Duh, pole sana dada.
Mimi nakushauri kama unaweza sali sana na hilo pepo likupitilie mbali, muombe bwana Yesu ainusuru ndoa yako, na baada ya hapo wewe sasa jipange upyaaaaaa!!!!!..
Unajuwa wamama wa siku tunajisahau sana katika ndoa zetu, we are taking everything for granted, unadhani ukiolewa ndiyo basi, unajinenepea bila mpango, kutwa kushiriki kwenye kitchen parties, kazi ofisini ni safari saa zoteeeee, hatupiki, hatufui, hatufanyi chochote majumbani mwetu, watoto wetu hatuwalei vizuri tunawaachia hao mahousegeli kuna wamama hata hawalali na watoto wao wakiwa wachanga wanaachwa na mahousegeli jamani ili mradi tu vituko. Tukiwa na kazi nzuri basi tunajiona na kujisikia kuwa tuko sawa na hao waume zetu, hapana inabidi tujirekebishe sana. Siyo wanaume wote wako sawa wengine wanakuangalia tu kama hawajali kumbe wanamaindi kimoyoni.
Hivi mnajuwa kuna wamama wanawaachia mahousegeli kufuwa hadi chupi zao na chupi za waume zao, jikoni wanaingia hata baada ya miezi 2 ndiyo wanafika jikoni, sex mpaka aanze mwanaume sisi kila siku tuko busy na tumechokaaa unadhani mume haoni yote hayo, wamama wengine wachafu na wavivu hata kutandika vitanda vyao hawawezi yote no dada anafanya, jamani waume wana macho nao wanaona, mwisho wa siku si bora ajiolee tu huyo housegeli.
By the way sisemi kama wewe unafanya haya yote ila nahisi kuna sehemu utakuwa ulikosea.
Anyway jipange upyaaaaaaa hujachelewa bado, naamini mume wako anakupendaaa ndiyo maana hata akakueleza yanayoendelea.
Nakutakia mafanikio mema na ujipange upya dada sawa. Muombe Mwenyezi Mungu atakusaidia na akupe nguvu.
Ni mimi Mahengo