Hoteli ya Sugu iwafumbue macho vijana kuhusu nguvu ya uwekezaji

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,979
Habari za boxing day wananchi,

Sisi tulio uzeeni tunafarijika sana kuona kijana Kama Sugu ambaye ameishi maisha ya taadhari zote za kiuchumi akifanikiwa kuwekeza kwenye hoteli huku akiwa hana skendo yoyote ya wizi wa fedha za umma.

Tumezoea kwa miaka mingi miradi ya vijana wa Chama cha Mapinduzi ikihusianishwa na biashara haramu na utakatishaji fedha ingawa hakuna ambaye amewahi kuhojiwa kuhusu tuhuma ambazo uelekezwa kwao.

Kwa mfumo wa siasa za Tanzania kila tajiri lazima awe ndani ya Chama Tawala la sivyo atafilisiwa hata Kama hakuna ushahidi wa jinai ndani ya utajiri wake.

Nichukue fursa hii kuwaomba vijana wenzangu tujitahidi sana kutafuta na kuwekeza kwa kesho yenu na vizazi vijavyo. Sugu amejaribu akifuata nyayo za Mwenyekiti wake wa chama, Profesa Jay yupo vyema, Msigwa pia yupo vyema.

Vijana wengine fanyeni kazi, wekezeni bila kulazimishwa kujiunga na chama Tawala. Utajiri ni moja ya nguzo kubwa yakufanikisha maamuzi kwenye jamii

Tunataka wapinzani wenye nguvu ya kiuchumi na si wapinzani wenye mawazo yakufadhiliwa.
 
Mshahara wa Mbunge take home ni zaidi ya million 11, na anakopesheka kwenye taasisi za fedha.

Mbunge yeyote ubunge wake ukiisha akawa na maisha mabovu ni kichaa huyo.

Mzindakaya ana ranji kabisa na kachukuwa sana mikopo kwa bond ya BOT na mikopo isiyokuwa na riba.
 
Mzindakaya ana ranji kabisa na kachukuwa sana mikopo kwa bond ya BOT na mikopo isiyokuwa na riba.
Huyo Mzindakaya alifisadi fedha kule BOT enzi ya marehemu Balali akaanzisha ranch na kiwanda cha nyama; sina hakika kama bado anamiliki hizo mali kwani kuna wakati ziliwekwa chini ya uangalizi wa Tanzania Investment Bank kwa kushindwa kwake kulipa madeni!!!
 
Mkuu hueleweki,

Mwanzoni umesema wewe ni mzee,( sisi tulio uzeeni), baadae umesema unawaomba vijana wenzako mjitahidi!!!!!!!!!. Ila hoja yako iko vizuri.
Wewe upo makini na mimi nimeliona hilo lakini inaonekana hamjui vizuri anayemsifia, itoshe kusema amefanya jambo jema kuwekeza ila kuhusu usafi wa hela aweke akiba ya maneno.
 
Huyo Mzindakaya alifisadi fedha kule BOT enzi ya marehemu Balali akaanzisha ranch na kiwanda cha nyama; sina hakika kama bado anamiliki hizo mali kwani kuna wakati ziliwekwa chini ya uangalizi wa Tanzania Investment Bank kwa kushindwa kwake kulipa madeni!!!
Mzindakaya hana chochote mkuu, shamba lenyewe analikodisha tu kwa wakulima.
 
Kusema Msigwa amebobea kwenye kilimo cha nyanya ni kumdharau?
Wewe una utindio wa ubongo nahisi

Mbona hujibu hao mataga wenzio wana miradi gani halali wewe nyumbu; kufananisha na mashamba ya nyanya ya Msigwa?
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom