Updates: Confirmed, ni Mama mtu mzima zaidi ya miaka 60 ambaye kwa sera ya wizara ya afya alipaswa kutibiwa kwa bima lakini pamoja na bima anadaiwa zaidi ya milioni 30 kutokana na kuwekewa oxygen kwa zaidi ya miezi miwili aliyolazwa hospitalini hapo.
Kitengo Cha uhasibu, menejimenti ya hospital ambayo ina viongozi wa dini pia ndiyo inayofanya haya. Tatizo la kukataliwa dhamana ni mgongano wa kisheria uliopo kwamba deni si la familia Bali ni la Marehemu hivyo kuliamishia kwa familia itasumbua kulipa.
Uongozi wa serikali wamekaa kimya na baadhi wameungana na Hospitali hiyo kwamba kinachofanyika ni sahihi. Kwa Mimi nadhani tatizo hizo hili la matumizi ya gesi ni kubwa kutokana na COVId na wanaopata changamoto hizi ni wazee zaidi. Endapo serikali itaendelea kujitenga na gharama za matibabu ya covid familia nyingi zitaongia mgogoro na serikali pamoja na Hospitali.
Wizara ya Afya najua mnaelewa mkasa huu kwa sababu naambiwa familia hiyo imeripoti serikalini zaidi ya wiki na nusu Sasa na hakuna hatua.
Awali nilidhani Hospitali ndiyo ina makosa kumbe ni msimamo wa baadhi ya viongozi japo unapingana na tamko la serikali. Nani yupo sahihi? Msimamo wa serikali, msimamo wa hospital na ofisi za Wilaya serikali Wilaya?
Naendelea kuchimba ntaleta majina ya mhusika na eneo exactly msiba ulipo ili vyombo vya habari vifike kuanika ukweli