Hoteli wanayopika ugali asubuhi

Hoteli wanayopika ugali asubuhi

Mkuu... Hilo ni jina la Mzee mmoja alikuwa anaitwa Chacha Makaranga. Akaauma kuitwa bar / club yake Makaranga..

Basi enzi hizo za primary wakati imefunguliwa tulitunga wimbo wa mchakamchaka... Tuliimba hivi..

"Mwenyekiti wetu Chacha Makaranga, wakong'a wasing'ara ku inkundo ya mande"

Aione Mwita Maranya na platozoom...

Dah!Huu wimbo wenu wa mchakamchaka nimecheka sana.Kweli Taaarime unaifahamu vizuri.Kuna mtoto wake nilisoma nae sehemu.Hiyo kitu ya Marura karibu na round about acha,nilikuwa nikifika Tarime lazima nipige ripoti.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kama watu hapa hapa mjini wanakula viporo vya wali maharage, iweje washindwe kumemena nguna!!!

Kwa taarifa yako wale wakulima wa Kisukuma au Kikurya, huwa wanakula ugali mkubwa wa dona halafu pembeni kunakuwa na ugali mdogo wa sembe...huo ugali mdogo ndio unafanywa kama mboga...na hayo yote hufanyika sio asubuhi bali ni alfajiri jogoo wa kwanza tu akiwika[/QUOT

wasukuma wa sehemu gani bwana mkubwa wanaokula dona kwa mboga sembe
 
Tujulisheni jamani ni wapi hapo nipate ugali asubuhi maana chai au supu ni usmbufu bora ukandamize asubuhi mpaka jioni tena ukiwa wa ulezi ndio poa au mtama
 
Akha akha
Polepole dada yangu. Mgambo wa JF hawachezi mbali.

Halafu nimemkumbuka dada mmoja alikuwa madarasa kadhaa mbele, yeye kila mtihani wa mhula anakuwa wa mwisho darasani.
Lakini alikuwa na bidii ya kuja shule na kutii taratibu zoote. Wakati wanasoma majina ya watu wa mwisho, kabla Mwalimu hajamaliza wanafunzi wanaitikia kwa kumtaja jina "Kinyunyiiiiiiii Chonchoriiiiiiiii".
charminglady unamkumbuka?

Nakumbuka saaana aise.... Afu kuna jamaa mmoja mwenye hilo jina la mwisho yuko.hapa town ana mawe ya kutosha!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Dah!Huu wimbo wenu wa mchakamchaka nimecheka sana.Kweli Taaarime unaifahamu vizuri.Kuna mtoto wake nilisoma nae sehemu.Hiyo kitu ya Marura karibu na round about acha,nilikuwa nikifika Tarime lazima nipige ripoti.

Marura ni noma aiseee..... Afu alikuwa nazo kama tatu hivi, moja karibu na round about ya Serengeti, nyingine palr uwanja wa CCM na nyingine huku barabaraba Imani Hotel. Sijui kama bado zinaoperate????
 
Ndugu yangu umenikumbusha mbali. Ukifika Butiama, nyumbani kwa Baba wa Taifa, sehemu inaitwa Stendi, hapo saa 12 asubuhi tayari kuna ugali na nyama vinakuwa vimeshaiva. Hicho chakula wenyewe utasikia wanasema, "Lete rungu kwa kichuri". Maana yake ni ugali wa mtama uliochanganywa kwa mhongo kwa nyama ya mbuzi. Pembeni lazima kuwe na pilipili.

sisi watu wa Butiama tunapata taabu sana huku mikoani hakuna ugari wa muhogo 'Obhukima bhwa Amaribhwa'
 
Ndugu yangu umenikumbusha mbali. Ukifika Butiama, nyumbani kwa Baba wa Taifa, sehemu inaitwa Stendi, hapo saa 12 asubuhi tayari kuna ugali na nyama vinakuwa vimeshaiva. Hicho chakula wenyewe utasikia wanasema, "Lete rungu kwa kichuri". Maana yake ni ugali wa mtama uliochanganywa kwa mhongo kwa nyama ya mbuzi. Pembeni lazima kuwe na pilipili.
Hapo kwenye RED... Aaah umetuzuga mkuu! Mi si mkurya lakini kwa ufahamu niliopata kipindi cha nyuma nilipokuwa mitaa ya hao jamaa... KICHURI ni kinyesi cha mbuzi kilichochanganywa na nyongo... Ngoja na wenyewe waje watuelezee zaidi...
 
duh ni baraa ,butiama kuna wataalamu wa kuchoma nyama na ugali wa mhogo na ile kitu inaitwa kchuri asubuh na mapema ndio kifungua kinywa,nilikuwa butiama miezi kama 7 iliyopita nilipata iyo kitu mida ya asubuhi kama sa 2,kweli nilifurahia
nita visit butiama next month kukumbushia iyo kitu,kweli maisha ya kijijini yana utamu wake.

Miezi hii kichuri huwa kinapumzishwa. Mpango mzima ni kimoro au vitenge, kama wenyewe wanavyopenda kuita. Hii ni nyama pori iliyokaushwa. Kimoro kinapendeza zaidi wakati wa baridi kali. Hasa kilichochomwa ni balaa, maana lazima kuwe na chumvi iliyolowekwa kwenye bakuri ikikolezwa na pilipili kichaa. Hapo ukila lazima kiji-kamasi chembamba kikutoke! Hata kama ni baridi, utatokwa jasho tu!
 
mkuu hakuna cha kushangaza hapo inashangaza sana inategemeana ww unapatikana wapi maeneo gani na unafanya kazi gani.kama unapatikana dar maaeneo ya posta huwezi kutana na hii kitu vile vile kama unafanya zile kazi za kiofisi zaidi basi hii kitu kwako lazima utaiona ni adim sana.
njoo maeneo ya mwenge hii kitu utakutana nayo kwa sana tuu mkuu
 
Hapo kwenye RED... Aaah umetuzuga mkuu! Mi si mkurya lakini kwa ufahamu niliopata kipindi cha nyuma nilipokuwa mitaa ya hao jamaa... KICHURI ni kinyesi cha mbuzi kilichochanganywa na nyongo... Ngoja na wenyewe waje watuelezee zaidi...

kati ya watu walionishangaza kwa mwaka huu we ni wakwanza, kwani manyerere ameelezea kichuri ni nini? na mbaya zaidi kwa kujiamini unasema umezugwa,soma upya post ya manyerere kwa umakini utamwelewa kitu alichokieleza.
 
Miezi hii kichuri huwa kinapumzishwa. Mpango mzima ni kimoro au vitenge, kama wenyewe wanavyopenda kuita. Hii ni nyama pori iliyokaushwa. Kimoro kinapendeza zaidi wakati wa baridi kali. Hasa kilichochomwa ni balaa, maana lazima kuwe na chumvi iliyolowekwa kwenye bakuri ikikolezwa na pilipili kichaa. Hapo ukila lazima kiji-kamasi chembamba kikutoke! Hata kama ni baridi, utatokwa jasho tu!

ehee kimoro nacho ni hatari,nazani kitakuwa kinatoka serengeti,yaani ukikipata kimoro cha swala +ugali wa mhogo+bamia,udenda lazima utoke.
 
Ni sawa tu mkuu kupika ugali asubuhi maana wataalamu wa masuala ya lishe wanatuelekeza tupende kula msosi wa kutosha asubuhi na mchana alafu usiku tunakula kiduchu tu na tuache utamaduni wetu wa vice versa (asubuhi chai andazi moja na nusu alafu mchana na usiku tunashindilia)
 
Mkuu mbona hayo maneno ya kawaida kure kwetu, je nikianza kuibhaka si server zinajam!!!!

ni ya kawaida lakini ukiyatafsiri kwa kiswahili lazima ban ikumaliza,kuna bibi mmoja apo tarime mjini mitaa ya ronsoti kila asubuhi akiamuka anatoa matusi kwa mabinti zake ata bila sababu, adi majirani wanaamka, utasikia nyakundo ,msagani, kivumvu cha nyakwenu na mengine siyakumbuki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom