa....kwani wewe ulikuwa hujui kuwa adui wa mwanamke mwanamke mwenziooo??...kalaghabahooo...hiyo inakula kwako usipokuwa makini na kufuata ushauri wangu...na kwa taarifa yako shukuru mungu huyo hauzi geli ****..angekuwa mjanja ungeshakuta kamlisha tigo baba watoto wako na ukistuka tuu...unatimuliwa na mmeo...USHAURI NASAHA SASA...ilitokea kwa mama m1 mjanja akagundua kuwa mmewe anamla h/g...sikumoja mama akasubiri baba/mmewe amesafiri...akampigia simu mmewe akamwambia kuwa mzazi wa h/g anaumwa sana lazma ampeleke kwao mitaa ya matombo huko morogoro....mshua akamwambia mkewe asubiri anarudi kesho yake...mama akasema poa...kesho yake akaamka asubuhi akamwambia hosegal kuwa amepigiwa cmu kuwa hali ya mama yake kijijini siyo..kama vipi fasta park vitu vyako tunatimuka mida ya saa 4 asubuhi..hg akaingia laini...safari ikaanza..baba na yeye akawa anarudi zake nyumbani amuwahi mkewe ili ampeleke hg kwao...wakapishana njiani...mama kufika kijijini kwa hg akamwaga mchele na mboga yote kwa mama wa housegal kuwa NIMEMRUDISHA MWANAO HANIFAI ANAKULA URODA NA MUME WANGU...KAMA ANANIDAI ASEME NI KIASI GANI NIMLIPE...wakamalizana na zoezi likaisha.....miezi mitatu baadae baba akaulizia kwa mkewe vip maendeleo ya mgonjwa mama yake na hg...wife akamtolea UVIVU mmewe kwa kumpa ukweli kuwa ulikuwa unamla-uroda ndio maana nimemuondoa na hatorudi tena...SOMO LA KUJIFUNZA....wanawake wetu mmekuwa magoigoi kupindukia na mnawaachia mabek3 majukumu ya msingi ya ndoa zenu..KWANI HAMJUI SIE NI KAMA WATOTO NA TUNAHITAJI KUDEKEZWA NA NYIE WAKE ZETU?...kwa hiyo hg akinidekeza ndo anakuwa mama mlezi wangu...HABARI NDO HIYOOOO.
 
Nani kakuambia kwamba laitoa Tig kwa baba mwenye nyumba,soma tena uelewe vizuri.

namshauri huyu mama punguze jazba amuite mama mkwe wake, mume wake na huyo dada wayaongee kwa uwazi bila kuuma uma maneno, halafu kama kuna sehemu alikuwa anakosea kama binadamu na mama mwenye nyumba ahakikishe anaparekebisha, akiona kuna uhusiano kati ya baba na binti amrudishe binti kwa wazazi wake amkabidhi na aeleze.
Kuna mtu niliona amemshauri aondoke aondoke aende wapi? yeye ni mwanamke anatakiwa awe strong apiganie nyumba yake na penzi lake, bora mume hana tatizo hao wengine wasikunyime usingizi
Ila ukumbuke responsibilities zako as a wife.
Kuwaita wote nadhani sio good idea,house girl awepo kwenye hicho kikao ili iweje?Hapana...ni vyema yeye aongee na mama mkwe pekee na pia cha muhimu zaidi ajirekebishe.

Kwa mrengo mwingine inawezekana mme wake pia katumia hekima tu kumweleza kwa namna inayoonyesha kama vile yeye binafsi hajali,lakini fahamu may be ameshindwa tu kueleza direct kuwa ata yeye hilo linamkera na labda kweli kuna issue inayoendelea kati ya huyo mme na house girl,kuna watu wengi ambao uwa hawawezi kumweleza mtu mapungufu yake direct kwa kuogopa kumuumiza na kuzua mgogoro ambao hauhitaji kwa wakati huo,......think big

Hii tabia ya kubinafsisha shughuli zote za nyumbani kwa house girl inakera sana, kumbuka kila binadamu ana uzuri na mvuto wake tofauti na mwingine,never underestimate anybody!!
 
WomenofSubstanc;430077]
Na je,
ukiwa na h'boy..inakuwaje? Huyo baba bado atamchukua? ( im playing the devil's advocate)

Ukiwa na house boy huyu sasa si anakuwa wa mama kipoozeo mzee anapo chelewa kurudi au anasafiri safiri mara kwa mara au anarudi amechoka...sasa ndipo utakapo iona kazi ya house boy.
 
Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa

Anti/kaka jamii

habari yako. Nategemea mzima wa afya na hutasita kunisaidia kunipa ushauri unaonifaa. Mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili. Tangu nimeolewa miaka sita iliyopita, nimekuwa na msichana wangu wa kazi mmoja ambaye nimempenda sana hasa kwa kuwalea vizuri watoto wangu na kuwa mwepesi wa kazi. Kutokana na kuishi vizuri na ‘housigeli’ huyu, amekuwa kama mtoto wa nyumbani na hata ndugu zangu na wa mume wangu wanampenda sana na wamemzoea kupita kiasi.

Tatizo hili la kuwazoea ndugu wa mume wangu sasa naona linataka kuharibu ndoa yangu kwani huyu msichana ameanza tabia mbaya na amemweleza mkwe wangu kuwa mimi situlii nyumbani na sina muda wa kumshughulikia mume wangu kwani kazi zote anafanya yeye, mimi kazi yangu kusafiri na kushinda kazini. Huyu mama mkwe wangu kusikia hayo, amekuja juu na sasa anamshinikiza mume wangu aniache eti nashindwa kuhudumia nyumba na badala yake amuoe ‘housigeli’. Mume wangu ameshtuka na amenieleza kila kitu hali iliyonikasirisha sana.

Sasa naomba ushauri wako kwani mama mkwe bado yupo kwangu, je, nifanyeje kabla hajaondoka kurudi kwake? Mama Kelvin Tabata, Dar es Salaam. Mama Kelvin pole sana kwani inaonekana huyo mama mkwe wako hajaelimika vya kutosha. Uzuri wa mwanamke haupimwi kwa kazi za nyumbani pekee, bali kuna mambo mengi na mkwe wako anapaswa kutambua kuwa wewe unafanya kazi hivyo huwezi kukaa nyumbani muda wote na ndiyo sababu ukatafuta msaidizi.

Lakini pia ni vyema ukiwa nyumbani ufanye kazi zilizopo ikiwamo kumpikia mumeo na kumhudumia ipasavyo. Usiwe na hasira za haraka kwa msichana wako wa kazi kwani inawezekana aliulizwa kimtego naye akajibu vizuri tu lakini mkweo akawasilisha kwa mumeo vibaya. Nadhani mumeo pia anapaswa amweleze mama yake kwa upole kuwa wewe unafanya kazi na huwezi kufanya kazi zote za nyumbani. Pia amweleze kuwa huyo msichana wa kazi kamwe hawezi kuwa mke wa mtoto wake.

Naamini mtoto wake akimwelimisha na akawa na msimamo, mama mkwe wako ataelewa au hata kama hataelewa, atashindwa kuendelea kusisitiza anachotaka. Ni vyema pia ukakaa na mshichana wako na kumhoji ilikuwaje hata wakazungumza hayo na mkweo na ukiona kama alichokonolewa basi mtahadharishe akae mbali na mama mkwe na asiwe mwepesi kueleza mambo ya ndani ya nyumba kwa mkweo.

Hata hivyo fanya uchunguzi wako kwa siri na ukiona msichana wako anapalilia ili aolewe yeye, basi ni vyema ukatafuta msichana mwingine wa kazi na huyo kumwondoa ili asije kuharibu ndoa yako. Haina haja kugombana na mtu yoyote kwani naamini huyo mkweo ataondoka na nyinyi mtaendelea na maisha yenu. Pia jifunze kuvumilia kwani wakwe wengine uelewa wao ni mdogo.


We mama, ebu mtimue huyo HG chap chap!!
 
ndoa nyingi zinavyunjwa na mahouse girl. mi nimezishuhudia nyingi tu. nyie chezeeni shilingi ******.
 
Mimi sikusoma yote yaliyoelezwa na wanaJF huko kabla. Ila Mama Mia nina wasiwasi umekasmisha majukumu yako kwa house girl! Wanawake hasa kama ukivyosema kuwa ni mtu wakusafirisafiri unahatarisha ndoa yako sana. Unapokaa na msaidizi wako kuna mambo ambayo unatakiwa uwe na uhakika kuwa ni lazima ufanye even you are tired! Kumwandalia mumeo yafuatayo, kumpokea mumeo arejeapo (kumfungulia mlango na kupokea hata malboro alokuja nayo), maji ya kuoga, chakula, na kuhakikisha yuko smart kama vile shati na suruali ni safi na hata chupi yake ni safi, tai kama ni muhimu siku hiyo. Unapomwachia house girl kufanya haya unampa nafasi yeye kutangaza biashara yake.
Mfano, wewe umewahi nyumbani, bwana anakuja anafunguliwa mlango na house girl na labda alikuwa bafuni anajitupia ka kanga kamoja ka India, ameshakula blue band na uji wa mtoto hapo kwako na mbaya zaidi hajui kuwa ni kosa kuwa hivo. Mama wewe umelala chumbani, umechoka! Ooo baba karibu, pole na kazi, maji yapo bafuni nk. Unategemea nini? Mtu mzima anajiapiza kuwa hapo lazima amege japo kidogo!
Nitaendele jumatatu natoka kidogo. Weekend njema
 
Huyo House girl sio anataka kuharibu ndoa, bali anataka kuitengeneza. Inaelekea mama ulishachukulia mambo mengi for granted. Kwa sababu h.girl anafanya kazi vizuri ukabweteka na kusahau baadhi ya majukumu yako nyumbani. Chunguza vema unaweza kukuta kuwa hakusaidii kuosha nguo za mzee tu, bali na mengne mengi anakusaidia

Ni kweli kina mama wakati mwingine wanajisahau hasa baada ya kuzoeana na mume wako.
Wanaume huponzwa na vitu vidogo sana hasa ukizingatia kuwa wao huwa ni moto mara moja, wakati mwingine h/g anakuwa mchangamfu kuliko hata mama mwenye nyumba na heshima zaidi kwani ana mheshimu bosi wake na mambo huanzia hapo.Kwa house Boy mara nyingi wanachangamkia tenda za maboss hasa mzee anapokuwa busy sana na kujisahau kuwa yeye ni baba,mume wamtu, na bosi ushauri tubalance mabo jamani ili tuponye ndoa zetu.
 
guys mko sawa lakini wake wengine wanakuwa hivyo kutokana na waume zao ...sasa hapa tuanzaje.....wabadilike kwanza
 
Back
Top Bottom