Hoteli wanayopika ugali asubuhi

Hoteli wanayopika ugali asubuhi

Weweweeeeeeee! kama una utani na Wasukuma na Wakuria sawa, vinginevyo unaweza kujikuta umepelekwa "Gambushi"!

Kwa taarifa yako wale wakulima wa Kisukuma au Kikurya, huwa wanakula ugali mkubwa wa dona halafu pembeni kunakuwa na ugali mdogo wa sembe...huo ugali mdogo ndio unafanywa kama mboga...na hayo yote hufanyika sio asubuhi bali ni alfajiri jogoo wa kwanza tu akiwika
 
Asubuhi tulipokuwa tunaenda kuchunga ng'ombe unapigwa ugali wa mhogo na sato wa kubanikwa, weee inanogaje? Kwa hiyo ukiniambia ugali unaliwa mchana tu sikuelewi kiviiiilee.
 
Pale korogwe karibu na kituo cha magari ya abiria kuna moja ina pika Pilau asubuhi, unashushia na chai kabisa!
 
Sasa si afadhali hata huo unapikwa asubuhi watu tushakula sana kiporo cha ugali na chai asubuhi alafu freesh tu unadunda mtaani!

kaka umenikumbusha mbali sana wkt nipo primary na kwa nguvu za Mungu now naitafuta shahada ya pili kiroho saaafii.
 
Njoo hapa kwetu Iringa keepleft ya uwanja wa samora, kama waelekea down ya ipogolo asubuhi nguna unapata tena nyeupe kabisa haina pumba kwa nyama choma .........
Will be there....never thought ugali upo pale. Nimevikinai vya stereo na Miami
 
Nenda Cameroon ugali unaliwa asubuhi na mchana. Kitaalam ugali (heavy meal) inatakiwa kuliwa asubuhi na mchana. Usiku light food is perfect since your body needs to rest. Kula Ugali asubuhi ni sahihi kabisa.
 
Kama umekulia Dar, lazima iwe BIG news. Mkoani hiyo kitu ni kawaida sana, kutokana na nature ya kazi zao, ambazo nyingi ni za nguvu. Nikawaida sana ukifika mji kama Mwanjelwa Mbeya kukuta ugali na wali viko tayari saa 12 asb. Watu wa minadani ambao hawana nafasi ya kula pia hula ugali ama wali mida hiyo ya asb

Mkuu nakumbuka niliwahi kufika pande za Tunduma nikakuta Makande ndiyo Breakfast yao.
tena siyo kiporo,, na kikikosekana wale jamaa walikuwa wanakosa raha kabisa...
 
Naanzisha Hotel hapo Mwenge itaitwa Nguma restaurant itakuwaa na ugali samaki wa michuzi na maziwa bila kusahau kachumbali nyingi kwa wenye hanghover
[/COLOR]
hii kali zaidi.nadhani watu wa hotel jijini watumie fursa ya kibiashara kuandaa dona asubuhi
 
mmmmh,
kichuri nasikia kinaongeza nguvu kwa me.

Mamkubwa Mamndenyi kichuri ni dawa ya magonjwa mengi. Uliza mkurya yeyote anakwambia. Make ni mchanganyiko miti aina mbalimbali... Na ujuavyo tiba mbadala kichuri ni mwisho... Kinatibu malaria, kinaongeza hamu ya kula n.k
 
Last edited by a moderator:
ni ya kawaida lakini ukiyatafsiri kwa kiswahili lazima ban ikumaliza,kuna bibi mmoja apo tarime mjini mitaa ya ronsoti kila asubuhi akiamuka anatoa matusi kwa mabinti zake ata bila sababu, adi majirani wanaamka, utasikia nyakundo ,msagani, kivumvu cha nyakwenu na mengine siyakumbuki.

Teh teh teh.... Afu ukitaka kuyatamka hayo matusi lazima unywe ubhusara kwanza, make utahisi njaa!!!
 
kaka umenikumbusha mbali sana wkt nipo primary na kwa nguvu za Mungu now naitafuta shahada ya pili kiroho saaafii.

Hongera sana brother,

Mimi huwa nakaa na kukumbuka yale maisha nabaki kucheka tu ila nimepigana sana namshukuru mungu,Sitaki mwanangu aje kuishi maisha kama yale tena.
 
Ajabu ipo wapi sasa?

Kwa kawaida(watu waliokulia mjni tunakuwa washamba kwa mambo ya kijijini). Hata mm siku ya kwanza kuona ugali asbh nilipoenda Mugumu mwaka 2010, sa1 watu na nguna...hakika nilishangaa sana! Ndipo nikawa najua kumbe ugali ni chai
 
Eneo la Kigamboni, Ferry Dar-es-Salaam. Asubuhi asubuhi kabisa unapata mlo wa moto uwe ugali, pilau n.k maana taimu hiyo ndo mashua/ngalawa yetu ya ukoo ilikuwa inarejea pwani na mzigo wa samaki huku ukiwa hoi bin taabani kwa mawimbi na njaa ya usiku nzima moja kwa moja unaanza na mlo kabisa iwe pilau, ugali n.k kwa mama/baba ntilie.
 
Teh teh teh.... Afu ukitaka kuyatamka hayo matusi lazima unywe ubhusara kwanza, make utahisi njaa!!!

umenikubusha ubhusara iyo kitu tamu balaa,wanakateknolojia kao jinsi ya kutengeneza,ila mwisho wa maneno kuna uji wao special wanutengeneza wakati wa harusi,jina nimesahau la huo uji,ni mtamu kupita maelezo,hii watu ya pande ya tarime inafaidi vitu vitatamu tamu.
 
mbona ni kawaida sana, tembelea mkoa wa Mara na wilaya zake zote, watu hawanywi chai asbh, ni ugali kwa kwenda mbele
Kwangu imekuwa news
baada ya kukuta mgahawa mmoja jijini Dar wateja wake wakila ugali mida
ya saa mbili asubuhi. Je hii ni kawaida?!
Maoni yako ni yapi ikiwa karibia hotel kadhaa zikaamua kupika saubuhi
chakula kinacholiwa mchana,bila kujali ni ndizi,wali ama ugali na
maharage
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom