Hoteli wanayopika ugali asubuhi

Hoteli wanayopika ugali asubuhi

Kaka yangu hapo hali maana ana Vidonda vya tumbo...... Hahahaaa umenivunja mbavu Mkuu.
Ndugu yangu umenikumbusha mbali. Ukifika Butiama, nyumbani kwa Baba wa Taifa, sehemu inaitwa Stendi, hapo saa 12 asubuhi tayari kuna ugali na nyama vinakuwa vimeshaiva. Hicho chakula wenyewe utasikia wanasema, "Lete rungu kwa kichuri". Maana yake ni ugali wa mtama uliochanganywa kwa mhongo kwa nyama ya mbuzi. Pembeni lazima kuwe na pilipili.
 
Arusha,Manyara,Singida ugali asubuhi tena majogoo ndo mlo wetu. Mh Dr W.P. Slaa,Mh Tundu Lisu,Mh L.Nyalandu wanajua vizuri utaratibu huu wa lishe.Hata mimi wakati niko single nilikuwa nagonga zege asubuhi jijini DSM.
Wazee wetu zamani ndo mtindo wao wa kula,chakula cha asubuhi kiliheshimiwa sana,hasa kwa wanaume.Babu yangu aliwahi kunieleza kuwa wanaume hukung'oli wanawake majogoo,hivyo asubuhi ni vizuri ushibe.Chai asubuhi sio mpango kabisa.
 
duh ni baraa ,butiama kuna wataalamu wa kuchoma nyama na ugali wa mhogo na ile kitu inaitwa kchuri asubuh na mapema ndio kifungua kinywa,nilikuwa butiama miezi kama 7 iliyopita nilipata iyo kitu mida ya asubuhi kama sa 2,kweli nilifurahia
nita visit butiama next month kukumbushia iyo kitu,kweli maisha ya kijijini yana utamu wake.
 
we unashangaa hiuo unaopikwa asubuhi??/ wengine asubuhi tunakandamiza uliobaki jana usiku kwa maharage yasiyoungwa wala kuchemshwa...
 
unawajau wale jamaa wa tanesco wanaofanya kazi ya kubeba nguzo kwa mikono?
hao ndo wanategemea hotel kama hizo ili kazi ifanyike.
 
Last edited by a moderator:
Kwangu imekuwa news baada ya kukuta mgahawa mmoja jijini Dar wateja wake wakila ugali mida ya saa mbili asubuhi. Je hii ni kawaida?!
Maoni yako ni yapi ikiwa karibia hotel kadhaa zikaamua kupika saubuhi chakula kinacholiwa mchana,bila kujali ni ndizi,wali ama ugali na maharage

Mi huwa napata ugali wa moto pale Kidonge chekundu kwa Da chiku
 
Wabongo tuwe logic tubadilike na elimu zetu za kimapokeo mimi binafsi simshangai mtu anaekula ugali asubuhi-tena huko ngenenepa aisee kwa sababu asubuhi lazima ule chakula cha nguvu kama ugali!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mama bhoke,hebu niphatie ugari na kichuri.
 
canteen za vyuo nashauri waanze pika wali na ugali asubuhi,ili kuwasaidia wanafunzi ku save hela, badala milo mitatu ,wanafunzi watakula milo miwili yaani asubuhi na usiku
 
Arusha,Manyara,Singida ugali asubuhi tena majogoo ndo mlo wetu. Mh Dr W.P. Slaa,Mh Tundu Lisu,Mh L.Nyalandu wanajua vizuri utaratibu huu wa lishe.Hata mimi wakati niko single nilikuwa nagonga zege asubuhi jijini DSM.
Wazee wetu zamani ndo mtindo wao wa kula,chakula cha asubuhi kiliheshimiwa sana,hasa kwa wanaume.Babu yangu aliwahi kunieleza kuwa wanaume hukung'oli wanawake majogoo,hivyo asubuhi ni vizuri ushibe.Chai asubuhi sio mpango kabisa.

Mkuu nakukubalia umuhimu wa kupata kifungua kinywa iliyo na uzito japo ni muhimu pia kuangalia aina ya kazi aendayo kufanya mlaji! Imagine kufakamia ugali kwa nyama choma asubuhi wakati unaenda kukaa mapokezi-wewe ni receptionist! Si utaishia kusinzia kwenye desk ukihudumia wateja?
 
Mkuu tunaangalia tamaduni zetu waTz kwa kawaida ni mchama ama usiku ila hii ya asubuhi itawashangaza wengi

kwa nini ishangaze wengi wakati umeshahambiwa mikoa mingi ni kitu cha kawaida
 
kuna hotel ngapi mji uaoishi wanapika ugali asubuhi? na kama ni chache kwanini?

Njoo hapa zambia hakuna mambo ya chai hapa ishu ni ugali tu mapema sana

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Me nilifikiri umekuta watu wanakula matofari! kumbe ugali? sasa hapo chakushangaza ni nini?
 
Back
Top Bottom