Housigeli anataka kuniharibia ndoa yangu jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Housigeli anataka kuniharibia ndoa yangu jamani

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Apr 22, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa

  Anti/kaka jamii

  habari yako. Nategemea mzima wa afya na hutasita kunisaidia kunipa ushauri unaonifaa. Mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili. Tangu nimeolewa miaka sita iliyopita, nimekuwa na msichana wangu wa kazi mmoja ambaye nimempenda sana hasa kwa kuwalea vizuri watoto wangu na kuwa mwepesi wa kazi. Kutokana na kuishi vizuri na ‘housigeli’ huyu, amekuwa kama mtoto wa nyumbani na hata ndugu zangu na wa mume wangu wanampenda sana na wamemzoea kupita kiasi.

  Tatizo hili la kuwazoea ndugu wa mume wangu sasa naona linataka kuharibu ndoa yangu kwani huyu msichana ameanza tabia mbaya na amemweleza mkwe wangu kuwa mimi situlii nyumbani na sina muda wa kumshughulikia mume wangu kwani kazi zote anafanya yeye, mimi kazi yangu kusafiri na kushinda kazini. Huyu mama mkwe wangu kusikia hayo, amekuja juu na sasa anamshinikiza mume wangu aniache eti nashindwa kuhudumia nyumba na badala yake amuoe ‘housigeli’. Mume wangu ameshtuka na amenieleza kila kitu hali iliyonikasirisha sana.

  Sasa naomba ushauri wako kwani mama mkwe bado yupo kwangu, je, nifanyeje kabla hajaondoka kurudi kwake? Mama Kelvin Tabata, Dar es Salaam. Mama Kelvin pole sana kwani inaonekana huyo mama mkwe wako hajaelimika vya kutosha. Uzuri wa mwanamke haupimwi kwa kazi za nyumbani pekee, bali kuna mambo mengi na mkwe wako anapaswa kutambua kuwa wewe unafanya kazi hivyo huwezi kukaa nyumbani muda wote na ndiyo sababu ukatafuta msaidizi.

  Lakini pia ni vyema ukiwa nyumbani ufanye kazi zilizopo ikiwamo kumpikia mumeo na kumhudumia ipasavyo. Usiwe na hasira za haraka kwa msichana wako wa kazi kwani inawezekana aliulizwa kimtego naye akajibu vizuri tu lakini mkweo akawasilisha kwa mumeo vibaya. Nadhani mumeo pia anapaswa amweleze mama yake kwa upole kuwa wewe unafanya kazi na huwezi kufanya kazi zote za nyumbani. Pia amweleze kuwa huyo msichana wa kazi kamwe hawezi kuwa mke wa mtoto wake.

  Naamini mtoto wake akimwelimisha na akawa na msimamo, mama mkwe wako ataelewa au hata kama hataelewa, atashindwa kuendelea kusisitiza anachotaka. Ni vyema pia ukakaa na mshichana wako na kumhoji ilikuwaje hata wakazungumza hayo na mkweo na ukiona kama alichokonolewa basi mtahadharishe akae mbali na mama mkwe na asiwe mwepesi kueleza mambo ya ndani ya nyumba kwa mkweo.

  Hata hivyo fanya uchunguzi wako kwa siri na ukiona msichana wako anapalilia ili aolewe yeye, basi ni vyema ukatafuta msichana mwingine wa kazi na huyo kumwondoa ili asije kuharibu ndoa yako. Haina haja kugombana na mtu yoyote kwani naamini huyo mkweo ataondoka na nyinyi mtaendelea na maisha yenu. Pia jifunze kuvumilia kwani wakwe wengine uelewa wao ni mdogo.
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180

  MamaMia
  pole sana kwa hiyo kadhia. kwanza naomba wasifu wa huyo hausigeli namaanisha nieleze maumbiko yake.
  pili natafuta hausigeli nadhani nikimpata huyo mkorofi atanifaa sana maana mie ni bingwa wa kurekebisha meno ya mamba.
  tatu wala usijiulize mara mbili wewe timua huyo hakufai, au la labda ni mdogo wako kwani siku hizi ndugu hugeukana na kutumikishana.... sina uhakika. ila ukitaka amani TIMUA wala usijiulezeulize.
  Nitumie PM ili nijue ntakujaje kumchukua awe hausigeli wangu....
  FIDEL upooo?
   
  Last edited by a moderator: Aug 26, 2009
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Apr 22, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Dear mama

  nina experiance ya vitu hivi niliwahi kuona nyumba moja baba analala na house chumbani na mke wake anajua hilo na wakati wanaenda kulala pamoja mke anajua ila niligundua kwamba yule mwanamke alikuwa anakosa nguvu fulani hivi ya kumwokoa -- hakui haki zake ni nini yeye kama mwanamke na kama mke wa mtu ( wamechukuwana mitaani ) so wengine huwa wanasema ahh hatujaowawna hana haki hizo -- wengine elimu zao na kutojua dunia inakwendaje kazi kukaa ndani tu
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nzuri ngoja ninywe kiloba nikushauri.
  Masanilo,Brenda,Mwanajamii,Nyamayao,WOS,Mbu,Msanii,Joyceline mnaweza mkaendelea na mjadala mwenzenu huyo jahazi linazama h/g katoa TG kwa baba mwenye nyumba.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  mkuu niliiona hii ndo maana nimemshauri amshawishi h/g huyo ahamie kwangu
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hahahaha amemzidi kete yeye hatoi sasa house girl katoa, huyo bora aendelee kuishi naye hapo hapo akimtimua tu kosa baba atampangia nyumba na kuwa nyumba ndogo watakuwa wanagawana umaskini.
  Mzee unataka akuache kwa Sadala duh hahahaha
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Huyo House girl sio anataka kuharibu ndoa, bali anataka kuitengeneza. Inaelekea mama ulishachukulia mambo mengi for granted. Kwa sababu h.girl anafanya kazi vizuri ukabweteka na kusahau baadhi ya majukumu yako nyumbani. Chunguza vema unaweza kukuta kuwa hakusaidii kuosha nguo za mzee tu, bali na mengne mengi anakusaidia
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mpita Njia chakula kikipikwa vizuri nyumbani nani anasifiwa?
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu Msanii unafikiri ana bofulo huyo?
  Mi nahisi hata mfadhaiko hutapata ngoja mama mia atupe details za huyo beki 3 wake je amebeba nyuma? Kama amebeba basi ndo maana baba alipata mfadhaiko unajua akina baba iwa hawatongozi kwa mabeki 3 yeye akipata mfadhaiko tu anavuta mtoto na kumaliza na mkwara mwingi usimwambie mama.
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  kama hana bofulo basi alichezwa huyo. anajua kuinyonga nafsi ya mtu akiitia mkononi.
  Mama mia mbona umegushi?? lete ishu tumfehem huyo kasablanca wako
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu tumekanyaga sio penyewe kume mama mia naye ameitoa hukooooooooo somewhere sio house girl wake huyo...
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hahahaha
  mambo ya masanilo na nyumba yake yenye bwawa la kufugia ngadu
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Anaypewa sifa ni mpishi
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ndo maanake, ngoja tuwasubili akina Nyamayao,Mwanajamii,WOS wanao pinga TG waangalie sasa huyu mama jahazi limesha zama mpaka mama mkwe anampigia pande h/g achukue nyumba duh...ameikubali kazi ya huyu h/g
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ndio maana nimeshamtahadharisha huyo mama kuwa nafasi yake imeshachukuliwa. Na akianza tu jitihada za kutaka kumwondoa kasichana, ataondoka yeye
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sasa Mpishi hapo ni house girl
  Nyumba anaipendezesha house girl
  Watoto anawalea na kuwabembeleza na kuwalisha na kuwaogesha house girl.
  Sasa baba au mama mkwe atamsifiaje huyo mke wake wkt kila kitu anafanya house girl pamoja na chakula cha usiku house girl anampa baba....aaah sifa ziende kwa house girl bana.
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyo mama hana chake ajipange upya asikurupuke eti kumtimua h/g akifanya hivyo tu basi amelikologa atulie tuliiiiiiiii mzee ajiexpress
   
 18. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani Mhusika ni Mama Mia?

  Mama Mia Mpe pole sana huyo mhusika, na amshukuru mume wake kwa kuwa muwazi kwake yeye, hii inaonesha mumewe bado anampenda kwa dhati so wakae chini waangalie ni jinsi gani wanaweza kukaa na mama mkwe na kumuelewesha kwamba hata mke ana majukumu ambayo ni muhimu katika kuijenda Nyumba yao

  Asante
   
 19. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  naona mama mia amejiinamia analia kwa kwikwi
  akinyamaza atajibu maswali yangu
   
 20. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  kuna mahali wamama tunajisahau sana napo ni hapo kwa kumuachia h'gal kila kitu akifanye, mpaka kutandikiwa kitanda jamani, hapana!, hii nayo imekaa vibaya mama mkwe nae kamkubali/anahalalisha ndoa na h'gal, hapa agangamale na mumewe amckie na yeye ana msimamo gani, mana mwenye uamuzi wa mwisho ni mume hapa, akiwa na mcmamo ndoa itaendelea kudumu(apiga maombi sana, shetani ananyemelea ndoa yake), kumfukuza kama walivyosema wengine kutaleta tabu hapo ndani na ikiwa mama mkwe yupo hapo hatokubaliana na hilo, na la mwisho jamani wamama 2we na mipaka na h'gals we2 jamani, sio kuwahusisha/waachia mpaka na vyumba vye2 japo najua 2napotoka maoficn tunakuwa hoi but tujitahidi japo kidogo, sio kwa kuzuia kwamba acje akatembea na mume bali 2jue tu kwamba hapo pana2husu wawili(mume/mke)
   
Loading...