Kama Mbunge au Waziri anashindwa kujenga nyumba ya kuishi atawezaje kuweka mipango sahihi ya nchi katika ulimwengu wa kibepari?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Ulimwengu wa kibepari unataka mwanasiasa anayeweza kusimama mwenyewe kiuchumi na siyo mwasiasa mjamaa. Viongozi wengi hawana nyumba ila wana magari makubwa ambayo kama siyo ya serikali basi ni mkopo wa Ubunge

Watu wa aina hii wengi wao hawajawahi kushika milioni mia moja ya pamoja. Akaunti zao zinasubiri pensheni ndipo ziwe na milioni mia ya pamoja. Hawa viumbe wana madhara makubwa sana kwa uchumi wetu.

Kwa sababu hakuna chochote anachosimamia au kumiliki anaweza akatunga sera mbaya za kodi, anawaona wenye fedha ni wezi na wanapaswa kufilisiwa, anaamini sana kwa utajiri wa wazungu siyo watanzania wala watu weusi, ni mtu mjinga wa fikra kwamba kushindwa kwake ni kushindwa kwa kila mmoja kwenye jamii.

Kutokana na kuwa na watu wengi wa aina hii tumekuwa wakopaji wakubwa kuliko kuzalisha. Tumekuwa wepesi wakuwapa wageni kila kitu tukiamini hakuna watanzania wanaweza. Tumekuwa wepesi kusifu wizi wa wazungu huku tukishinikiza wananchi wetu kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi.

Hali hii imepelekea watanzania wengi kukosa confidence yakuendesha biashara na matokeo yake wafanyabiashara wengi wameamua kutengeneza makampuni na RAIA wa kigeni wakiamini kwamba wageni ni kinga kwao. Kwamba wakiulizwa watasema ni mali ya mchina au mzungu.

Kwa muktadha huu wakukosa watanzania wenye kumiliki uchumi kumepelekea nchi kukosa dola kwani wageni wanahamisha fedha na kupeleka kwao. Kwa upande mwingine kila tajiri ameonekana ni lazima awe mfadhili wa siasa za Tanzania hasa za chama tawala. Kukataa kuchangia siasa za chama tawala kimetafsiriwa na wabunge na mawaziri masikini kama kigezo cha kuelekeza ufilisiwe.

Kwa mantiki hiyo mwaka huu na mwakani wafanyabiashara wengi maisha yao ni kuwapa fedha wagombea na viongozi wa chama. Biashara zimekuwa ngumu na hata yanapitishwa katika vikao rasmi na hakuna uthibitisho wa kupokea fedha husika.

Haya ni madhara yakuwa na watu wasio na akili yakutafuta fedha na kuwekeza. Wamejaa roho za kimaskini na wanatumia madaraka yao kisiasa kuzamisha meli za wajasiriamali wa ndani

Wageni nao wameanza kusumbuliwa na kibaya zaidi wanaripoti usumbufu huu kwenye balozi zao. Matapeli nao wanatumia huu mwanya kuweka picha za viongozi ofisini kwao na kutembea na sare za chama kujichukulia fedha.

Ni taifa linalokosa dira pekee ndilo linaweza kuwekeza kwa wanasiasa masikini wakitegemea wawe na mafanikio. Taifa linahitaji matajiri wakubwa kusimamia siasa siyo kuendesha siasa wakiwa mafichoni. Tanzania inakwenda kuingia kwenye umaskini kwa viongozi wa kisiasa kuweka akilimwao kwamba kila mwenye fedha lazima apige magoti kwao.

Viongozi wetu wamegeuka ombaomba na sasa wanaanza kusumbua hata wawekezaji wachangie chama na fedha kwenda mifukoni. Wapo wapi makachero kuona namna chama kinachotumika vibaya? Kweli tumefika mahali kila kampuni nchni lazima Itenge fedha za kuchangia wanasiasa ? Je watu wa aina hii wanaweza kusimamia ukusanyaji kodi au watageuka watetezi wa wakwepa kodi?


Kuelekea 2025 tuondoe maskini na academicians kwenye siasa tuweke watu wanaoweza kulisha familia bila kutegemea malipo ya serikali. Vyama vya siasa viache kuteua maskini wateue wenye fedha halali ili maskini wengi wawe na hasira yakuwa matajiri. Teuzi kwa maskini zifutwe ili watumishi wa umma na sekta binafsi wajifunze kuweka akiba na kuwekeza
 
Tunahitaji Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya kabla ya Uchaguzi wowote,

Nchi yetu ni ya wakulima na wafanyakazi.

Sera Bora za kiuchumi zinahitajika kuwatajirisha wananchi wote, Si kundi dogo la walanguzi.
 
Mtu yeyote yule anayegombea nafasi ya kuwawakilisha wananchi, lazima awe mwananchi mwenye shughuli inayoeleweka yenye kumuingizia kipato cha kuendesha maisha.
Kwa maneno mengine anawawakilisha wananchi wenzake wenye shughuli kama hizo wanaolipa Kodi (ambayo huendesha serikali na shughuli za maendeleo).
Pili lazima awe na makazi (minimum standard).
 
Back
Top Bottom