Hotuba Ya JK: Tafsiri Yangu

Hotuba Ya JK: Tafsiri Yangu

hata tusemeje, kama tume ya marekebisho inaanzia kwa JK ina maana yeye atakua na mkono kwenye kila kitu... then i dont want it;
he has promised me as a normal citizen heaven... all i got was hell
he has messed up my country
sielewi rais gani unaunga mkono wananchi wako kubebeshwa mizigo ya kampuni kama dowans wakati wewe unatuhumiwa kuwa mmiliki

If supporting JK on this one is right, then i dont wanna be right
 
maggid,
i said this once but I will repeat it again;
I used to love your articles on RAI enzi za MRABA WA MAGGID...
but what u av been writing lately, we both know, kuna mkono wa mtu! it's just not the Maggid i knew...
 
Fikirieni mara mbili mbili juu ya Tume ya Katiba kuzaliwa Ikulu badala ya bungeni.
5. Njia sahihi: Mchakato huu ni vema uanzie ndani ya Bunge. Hili si suala la serikali ni la Wananchi ambao wawakilishi wao wako Bungeni.

Bunge gani mnaloliongelea? hatuna choice kwa sasa, CCM ina majority Bungeni na maamuzi ya wabunge wa CCM "kama kamati ya chama chao" ndiyo yatakayokuwa maamuzi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Salama yetu ni kama tu JK analiona atakaloli..gain kwa kufanikisha mchakato huu, kwani akilitekeleza vizuru atagain zaidi kuliko mwingine yeyote, historia itamkumbuka kama Rais aliyeanzisha mchakato uliompunguzia madaraka ya Rais katika utawala wa nchi hii, na kama Nyerere alivyokuwa "hero" katika uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi nchini ndivyo JK atakavyokuwa "hero" kwenye katiba mpya.

Hii inanikumbusha Ruud Van Nistelrooy alivyokuwa akijiposition vizuri na kupachika mabao kiulaini na kuwa shujaa wa mechi japo kazi kubwa na ngumu zaidi ilifanywa na wengine. Ndivyo maisha yalivyo, kwenye jambo lolote kubwa na lenye manufaa shujaa uwa ni mtu mmoja tu na kwa bahati mbaya sana yawezekana hakuwa "shujaa halisi" na mbaya zaidi "mashujaa halisi" husahauliwa haraka na kutokumbukwa katika historia, that is life!!
 
Afadhali JK amekubali yaishe ila awe makini uchakachuaji wa tume na mchakato wake usipewe nafasi. Kamwe mawazo ya mafisadi na wahujumu uchumi yaepukwe kama EBOLA
 
Ndugu Zangu,

NIMEMSIKILIZA Rais wetu akilihutubia taifa jana jioni. Hii ni tafsiri yangu ya alichokiongea.

Kwanza kabisa nataka niseme, kuwa hotuba ile ya Rais Kikwete ni ya kihistoria. Ni moja ya hotuba muhimu sana katika historia ya nchi yetu tangu tupate uhuru. Maana, jambo lile la nne na la mwisho lililozungumzwa na Rais wa Awamu ya Nne kwenye hotuba yake, ndilo jambo lililofungua ukurasa mpya wa taifa letu baada ya miaka 50 ya uhuru. Rais

Jakaya Kikwete ameongea jambo kubwa sana usiku wa jana. Hakika, Kikwete hatabiriki na ni mtu wa rekodi. Jana ameweka rekodi nyingine.

Gwiji wa fasihi ya Kiswahili katika Tanzania na Afrika Mashariki, marehemu Shaaban Bin Robert alipata kuandika kitabu chenye kuhusu maisha yake; ”Maisha Yangu Na Baada Ya Miaka 50”.

Kwa hotuba ile ya Kikwete iliyobeba vision ya Kikwete kwa Tanzania kwa miaka 50 ijayo, inaweza kabisa kumweka JK katika nafasi ya kuanza kuandika kitabu juu ya kumbukumbu za maisha yake. Jinsi yeye, kama Jakaya Kikwete alivyoiona miaka yake 50 ya alikotoka na anavyoiona miaka 50 ijayo, si kwake tu, bali kwa nchi kubwa aliyojaaliwa kupata bahati ya kuiongoza. Nchi ya Tanzania.

Maana, JK kama binadamu, kuna mazuri na mabaya aliyoyafanya katika utendaji wake wa kazi maishani mwake. Na katika hili la Uona Mbali juu ya Katiba yetu, basi, kama JK atafanikiwa kuongoza juhudi hizi za Watanzania kupata Katiba iliyofanyiwa marekebisho makubwa, sina shaka yeyote, kuwa ataacha legacy kwa maana ya haiba. Katiba Mpya itakuwa moja ya jambo kubwa atakalokumbukwa nalo.

Ndio, JK atakumbukwa kama Rais aliyeongoza mabadiliko makubwa na ya kihistoria yaliyopata kufanyika katika nchi yetu. Kukumbukwa kwa kuchangia kuifanya nchi yetu kuwa mahali pema pa kuishi; kuwa nchi ya kisasa zaidi kuliko ilivyo sasa. Hofu yangu, ni kama JK ataweza kuachwa kuifanya kazi hii bila kukwamishwa na nguvu hasi za wahafidhina ndani ya chama chake, CCM.

Kwa anachotaka kufanya JK yaweza kabisa ikawa mchango wake katika kukinusuru chama chake, CCM. Kwamba CCM, kama chama, kisije kikapotea kabisa kwenye ramani ya kisiasa. Kwamba hata CCM ikija kushindwa, ibaki kuwa Chama cha Upinzani chenye nguvu na kinachoweza kurudi tena madarakani.

Maana, huko twendako, upo, uwezekano wa CCM kushindwa uchaguzi. Kwa Katiba ya sasa, siku CCM ikishindwa uchaguzi, itakuwa na maana ya chama hicho kuporomoka kama nyumba ya karata. Si hata Mzee Makamba mwenyewe alipata kutamka hadharani, kuwa Mtaji wa CCM ni Kikwete!

Na juzi hapa Mzee Makamba akatamka; kuwa hana maoni juu ya Katiba, anamsubiri JK atoe tamko. Hicho pia ni kielelezo cha mapungufu ya Katiba yetu. Na tushukuru nchi yetu haijapata bahati mbaya ya kuwa na ’mwendawazimu’ pale Ikulu ya Magogoni.

Na wenye kutanguliza ubinafsi wao ndani ya CCM hawauoni ukweli, kuwa si miaka mingi kutoka sasa, Chama Cha Mapinduzi kitakuwa chama cha upinzani. Hawautambui ukweli, kuwa himaya zote duniani hujengwa na kuporomoka. Hakuna himaya iliyodumu daima. Hata Roma iliporomoka. Kwa vijana wa sasa, salamu ya ” CCM Daima!” ni kielelezo cha watu waliopitwa na wakati.

Na kumsaidia JK katika kutupitisha kwenye njia hii salama tunayoitaka sasa ni kwa Watanzania kutambua ukweli, kuwa demokrasia yetu bado changa. Tumefanya chaguzi zenye walakini mwingi, ni sehemu ya kujifunza. Na sasa tuna fursa ya kuandaa Katiba itakayotufanya tujenge misingi imara ya demokrasia yetu.

Kumsaidia JK ni kukubali ukweli kuwa Uchaguzi uliopita umeshapita. Kwamba Serikali iliyo madarakani kwa sasa ndio hiyo inayoongozwa na JK kama Rais. Hatuna Rais mwingine. Hatuna Serikali nyingine. Rais tuliye naye sasa ni Jakaya Mrisho Kikwete.
Na tuukubali ukweli pia, kuwa wakati umebadilika na kuwa wananchi wanaukubali upinzani. Na kwamba kwa sasa CHADEMA ndio chama kikuu cha upinzani kikifuatiwa na CUF. CCM, CHADEMA , CUF na wengine wana lazima ya kushirikiana katika mambo ya msingi na yenye maslahi kwa taifa letu.

