Hotuba Ya JK: Tafsiri Yangu

Doooh!
Majjid kuna mengi umenena na sijakubaliana nayo.
Kwamba JK ametumia busara, sidhani kama uko sahihi - Shinikizo ni kubwa kwa sasa (watu wana mwamko).
Kwamba JK si mwendawazimu, labda uko sahihi - ila mbona alikuwa anaongea kimajungu sana juu ya watu wanaotaka kusababisha vurugu? kama rais wa nchi amewashindwa wafanya vurugu nani atawaweza? (hapo namaanisha kuwa mleta vurugu namba moja ni yeye)
Kwamba JK amefocus miaka 50 ijayo, si kweli - Angeanza na kuisafisha system

I have a strong feeling of Hatred towards my President.. Yes, i said so!
 
I believe rais anapata ushauri kutoka sehemu nyingi ambao sometimes is confusing but kwa kusikiliza kilio cha watanzania kuhusu katiba nampa credit. Anayesema CDM ndo walianzisha movement ya katiba huo ni uongo maana nakumbuka mtikila ashawahi hadi kulipandisha mahakamani hili swala. Just tuwe wa kweli kwamba now hili swala limepata mwamko mkubwa kutoka kwa wananchi ndo maana limepita.
Mkisema rais anafanya kazi kwa kushinikizwa huo ni uongo maana rais kachaguliwa na wananchi so anasikiliza wananchi wanataka nini bila kubagua chama, kabila, rangi wala dini.
But hotuba ya rais ina mapungufu mengi hasa kwenye swala la ufisadi wa mikataba ya umeme ambao amekua muda mrefu ameweka pamba maskioni. TANESCO imekua mwiba kwa kodi za wananchi lakini yeye kama rais hajawahi kutoa msimamo wake juu ya kashfa za Tanesco.
 
jaamani tusiwe watu wa kulaumu kwa kila kitu, kunapokuwa na kizuri japo kidogo basi tutoe pongezi. mimi siku zote napinga sana uongozi wa JK kwa ujumla maan ni wa kishikaji zaidi.
Lakini kwa hili inagwa ni kweli amesoma majira na nyakati, yey kama Raisi hata kama angekataa ,kwani ungemlazimisha ? kuna serikali nyingi tu duniani haka USA zinafanya vitu vingine sababu tu ya influnce ya media, kwahiyo sioni ajabu kwa kikwete kukubaliana na kitu kulingana na upepo halisi.
 
SIJASOMA THREAD hii .... kwa kuwa naamini KILA ANACHOONGEA KIKWETE huwa ni MANENO.... mimi nitasema BAADA ya kuunda katiba... no comment
 
mnasahau kuwa wenzetu walifika kwenye katiba mpya baada ya kumwaga damu na kutiana jela.

JK tunampongeza kwa kutupeleka kwenye mjadala wa jambo hilo bila ya kufika huko na kwa hilo ndio tunapomsifia

JK ni kiongozi na sio mtawala


Na yeye kakubali katiba baada ya kuiba ushindi wa urais. Tofauti iko wapi?
 

We kichwa sana Mkuu! Ningekuwa na uwezo wa kukugongea Thanks nyingine 50 basi ningefanya hivyo. Sijui kwanini huyu jamaa hakusema ni lini jopo hili litaundwa. na kwa maoni yangu hii ya kuwa kimya ilikuwa ni makusudi kabisa ili waendelea kuangalia upepo kuhusu mjadala huu wa katiba. Wakiona wanaweza kuendelea kusubiri basi si ajabu hii 2011 ikakatika bila jopo hilo kuundwa maana ameshazoea kufanya kazi kwa kushinikizwa vinginevyo hawezi kuchukua leadership role.

 



Hivi wewe bado unafiki suala la katiba mpya limeletwa na mchungaji Slaa?

haya ni malalamiko ya Muda mrefu kwa upinzani hasa CUF toka zamani, Slaa wakati huo ana support ccm akiwa kanisani kabla ya kunyimwa kugombea ubunge kwa ticket ya ccm, hivi ulikuwa wapi wakati ule ??
 
So far What JK is doing now ni kujaribu kupunguza Pressure, hapo ana buy time tu hana Lolote, kwamba Watu wakisema basi ionekane hakuna Sababu maana Mkulu ameshalizungumzia ha ha ha
 
So far What JK is doing now ni kujaribu kupunguza Pressure, hapo ana buy time tu hana Lolote, kwamba Watu wakisema basi ionekane hakuna Sababu maana Mkulu ameshalizungumzia ha ha ha

Haswa!
 
Redet: JK soma alama za nyakati Send to a friend Friday, 31 December 2010 20:48

Salim Said
MWENYEKITI Mwenza wa Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet), Dk Benson Bana, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kusoma alama za nyakati na kubeba ajenda ya katiba mpya ili kuweka vipaumbele vyake na kujijengea heshima baada ya kustaafu kwake.
Akizungumza na Mwananchi kwa simu jijini Dar es Salaam jana, Dk Bana alimtaka Rais Kikwete kuwapa Watanzania salamu bora za mwaka mpya kwa kuwaahidi katiba mpya kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka 2014.

"Kama napata fursa ya kukutana na rais leo (jana), kabla hajaanza kuwahutubia Watanzania, ningemshauri na kumuomba kabisa asome alama za nyakati, ni aibu ajenda ya katiba mpya kuongozwa na wapinzani, wanaharakati na watu wengine wakati serikali ipo," alisema Dk Bana na kuongeza:
"Mifano ipo ya kutosha, wenzetu wa Kenya na Uganda wameachana kabisa na katiba hizi za watu waliojifungia vyumbani na kutunga katiba bila ya kushirikisha jamii husika."

Dk Bana anaungana na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Makungu, Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye na Jaji Mkuu mstaafu Augostino Ramadhan kuunga mkono hoja ya kuundwa katiba mpya.

Madai ya Katiba mpya, pia yamewahi kutolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ambaye alisema bayana kuwa katiba mpya iandikwe mapema kabla ya mambo kuharibika.
Dk Bana anapingana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, aliyetaka katiba iliyopo iwekewe viraka.

"Suala la katiba mpya halitaki mjadala mrefu na wala sio la kuweka viraka, haya tumeweka viraka halafu iweje? Itasaidia nini? Hivyo viraka tumeweka mpaka tumechoka, lakini hakuna mabadiliko matatizo yanaendelea kuzidi," Dk Bana alipinga vikali kauli ya Jaji Werema.

Alisema katiba mpya ni msingi kwa Tanzania ya sasa na kwamba, serikali haipaswi kupata kigugumizi katika kuchukua ajenda hiyo ya kuanzisha mchakato wa kuipata haraka.
Dk Bana ambaye pia ni Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema katiba iliyopo haijibu maswali ya msingi ya Watanzania kuhusu mustakbali.

"Katiba ndio msingi wa taifa kwa kila kitu, hivyo pamoja na mambo mengine, lazima ijibu maswali ya msingi ya Watanzania, mambo ya Tume huru ya uchaguzi, nguvu ya rais, viongozi wa umma wawajibike kwa nani, katiba lazima iweke wazi mambo haya mazito," alisema Dk Bana.

Alifafanua kuwa, katiba mpya lazima iwe na fikra na mawazo shirikishi sio suala la mtu au kikundi cha watu kujifungia ofisini na kuandika katiba kwa niaba ya Watanzania.
Madai ya katiba mpya yalizidi kupamba moto baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo Rais Kikwete alitangazwa mshindi kupitia CCM.

Pia, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, tayari amewasilisha hoja binafsi ofisi za Bunge ili iweze kujadiliwa katika kikao kijacho cha bunge na CUF wamewasilisha mapendekezo yao ya katiba mpya kwa Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani.
 

Nadhani hujaisoma post ya mwanzo ya thread hii kiukamilifu.

Uelewe kuwa katiba si hoja mpya na wala si hoja ya Chadema au dk silaa!

CUF walishaandika rasimu ya katiba zamaaaaani.

CCM chini ya Mwinyi, kundi la wana CCM wakiongozwa na fundikira walishadai zamani katiba mpya.

Uelewe kuwa, katiba si msahafu, itakwenda ikibadilika na hakuna jipya hapo.

Kikwete jana kafunga kazi na nnakuhakikishia ataondoka kaacha, si tu katiba mpya au mwelekeo wa katiba mpya bali mengi mazuri na mema kwa Taifa. Maendeleo tuliyopata Tanzania katika miaka mitano ya Kikwete hayajawahi kufikiwa hata robo kwa awamu zote zilizopita kwa pamoja.
 
Kwanini jambo kubwa hili namna hii halikuwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM miezi michache tu iliyopita? Au ilipoifika Disemba 31, ndio walikumbuka kuwa tunaanza miaka hamsini ya uhuru wetu?

Ni kikao gani cha CCM kilichopitisha suala kuingizwa na CCM maana hadi hivi sasa Katiba mpya siyo sera ya CCM; sera ya CCM ni "kufanyia mabadiliko hii Katiba iliyopo kwani inatufaa" au tuanze kukumbushia kauli zao hizo tangu enzi za kina Mary Nagu, Mathias Chikawe n.k?

Yeye amepata wapi madaraka ya kuanzisha mchakato wa KUubadilisha ya nchi au kwa vile ni "Rais" basi tunaamini anaweza kufanya lolote wakati wowote with impunity?
 

The past is history in files. We are longing for issues to be resolved. Tume ya kusimamia mabadiliko ya Katiba itaanza kazi lini, na kazi hiyo itaisha lini, to mention a few.

Kumbuka Rais hayuko kwa maslahi ya chama chake tu. Issue iwe ya chama cha upinzani au chama tawala, kama ni valid kwa ustawi wa wananchi wote na inahitaji mkono wa Rais, hana makosa kuichukua na kuifanyia kazi.
 
Dar-es-Salaam,
You keep talking of maendeleo tuliyoyapata Tanzania katika miaka mitano ya uongozi wa Kikwete. Naomba unifahamishe hayo maendeleo kwa sababu mimi mwenzako sijaona kitu. Hasa pale unaposema hayajawahi kufikiwa hata robo kwa awamu zote zilizopita. Nitajie angalau mawili matatu na mimi niondoe tongotongo machoni.
 

:frusty::frusty::A S 114::A S 114::blah: You Maggid, ww kazi yako si Journalist wa Siasa, bakia Global publishers, UDAKU fits you best, acha kuandika

usichojua, koma, kaandike nani KAFUMANIWA,na GUEST GANI, Nani na nani wanatoka kungonoka etc, hii ndio kazi yako, umbea Journalism
& kujua Ubongo wako how low u r, ETI JANA JK KAFANYA JAMBO KUBWA SANA.....!!!!!!!!!!???? :frusty::frusty: :smash::smash: hii njaa hii, mbaya sana,
hasa unapokuwa na njaa ya akili, kwani nani alianzisha hoja ya katiba mpya? hata hujui unaandika nini, na TUNATAKA TUME HURU IUNDWE NA BUNGE na Dowans mbona hujamuuliza
hajasema chochote?, nadhani umeelewa why i said ww UMBEA, UDAKU, Upaparazzi unakufaaaaa, hivi have you even Graduated F4? Kaandike Amani, Ijumaa, Uwazi, Risasi usiingilie kuandika Siasa, get out, hata hufanani na Kinyonga wala Bendera fuata upepo, shame on you, hufaiiiii period
 

Maggid katoa maoni yake, na wewe toa ya kwako. Mijitusi kwako ndio hoja.
 
Ukweli kuhusu hili ni kuwa kaanza kutekeleza ilani ya CHADEMA - within the first 100 days in office (though through the tunnel - like any other thief), ametangaza kuanza mchakato.

Ingawa ni mapema mno kusherehekea - maana wazaramo wana msemo wenye tafsiri ya 'kilonga mbali, kitenda mbali'

Time will tell
 
Maggid katoa maoni yake, na wewe toa ya kwako. Mijitusi kwako ndio hoja.

Most u r comments show u r KIHIYO as Maggid, arrogance dominates u r mind, you never say the truth, hatutaki Kiongozi of copying & pasting, pure & simple
 
Maggid katoa maoni yake, na wewe toa ya kwako.

Maggid hii ni fani yake..... kwahiyo we expect more from his analysis..... simjui vizuri kwahiyo siwezi kusema huko nyuma aliyoandika lakini kwa hili... very dissapointing.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…