Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Habari za boxing day wananchi,
Sisi tulio uzeeni tunafarijika sana kuona kijana Kama Sugu ambaye ameishi maisha ya taadhari zote za kiuchumi akifanikiwa kuwekeza kwenye hoteli huku akiwa hana skendo yoyote ya wizi wa fedha za umma.
Tumezoea kwa miaka mingi miradi ya vijana wa Chama cha Mapinduzi ikihusianishwa na biashara haramu na utakatishaji fedha ingawa hakuna ambaye amewahi kuhojiwa kuhusu tuhuma ambazo uelekezwa kwao.
Kwa mfumo wa siasa za Tanzania kila tajiri lazima awe ndani ya Chama Tawala la sivyo atafilisiwa hata Kama hakuna ushahidi wa jinai ndani ya utajiri wake.
Nichukue fursa hii kuwaomba vijana wenzangu tujitahidi sana kutafuta na kuwekeza kwa kesho yenu na vizazi vijavyo. Sugu amejaribu akifuata nyayo za Mwenyekiti wake wa chama, Profesa Jay yupo vyema, Msigwa pia yupo vyema.
Vijana wengine fanyeni kazi, wekezeni bila kulazimishwa kujiunga na chama Tawala. Utajiri ni moja ya nguzo kubwa yakufanikisha maamuzi kwenye jamii
Tunataka wapinzani wenye nguvu ya kiuchumi na si wapinzani wenye mawazo yakufadhiliwa.