Ndio, tumeumaliza mwaka jana na mjadala wa Katiba mpya. Tunaingia mwaka 2011 na mjadala wa Katiba Mpya. Hili ni jambo jema. Na lililo muhimu kabisa katika mjadala wowote uwao ni kujiuliza; nini shabaha na malengo yetu?
Nionavyo, shabaha na leo letu liwe kudumisha Umoja wetu wa Kitaifa, amani na utulivu tulio nao.

Kama swali ni je, Katiba yetu ya sasa, na kwa wakati uliopo, inakidhi matakwa ya shabaha na malengo yetu kama taifa? Jibu langu ni HAPANA. Na ndio maana nimekuwa na nitaendelea kuunga mkono juhudi za kufanya marekebisho makubwa ya Katiba yetu.

Na katika hili hatuna sababu za kugombania fito ilihali nyumba tunayojenga ni moja na ni yetu sote.
Ieleweke, kuwa madai ya Watanzania kupata Katiba mpya ni madai muhimu na ya kihistoria. Tumewasikia hata wanaojidanganya, wakiandika, kuwa madai haya yanatokana na ‘ Njama za mabeberu!’. Hizi ni propaganda za miaka ya 70, zimepitwa na wakati.

Ni busara kutambua, kuwa wakati umebadilika. Mtanzania wa mwaka 1977 si Mtanzania wa mwaka 2010. Hoja hii ya Katiba si kama nzi anayetua na kuruka. Hoja ya Katiba kwa sasa inaongozwa na kundi kubwa la vijana wanaotaka mabadiliko. Hawa si nzi wanaotua na kuruka, ni siafu wanaokuja kwa kuongezeka idadi yao.

Na madai ya marekebisho ya Katiba si madai mapya. Si madai ya chama au kikundi kidogo cha ’wapinzani’ wasioitakia mema nchi hii. Ni madai ya msingi ya Watanzania, bila kujali tofauti zao za kiitikadi, kidini, rangi na makabila.

Kama ni shauri mahakamani, basi, lilishafunguliwa. Kinachofanyika sasa ni mwendelezo wa shauri. Ndio, tunapongia mwaka 2011, madai ya Katiba mpya yatatimiza miaka 20. Yalianza tangu mwaka 1991.

Ndio, si wengi, miongoni mwa vijana wa sasa, wenye kumbukumbu ya ukweli huu. Tayari mwaka 1991 vuguvugu la kudai vyama vingi na Katiba mpya lilishaanza. Wakati huo madai makubwa yalikuwa mawili; vyama vingi na Marekebisho ya Katiba. Kuna mnaokumbuka ’ KAMAKA’- Kamati ya Marekebisho ya katiba iliyondwa na wanaharakati. Hayo yalikuwa ni madai ya Watanzania ndani ya mfumo wa chama kimoja.

Marehemu Chifu Abdalah Fundikira aliongoza Kamati iliyoundwa, si na Serikali, bali wanaharakati, kuratibu mchakato wa kudai vyama vingi na Katiba mpya.

Hata wakati huo Mzee Mwinyi, kama Rais, aliweka ‘ mkwara’, kuwa madai hayo yasiendeshwe na watu au makundi ya watu bila kibali cha Serikali. Presha ya madai ilipoongezeka, tunakumbuka, kuwa Mzee Mwinyi aliweza kusoma alama za nyakati. Aliongea pale Chuo Kikuu Mlimani na kuweka bayana dhamira ya Serikali ya kuunda ‘ Tume ya Nyalali’ . Tume hiyo ilizunguka nchi nzima kuwauliza Watanzania kama wanataka kuendelea na Chama kimoja au Vyama vingi.

Itakumbukwa, Chifu Fundikira alipata kutamka; kuwa huko ni kupoteza muda na fedha za wananchi. Itakumbukwa pia, Mabere Marando alikuwa Katibu wa Kamati ile ya wanaharakati ya kuratibu mchakato wa madai ya kuwepo na vyama vingi na marekebisho ya Katiba.
Marando alipata kutamka na kunukuliwa na Daily News, April, 12, 1991; “ We have a bad political system because our Constitution embraces political discrimination. What we want is that all of us should shout out that our Constitution is bad.” ( Mabere Marando, Daily News, April 12, 1991)

Ndio, Marando aliyasema hayo katika Semina ya kwanza ya Kamati ya kuratibu mchakato wa madai ya vyama vingi na Katiba mpya iliyoongozwa na Chifu Fundikira. Semina hiyo iliudhuriwa na watu wapatao 800 kwa mujibu wa taarifa ya Daily News la April 12, 1991.

Na akina Chifu Fundikira waliandamwa sana. Kwa mujibu wa Daily News la April 26, 1991, Mbunge wa Shinyanga, Ndugu Paulo Makolo alimshambulia Fundikira kwa kusema kuwa , katika hilo la kuwa na vyama vingi na katiba mpya , Chifu Fundikira hawasilishi mawazo ya Wasukuma na Wanyamwezi wenzake; “ This is not a Wanyamwezi and Wasukuma movement. It is the selfish interests of Fundikira and his ten colleagues. Our people are not after parties. They want food, water, education and health care.” ( Paulo Makolo, MP, Shinyanga, Daily News, April 26, 1991). Mwenyezi Mungu umrehemu Chifu Abdalah Fundikira.

Maggid
Iringa,
Januari Mosi, 2011
mjengwa

Waandishi wetu wa habari huwa wananiacha hoi sana! Nilichofurahia hapa hujamwita Dr Kikwete kama ufanyavyo huko nyuma
 
waandishi wetu wa kibongo bwana! wanachekesha sana maggid anasema JK ametoa hotuba ya kihistoria? ipi? kuunda tume ya katiba mpya mbona hizo tume zilishaundwa hata na marais waliotangulia na ni wazi lazima katiba ibadilishwe,kwanza kutokana na mabadiliko ya zanzibar.na pili kuifanya nchi iwe salama.
utakumbuka jk ana 26% tu ya watu waliomchagua wenye sifa za kupiga kura.hatujui wale 52% ambao hawakupiga kura wana mtizamo gani lakini nachotaka kumwambia maggid kila jambo lina wakati kama ilivyokuwa 1992 hata angekuwa yeye mfumo wa vyama vingi angeruhusu,apende asipende.cha muhimu tunahitaji ushujaa wa kubadilisha uchumi wa wananchi.watanzania wanahitaji chakula mezani siyo blabla.
 
Mhh halafu kuna watu hivi wanakaa chini kusoma au kusikiliza hotuba za huyu sijui mnamuita jina limenitoka:redfaces::redfaces::redfaces::redfaces:

Wow! kwa hiyo wewe unatushauri tusimsikilize? Ila tuje humu kwenye forum kuchangia maoni juu ya points au pumba anazotoa kwenye hotuba... does this make sense? Please help me.
 
Maggid....? nimesoma kidogo hapo juu baadaye nikaangalia mwandishi mmmhhh nimewaachia wenyewe!

What do you mean? did that "Maggid" ever do something that permanently negates his views from being heard? yaani mi sijaelewa? wewe kaa hapo na stereotypic/prejudicial thinking yako... its better to hear it all and then sort the relevant from the rubbish... thats what they call maturity..you should try it out...
 
Just another proof that we are a nation of loons!!!!!!!
 
Ndugu Zangu,

NIMEMSIKILIZA Rais wetu akilihutubia taifa jana jioni. Hii ni tafsiri yangu ya alichokiongea.

Kwanza kabisa nataka niseme, kuwa hotuba ile ya Rais Kikwete ni ya kihistoria. Ni moja ya hotuba muhimu sana katika historia ya nchi yetu tangu tupate uhuru. Maana, jambo lile la nne na la mwisho lililozungumzwa na Rais wa Awamu ya Nne kwenye hotuba yake, ndilo jambo lililofungua ukurasa mpya wa taifa letu baada ya miaka 50 ya uhuru. Rais

Jakaya Kikwete ameongea jambo kubwa sana usiku wa jana. Hakika, Kikwete hatabiriki na ni mtu wa rekodi. Jana ameweka rekodi nyingine.

Gwiji wa fasihi ya Kiswahili katika Tanzania na Afrika Mashariki, marehemu Shaaban Bin Robert alipata kuandika kitabu chenye kuhusu maisha yake; ”Maisha Yangu Na Baada Ya Miaka 50”.

