Hotuba ya Freeman Mbowe kwenye Msiba wa Sabodo imefichua mengi ambayo tulifichwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,730
218,305
Screenshot_2024-03-25-21-19-06-1.png


Wema wa Sabodo si huu kiduchu wa kusaidia vyama vya siasa nchini Tanzania , Huyu mtu kifo chake ni pigo kuliko hata mapigo mnayoyajua , Kuna haja ya Hotuba ile ya Mbowe kuletwa hapa JF kwa njia ya Video (Naitafuta) , Ifike wakati sasa Bendera ziwe zinapepea nusu mlingoti kwa baadhi ya Wazalendo kama Sabodo wanapofariki , Ikiwezekana hata mizinga ivurumishwe hewani watu hawa wanapofariki , haiwezekani tunawaenzi wezi na makatiri lakini tunawaacha watu wema kama hawa .

Kumbe kuna wakati Sabodo alibeba dhamana ya Nchi kwenye uhaba wa Mafuta (nadhani ni diesel na Petroli) , cha kushangaza anasubiriwa Mbowe ndio ayaseme haya ! hivi viongozi wanaoficha historia hii hawaijui au hawataki ?

Iko haja ya viongozi wapya wachanga wa nchi hii kufundishwa kwanza walioifikisha hii nchi hapa ilipo badala ya kupewa vyeo kwa mtindo wa Koneksheni na Uchawa .

Uhakika ni kwamba over 90% ya viongozi wa nchi hii wakiwemo mawaziri na viongozi wa ccm hawajui Uzalendo wa Sabodo na ni Aibu kwao na Aliyewateua , Unateuaje watu wasioijua Nchi yao ?
 
Hotuba ile ya Mbowe kuletwa hapa JF kwa njia ya Video (Naitafuta) , Ifike wakati sasa Bendera ziwe zinapepea nusu mlingoti kwa baadhi ya Wazalendo

Shughuli nzima hii hapa Mustafa Rajabali Jaffer


View: https://m.youtube.com/watch?v=BZaE5qS0W7k
KSIJ Imambargah, Dar es Salaam, Tanzania. It is with great sadness that we share the news of the demise of MUSTAFA RAJABALI JAFFER (SABODO) who passed away in Dar es Salaam on Saturday, 23rd March 2024 May Allah (SWT) bless the departed soul amongst His chosen ones and grant the family patience to bear this loss - Ameen. You are kindly requested to remember the departed soul with a Sura-e-Fateha, Sadaqa and Namaaz-e-Hadiya Mayyit.Kafan - Dafan Committee
Kwa hisani kubwa ya: Sameer Haidershah
 
Hata mimi namshangaa huyu Erythrocyte kumbe ni mbumbumbu wa mambo mengi ambayo kwake ni mageni kabisa masikioni mwake. Ndio maana Mbowe anawaburuza sana huko CHADEMA kama manyumbu au makondoo.
Kuna jamaa kwenye jukwaa la maoni na malalamiko..

Amekuanzishia Uzi akiwaambia mods unatukana Sana watu..

Jamaa hakukosea.

All in all,

Lucas Huwaga haupo rational upo bias yaan wewe hunaga Jambo zuri lolote kwa opposition party
 
Kumbe kuna wakati Sabodo alibeba dhamana ya Nchi kwenye uhaba wa Mafuta (nadhani ni diesel na Petroli) , cha kushangaza anasubiriwa Mbowe ndio ayaseme haya ! hivi viongozi wanaoficha historia hii hawaijui au hawataki ?

Iko haja ya viongozi wapya wachanga wa nchi hii kufundishwa kwanza walioifikisha hii nchi hapa ilipo badala ya kupewa vyeo kwa mtindo wa Koneksheni na Uchawa .

Uhakika ni kwamba over 90% ya viongozi wa nchi hii wakiwemo mawaziri na viongozi wa ccm hawajui Uzalendo wa Sabodo na ni Aibu kwao na Aliyewateua , Unateuaje watu wasioijua Nchi yao ?
Anyway Sabodo alikuwa mjanja wa mjini.

Hayo mafuta Toka Iran tuliyapata ila kwa mkopo .Iran Haikutoa bure.Ilitaka lazima ilipwe pesa zake.Tukashindwa kulipa deni lao cash wala haukuwa na riba .Ila nchi ikawa choka mbaya.Ieleweke Sabodo huo mkopo haukuketwa bure na yeye hakufanya hiyo kazi bure.Ni agent dalai mjanja fulani hivi .Na kila dalai huwa na chake.Niishie hapo Mafuta tukapata toka Irani lakini sio bure.Walitukopesha.Tukashindwa kulipa hali ngumu pesa za kigeni hamna.Hawakuwa na shida kudai hilo deni kipindi cha Raisi Mwinyi muislamu mwnzao akiongea kitu walikubali kwa shingo upande ila pesa zao walitaka


Kipindi raisi Mkapa Mkristo kashika Iran wakachachamaa wanataka pesa zao sababu waliogopa Mkristo aweza kataa deni wakiamini muislamu ndio mwaminifu kulipa deni

Mkapa akaona aoengee na waislamu wanazuoni wazalendo wa uhakika waaminiwa na serikali na umma waliotulia kiimani na wenye hekima kubwa Wazee wa hekima wanaojali nchi yao Tanzania kuwa jua liwake mvua inyeshe wako na Tanzania
ukatumwa ujumbe mzito wa waislamu nchi hii wazalendo kwenda Iran sitaki kuwataja toka misikitini ,serikalini nk wakaomba hilo deni la Iran lilipwe sio kwa fedha taslimu za dola wakaomba lilipwe kwa fedha za Tanzania au chochote kinacholingana na hizo pesa za den la Irani ila badala ya kwenda Iran ziende kwa waislamu wa Tanzania kutatua changamoto zao

.Iran iliposikia kuwa zitaenda kwa waislamu kutatua changamoto zao ikakubali na kiatoa msamaha mkubwa tu wa deni.Zilizobaki wakasema wakaulizwa mnataka ziende hawana chuo kikuu cha kiislamu wala hawana uwezo wa kujenga Mkapa akakubali mahesabu yakapigwa waislamu wakapewa chuo kikuu cha Morogoro kilichokuwa chuo cha Tanesco pale Morogoro na serikali ikamalizana na lile deni na Irani .Serikali ikawapa waislamu kwa faida yao kama ilivyokubalika
Kuna kesi nyingi za nchi kudaiwa na kurudisha mali zilizotaifishwa za makanisa nk kulipia madeni nchi ilishindwa kulipa viongozi wa makanisa wanatumwa nchi zao dini za Kikristo na viongozi wakiristo serikalini nk wanatumwa kujadili na nchi kupata ufumbuzi unapatikana kupitia viongozi wa dini tu

Mbowe na upinzani Tanzania bado watoto sana wanaendekeza individual politics nchi kama nchi ina deal.na mambo mazito far above individuals na sifa za kibinafsi za majukwaani au mitandaoni za ohh sijui huyu alifanya hivi kuna mengine hayawekwi wazi other side

Usione viongozi wa dini wanakaa vitu vya mbele raisi akiwepo au shughuli ya kitaifa ikiwepo they deserve

Utawaona wamekaa kama wajinga fulani hivi .Wanaelewa mambo mengine mazito solutions zake kuliko wanasiasa au viongozi wa serikali wanaotembea na misafara
 
Back
Top Bottom