Kweli wajinga ndio waliwao,taarifa ya mafuta ilikuwepo kwenye magazeti siku moja baada ya huyu mzee aliedhulumiwa na chadema kufarikiView attachment 2945198
Wema wa Sabodo si huu kiduchu wa kusaidia vyama vya siasa nchini Tanzania , Huyu mtu kifo chake ni pigo kuliko hata mapigo mnayoyajua , Kuna haja ya Hotuba ile ya Mbowe kuletwa hapa JF kwa njia ya Video (Naitafuta) , Ifike wakati sasa Bendera ziwe zinapepea nusu mlingoti kwa baadhi ya Wazalendo kama Sabodo wanapofariki , Ikiwezekana hata mizinga ivurumishwe hewani watu hawa wanapofariki , haiwezekani tunawaenzi wezi na makatiri lakini tunawaacha watu wema kama hawa .
Kumbe kuna wakati Sabodo alibeba dhamana ya Nchi kwenye uhaba wa Mafuta (nadhani ni diesel na Petroli) , cha kushangaza anasubiriwa Mbowe ndio ayaseme haya ! hivi viongozi wanaoficha historia hii hawaijui au hawataki ?
Iko haja ya viongozi wapya wachanga wa nchi hii kufundishwa kwanza walioifikisha hii nchi hapa ilipo badala ya kupewa vyeo kwa mtindo wa Koneksheni na Uchawa .
Uhakika ni kwamba over 90% ya viongozi wa nchi hii wakiwemo mawaziri na viongozi wa ccm hawajui Uzalendo wa Sabodo na ni Aibu kwao na Aliyewateua , Unateuaje watu wasioijua Nchi yao ?