Kwa hotuba ile ya Kikwete iliyobeba vision ya Kikwete kwa Tanzania kwa miaka 50 ijayo, inaweza kabisa kumweka JK katika nafasi ya kuanza kuandika kitabu juu ya kumbukumbu za maisha yake. Jinsi yeye, kama Jakaya Kikwete alivyoiona miaka yake 50 ya alikotoka na anavyoiona miaka 50 ijayo, si kwake tu, bali kwa nchi kubwa aliyojaaliwa kupata bahati ya kuiongoza. Nchi ya Tanzania.

Maana, JK kama binadamu, kuna mazuri na mabaya aliyoyafanya katika utendaji wake wa kazi maishani mwake. Na katika hili la Uona Mbali juu ya Katiba yetu, basi, kama JK atafanikiwa kuongoza juhudi hizi za Watanzania kupata Katiba iliyofanyiwa marekebisho makubwa, sina shaka yeyote, kuwa ataacha legacy kwa maana ya haiba. Katiba Mpya itakuwa moja ya jambo kubwa atakalokumbukwa nalo.

Ndio, JK atakumbukwa kama Rais aliyeongoza mabadiliko makubwa na ya kihistoria yaliyopata kufanyika katika nchi yetu. Kukumbukwa kwa kuchangia kuifanya nchi yetu kuwa mahali pema pa kuishi; kuwa nchi ya kisasa zaidi kuliko ilivyo sasa. Hofu yangu, ni kama JK ataweza kuachwa kuifanya kazi hii bila kukwamishwa na nguvu hasi za wahafidhina ndani ya chama chake, CCM.

Kwa anachotaka kufanya JK yaweza kabisa ikawa mchango wake katika kukinusuru chama chake, CCM. Kwamba CCM, kama chama, kisije kikapotea kabisa kwenye ramani ya kisiasa. Kwamba hata CCM ikija kushindwa, ibaki kuwa Chama cha Upinzani chenye nguvu na kinachoweza kurudi tena madarakani.

Maana, huko twendako, upo, uwezekano wa CCM kushindwa uchaguzi. Kwa Katiba ya sasa, siku CCM ikishindwa uchaguzi, itakuwa na maana ya chama hicho kuporomoka kama nyumba ya karata. Si hata Mzee Makamba mwenyewe alipata kutamka hadharani, kuwa Mtaji wa CCM ni Kikwete!

Na juzi hapa Mzee Makamba akatamka; kuwa hana maoni juu ya Katiba, anamsubiri JK atoe tamko. Hicho pia ni kielelezo cha mapungufu ya Katiba yetu. Na tushukuru nchi yetu haijapata bahati mbaya ya kuwa na ’mwendawazimu’ pale Ikulu ya Magogoni.

Na wenye kutanguliza ubinafsi wao ndani ya CCM hawauoni ukweli, kuwa si miaka mingi kutoka sasa, Chama Cha Mapinduzi kitakuwa chama cha upinzani. Hawautambui ukweli, kuwa himaya zote duniani hujengwa na kuporomoka. Hakuna himaya iliyodumu daima. Hata Roma iliporomoka. Kwa vijana wa sasa, salamu ya ” CCM Daima!” ni kielelezo cha watu waliopitwa na wakati.

Na kumsaidia JK katika kutupitisha kwenye njia hii salama tunayoitaka sasa ni kwa Watanzania kutambua ukweli, kuwa demokrasia yetu bado changa. Tumefanya chaguzi zenye walakini mwingi, ni sehemu ya kujifunza. Na sasa tuna fursa ya kuandaa Katiba itakayotufanya tujenge misingi imara ya demokrasia yetu.

Kumsaidia JK ni kukubali ukweli kuwa Uchaguzi uliopita umeshapita. Kwamba Serikali iliyo madarakani kwa sasa ndio hiyo inayoongozwa na JK kama Rais. Hatuna Rais mwingine. Hatuna Serikali nyingine. Rais tuliye naye sasa ni Jakaya Mrisho Kikwete.
Na tuukubali ukweli pia, kuwa wakati umebadilika na kuwa wananchi wanaukubali upinzani. Na kwamba kwa sasa CHADEMA ndio chama kikuu cha upinzani kikifuatiwa na CUF. CCM, CHADEMA , CUF na wengine wana lazima ya kushirikiana katika mambo ya msingi na yenye maslahi kwa taifa letu.

Ndio, tumeumaliza mwaka jana na mjadala wa Katiba mpya. Tunaingia mwaka 2011 na mjadala wa Katiba Mpya. Hili ni jambo jema. Na lililo muhimu kabisa katika mjadala wowote uwao ni kujiuliza; nini shabaha na malengo yetu?
Nionavyo, shabaha na leo letu liwe kudumisha Umoja wetu wa Kitaifa, amani na utulivu tulio nao.

Kama swali ni je, Katiba yetu ya sasa, na kwa wakati uliopo, inakidhi matakwa ya shabaha na malengo yetu kama taifa? Jibu langu ni HAPANA. Na ndio maana nimekuwa na nitaendelea kuunga mkono juhudi za kufanya marekebisho makubwa ya Katiba yetu.

Na katika hili hatuna sababu za kugombania fito ilihali nyumba tunayojenga ni moja na ni yetu sote.
Ieleweke, kuwa madai ya Watanzania kupata Katiba mpya ni madai muhimu na ya kihistoria. Tumewasikia hata wanaojidanganya, wakiandika, kuwa madai haya yanatokana na ‘ Njama za mabeberu!’. Hizi ni propaganda za miaka ya 70, zimepitwa na wakati.

Ni busara kutambua, kuwa wakati umebadilika. Mtanzania wa mwaka 1977 si Mtanzania wa mwaka 2010. Hoja hii ya Katiba si kama nzi anayetua na kuruka. Hoja ya Katiba kwa sasa inaongozwa na kundi kubwa la vijana wanaotaka mabadiliko. Hawa si nzi wanaotua na kuruka, ni siafu wanaokuja kwa kuongezeka idadi yao.

Na madai ya marekebisho ya Katiba si madai mapya. Si madai ya chama au kikundi kidogo cha ’wapinzani’ wasioitakia mema nchi hii. Ni madai ya msingi ya Watanzania, bila kujali tofauti zao za kiitikadi, kidini, rangi na makabila.

Kama ni shauri mahakamani, basi, lilishafunguliwa. Kinachofanyika sasa ni mwendelezo wa shauri. Ndio, tunapongia mwaka 2011, madai ya Katiba mpya yatatimiza miaka 20. Yalianza tangu mwaka 1991.

Ndio, si wengi, miongoni mwa vijana wa sasa, wenye kumbukumbu ya ukweli huu. Tayari mwaka 1991 vuguvugu la kudai vyama vingi na Katiba mpya lilishaanza. Wakati huo madai makubwa yalikuwa mawili; vyama vingi na Marekebisho ya Katiba. Kuna mnaokumbuka ’ KAMAKA’- Kamati ya Marekebisho ya katiba iliyondwa na wanaharakati. Hayo yalikuwa ni madai ya Watanzania ndani ya mfumo wa chama kimoja.

Marehemu Chifu Abdalah Fundikira aliongoza Kamati iliyoundwa, si na Serikali, bali wanaharakati, kuratibu mchakato wa kudai vyama vingi na Katiba mpya.

Hata wakati huo Mzee Mwinyi, kama Rais, aliweka ‘ mkwara’, kuwa madai hayo yasiendeshwe na watu au makundi ya watu bila kibali cha Serikali. Presha ya madai ilipoongezeka, tunakumbuka, kuwa Mzee Mwinyi aliweza kusoma alama za nyakati. Aliongea pale Chuo Kikuu Mlimani na kuweka bayana dhamira ya Serikali ya kuunda ‘ Tume ya Nyalali’ . Tume hiyo ilizunguka nchi nzima kuwauliza Watanzania kama wanataka kuendelea na Chama kimoja au Vyama vingi.

Itakumbukwa, Chifu Fundikira alipata kutamka; kuwa huko ni kupoteza muda na fedha za wananchi. Itakumbukwa pia, Mabere Marando alikuwa Katibu wa Kamati ile ya wanaharakati ya kuratibu mchakato wa madai ya kuwepo na vyama vingi na marekebisho ya Katiba.
Marando alipata kutamka na kunukuliwa na Daily News, April, 12, 1991; “ We have a bad political system because our Constitution embraces political discrimination. What we want is that all of us should shout out that our Constitution is bad.” ( Mabere Marando, Daily News, April 12, 1991)

Ndio, Marando aliyasema hayo katika Semina ya kwanza ya Kamati ya kuratibu mchakato wa madai ya vyama vingi na Katiba mpya iliyoongozwa na Chifu Fundikira. Semina hiyo iliudhuriwa na watu wapatao 800 kwa mujibu wa taarifa ya Daily News la April 12, 1991.

Na akina Chifu Fundikira waliandamwa sana. Kwa mujibu wa Daily News la April 26, 1991, Mbunge wa Shinyanga, Ndugu Paulo Makolo alimshambulia Fundikira kwa kusema kuwa , katika hilo la kuwa na vyama vingi na katiba mpya , Chifu Fundikira hawasilishi mawazo ya Wasukuma na Wanyamwezi wenzake; “ This is not a Wanyamwezi and Wasukuma movement. It is the selfish interests of Fundikira and his ten colleagues. Our people are not after parties. They want food, water, education and health care.” ( Paulo Makolo, MP, Shinyanga, Daily News, April 26, 1991). Mwenyezi Mungu umrehemu Chifu Abdalah Fundikira.

Maggid
Iringa,
Januari Mosi, 2011
mjengwa

JK hawezi na wala hastahili kupewa pongezi kwa hili, amelazimishwa. JK amekuwepo kwenye utawala wa nchi hii kwa miaka mingi, ameingia kwenye uchaguzi, vyama vya upinzani vikiwa vinalalamikia uchaguzi kuendeshwa na tume ya uchaguzi usiyo huru. Tunamlaumu JK, watangulizi wake na hasa kabisa CCM kwa kuweza kujionesha kwa uwazi kabisa kuwa mara nyingi kimekuwa kikiendesha mambo yake kwa dhamira mbaya dhidi ya watanzania wengi kwaajili ya maslahi yao ya chama na mafisadi wao.

Hivi, mtu au chama chenye dhamira safi hakiwezi kuona kuwa mgombea wao ambaye ni Rais kumpa madaraka ya kuchagua tume ya uchaguzi ambayo itasimamia uchaguzi ambao na yeye anagombea, ni kinyume kabisa cha misingi ya utendaji haki? Ningeimba wimbo wa kumsifu JK, na ningependekeza aingizwe kwenye kumbukumbu za wapenda demokrasia Duniani kama kabla ya uchaguzi wa 2010, yeye akiwa Rais angekubali kuunda tume huru ya uchaguzi, na kukishawishi CCM kuweka ndani ya ilani yake hoja ya kupatikana katiba mpya, hapo ningejua na kuamini dhamira safi ya JK. Hivi ukimtambua mwizi, baadaye ukachachamaa kuwa ni lazima nitengeneze mlango ili huyu mwizi wa sasa na wengine wa baadaye wasiniibie tena, halafu yule mwizi naye akakuambia kuwa nakuunga mkono, na ili ufanikiwe ngoja nitakutafutia watu wa kukusaidia kutengeneza mlango mzuri ili usiibiwe tena, baada ya hapo utatoka na kuanza kumsifia mwizi wako wa siku zote? Tunachotakiwa kujiuliza ni je kweli JK na CCM wana dhamira ya kutengeneza mlango imara? Na je, sasa hivi huyu mwizi wetu wa siku zote ameamua kuacha kuiba? Kama bado anategemea kuendelea kuiba, si ajabu akatuletea mlango unaoonekana imara kwa macho, lakini watengenezaji wakamwonesha sehemu zilizo dhaifu ambazo zitamruhusu yeye kuendelea kuingia na kuiba.

Tamko la katiba mpya litolewe na bunge la JMT. Serikali kwa kuwa ndiyo yenye rasilimali nyingi, ipewe mwongozo na bunge jinsi ya kushughulikia upatikanaji wa katiba mpya kadiri ya matakwa ya watanzania. Hatutaki katiba iandaliwe na serikali halafu wananchi wawe wachangiaji au watoa maoni.
La muhimu kuliko yote, watanzania ni lazima tutengeneze mlango wetu (katiba) bila ya kuongozwa na wevi, waliotutengenezea mlango wa zamani uliowaruhusu wao kuingia na kuendelea kuiba bila shida, pengine kwa staili nyingine.
 
Ndugu Zangu,
Historia ni mwalimu mzuri. Bado kuna umuhimu wa kukumbushana tulikotoka. Huko nyuma nimeuliza kama kuna wanaokumbuka alichotamka Bw. Augustiono Mrema. Ni mrema huyu aliyepata kuwa Waziri wa Mambo ya ndani katika kipindi cha Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi.

Katikati la vuguvugu lile la mageuzi ya kisiasa miaka ya 90 mwanzoni, Watanzania zikatufikia habari; kuwa Oscar Kambona, aliyekosana na Nyerere na aliyekimbila uhamishoni Uingereza alikuwa njiani kurudi nyumbani. Ujio wa Oscar Kambona ukawa gumzo la mjini na nje ya jiji. Kuna waliojiandaa kwenda uwanjani kumpokea.

Usiku mmoja ikasikika sauti ya Bw. Mrema redioni. Sauti ya Waziri wa Mambo ya ndani. Mrema alitamka, kuwa kama Kambona angekanyaga mguu wake Dar es Salaam, basi, angekamatwa kujibu mashtaka ya uhaini.

Ni hofu ile ile ya Serikali hata wakati huo. Hofu ya kuimarika kwa fikra za upinzani na kukua kwa upinzani. Mrema akatumika au akajituma kuwatisha Watanzania. Kambona alikanyaga Dar, hakuwa na mashtaka ya kujibu. Ulikuwa ' mkwara' tu, kama wanavyosema mitaani.

Na Mrema, akiwa Waziri wa Mambo ya ndani, alifanya kweli kazi ya kuwa ' Mbwa wa Serikali'. Na alibwaka kweli. Nakumbuka usiku mmoja mwanzoni mwa miaka ya tisini nilimsikia Mrema akitoa ' mkwara' redioni kutishia maandamano ya CUF. Maandamano yale yalikuwa yahitimishwe kwa mkutano viwanja vya Mnazi Mmoja. Mwenyekiti wa CUF, ( Tanzania Bara) Bw. James Mapalala ndiye alikuwa aongoze maandamano hayo na kuhutubia.

Augustino Lyatonga Mrema akaaunguruma redioni usiku ule. Alirusha ' mkwara' mzito. Kuwa maandamano hayo si halali na yangekutana na nguvu za dola. Kesho yake CUF waliingia mitaani. Ndio, Ungangari wa CUF ulianza siku nyingi.

Pale mnazi mmoja FFU wakamwagwa, na farasi wao pia. Virungu vilitembea. James Mapalala, Mwenyekiti wa CUF hakuonekana. Kukawa na taarifa kuwa anatafutwa na polisi.

Dar ilikuwa ndogo wakati huo, lakini James Mapalala hakupatikana siku hiyo.
Ninazo taarifa za kuaminika za kibalozi, kuwa James Mapalala alikuwa amejificha kwenye moja ya makazi ya rafiki yake, balozi wa nchi moja ya Kimagharibi. Ni balozi gani huyo? Na nini hasa kilitokea miaka 20 iliyopita?

James Mapalala yungali hai. Huu ni wakati kwa waandishi vijana kuwatafuta wazee veterani wa harakati za mageuzi ya kisiasa hapa nchini kama akina Mzee James Mapalala.

Hawa ni watu muhimu sana watakaotusaidia kupokea simulizi zao. Kisha ziwekwe kwenye maandishi na iwe kumbukumbu za kihistoria. Ni historia yetu, tusiionee aibu. Ni urithi tutakaowaachia wajukuu zetu ili nao waweze kujitambua na kujenga mioyo ya uzalendo.
Huu wangu ni mchango mdogo tu.
Maggid

http://mjengwa.blogspot.com
 
Back
Top Bottom