Barua kwa vijana wetu (Dear Vijana)

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Wadogo zangu vijana wa Kitanzania habari zetu. Mimi ni kijana mkubwa 40+ na napenda niwaandikie barua kutoka moyoni kwangu kwa ninayo yaona miaka hii na kwa nchi yetu ya Tanzania. Mambo nitakayo yasema unaweza usayaelewe kwa wakati huu kutokana na umri wako au uzoefu wako kwenye maisha lakini haita kuwa vizuri kila siku kuishia kuwapiga madongo kila siku badala yake huu ni wakati wa kusema kama Kaka.

1. Tanzania ya sasa mwaka huu 2024 ni bora kiuchumi kuliko wakati sisi tuna maliza Form 6 kwa mimi binafsi ilikuwa mwaka 1996 pale Tambaza Secondary. Hivyo asije kutokea mtu akawadanganya kwamba uchumi wa sasa ni mbaya kuliko zamani hii sio kweli.
2. Tanzania bado ni nchi masikini sana pamoja na rasilimali tulizonazo. Mimi nimetembea nchi nyingi sana na nimekuwa naishi nchi tofauti toka mwezi wa nane 1997 hivyo nasema haya kwa kujiamini na uzoefu na sio kwa kubahatisha.
3. Mabadiliko ya tabia nchi ni ya kweli hivyo mazingira ya mvua, mafuriko , kiangazi ni zaidi sasa kuliko miaka ile ya kwetu tukiwa 20's. Hivyo kwenye mipangalio yako tilia hili maanani.
4. Teknologia ni bora sana kwa vyakati zenu kuliko wakati wetu. Ingawa Teknologia kwa vijana wengi hamuitumia kwa faida ya kujiendeleza.
5. Ushindani wa sasa wa kazi, na maarifa kwenu ni mkubwa zaidi maana mnashindana kitaifa na sio Tanzania peke yake lakini vilevile fursa mnazo zaidi ya nyakati zetu.
6. Siasa za Tanzania hazibadilika sana zaidi ya wapinzani kupata nguvu zaidi . Lakini ukweli ni kwamba hatujawahi kubahatika kupata watu kwenye chama chetu tawala ambao wameweka mbele nchi zaidi ya marafiki zao, famillia zao na kundi la wachache viongozi wa vigogo wa kisiasa. Majina kama Kikwete, Mwinyi, Karume, Kinana, Kingunge. Nauye, Makamba., Malecela, Lowassa tumeyasikia kwa miaka zaidi ya 30. Hivyo viongozi wenu wa kisiasa na wabunge hawajawahi kuwajali na hawajali hata sasa kama wanavyo jiaminisha.
Je nawashauri mfanye nini

1. Ushauri wangu wa kwanza . Kila kijana jiulize kwa undani wako unapenda kuwa nani kwenye maisha yako. Usifanye vitu kwa kuiga iga fanya vitu kutoka moyoni.
2. Tumieni teknologia kujiendeleza kiuchumi mfano kutafuta kazi, kuomba mawazo, kutafuta shule, kutengeneza App, kusoma, kutafuta kazi za nje, kumuamini mungu zaidi, kujiunga na makundi ya nje ya nchi ya kimaendeleo n.k. Weka muda maalumu wa kutumia mitandao kwa mambo mengine lakini muda mwingi uwe kwenye maendeleo
3. Ukishajua kitu unachopenda tafuta Mentor. Memntor ni mtu ambaye ni mfano wa wewe unataka kuwa huyu ni mshauri lakini mwenye uzoefu wa kweli. Mfano wewe unataka kuwa mwana siasa basi hata hapa mitandaoni watafute wakina Zitto, Mwigulu na wengine sio lazima wawe maarufu tafuta mmoja mwombe awe mentor wako. Lakini kuna Mentor wa biashara, kilimo, elimu, chochote utakacho. Memntor sio lazima awe Mtanzania. Mimi nipo Texas na kwa asilimia kubwa nimefanikiwa kwa kushauriwa na wazungu ambao kwa wengine wanaweza kuitwa wabaguzi lakini unahitaji mmoja mzuri tu kukushauri na kukutoa.
4. Msikimbilie kuoa. Maisha ya siku hizi na maendeleo ya afya mnakuwa na maisha marefu wengi wenu tumieni muda kutafuta marafiki na watu mtakao endana nao badala ya kukimbia kuona kwa kufikiri umechelewa. Kosa la kukimbia kuoa na kuzaa linaweza kukuharibia ndoto zako.
5. Pesa haitatosha kukupa furaha. furaha utapata kutoka kwa watu na kusaidia watu na sio kuwa na pesa nyingi. Hata pale utakapo pata pesa furaha watu wanapata pale wanapoona watoto wao na ndugu zao wanafurahi na sio pesa yenyewe.
6. Hakuna maisha bila kufanya kazi. Unaweza kupata kazi inallipa sana lakini majukumu nayo yanakuwa makubwa. Muda unakuwa mdogo, kodi nyingi, wafanyakazi wengi kwasabbu kipato kuongezeka mara nyingi gharama za maisha nazo zinaongezeka. Hivyo matatizo hayaishi bali yanahama tu. Hakuna kazi rahisi popote Duniani.
7. Afya zenu nmuhimu sana. Pombe kunywa kwa kiasi, hakikisha unaangalia kila kitu kwenye mwili wako. Mwili ni kama gari ambalo ninaishi mpaka miaka 100 na ni mmoja tu. Gari utanunua lingine lakini mwili wako ni huohuo. Macho ni hayo hayo, miguu ndiyo hiyo hiyo kuwa mwangalifu.
8. Kuweni makini sana na vyakula vya kisasa. Piza, buggers na vyakula vya makopo.
9. Usiogope kutafuta kazi nje ya nchi kwa faida ya famila yako
10. Msisubiri kuletewa maendeleo na serikali tumesubiri kwa miaka 60 sasa!
11. Upinzani pekee sio suluhisho nyie ndiyo mnatakiwa kupigania maendeleo yenu sio vyama vya siasa pekee. Hakuna wa kulaumu kama nyie wenyewe mnaridhika kirahisi na umasikini. Mna nguvu kuliko mnavyojifikiria
12. Kuna wakati kwenye maisha yako pesa na mambo mengine yote hayata weza kukusaidia na wewe kuwa sawa ni lazima uwe na Imani kwa Mungu. Ukifiwa, kuumwa ndiyo utajua hili. Ni lazima uweke imani mbele
13. Achani kuwa fake
14. Uwezo wako uko moyoni kwako. Unajua unaweza sasa kwanini unalalamika sana. Acheni tabila za kulalamika. Mfano kwenye siasa Lissu kapigwa risasi bado ana andamana na sio kulalama pekee.
15. Jiwekee mipango ya maendelo kila mwaka
16. Jiamini na msiogope.

Ka ijumaa hii nitaishia hapo nawatakia siku njema
 
View: https://youtu.be/3gaMydWMUDo?si=jCTi67AC5eO4QCbY
 
Vijana waache kutumia muda mwingi kwenye ushabiki wa mipira na miziki.
Angalia wakati unatafuta fursa, wewe usije geuzwa fursa.
Msipende kukimbilia kazi rahisi. Nafasi za kisiasa, u ubunge. Tafuta kazi za kutumia akiri na nguvu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom