Tetesi: Hospitali ya Seliani Arusha inayomilikiwa na Kanisa yazuia mwili wa Marehemu wakidai walipwe fedha za matibabu cash

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nimepata Taarifa kutoka kwa familia moja ambao wameoa huko Mkoani Arusha zikisema walipata msiba wa Mkwe zaidi ya wiki Sasa lakini mazishi hayajafanyika kwa sababu Hospitali inadai haitotoa mwili hadi walipwe deni la matibabu. Taarifa zinadai wanafamilia wamepeleka zaidi ya nusu ya fedha na hati za nyumba lakini Hospitali imekataa kutoa mwili.

Hii inatokea siku chache baada ya Viongozi wa awamu ya sita kupiga marufuku utaratibu huu wakutoa adhabu kwa Marehemu au kulazimisha familia kulipa frdha ambazo kiukweli awana uwezo nazo.

Nazidi kufuatilia jina la wahusika na viongozi waliohusika kupingana na maelekezo ya Mhe. Rais na ntawaweka adharani hapa pale ntakapofanikiwa kupata Taarifa rasmi.

Aidha, ni wakati muafaka wizara ya Afya kufuatilia kadhia hii ambayo naambiwa imeripotiwa kwa mkuu wa Wilaya na Mganga mkuu na hakuna hatua walizochukua Hadi Sasa. Wizara mnapaswa kusimamia kwa vitendo maelekezo ya Mhe Rais ikiwezekana mkatoa mwongozo wa Nini hospital binafsi na hospital za serikali zifanye pale wanapobaini deni la mgonjwa linaongezeka kuliko kung'ang'ana na mwili wa Marehemu ambao kwa vyovyote vile hautaweza kulipa hizo gharama.

Lakini pia taasisi za dini angalieni utaratibu huu mnaotumia kwenye taasisi zenu
 
Najua wengi mtakimbilia KUSEMA au mnawaza itakuwa ya wakatolik ila jamani sio,. ni ya LUTHERAN
 
Juzi kati niliandika kwamba bado zipo hospital zinakiuka maelekezo ya serikali

Tatizo matamko ya serikali yanatolewa kisiasa, na hapa usishangae Waziri akamshukia Mganga Mkuu au Dc kwa uzembe.

Vinginevyo wanafamilia wakiandamana kwenda Hospitali ndo utasikia matamko ya DC na RC kuhusu kadhia hizi.

Kwa uzi huu subirini mtasikia watakavyocharuka kutetea ugali. Ila pia kanisa linapaswa kuwa Suluhu kwa mambo yanayokiuka utu. Hii Ni kashfa kwa kanisa linalomiliki hii hospital endapo itabainika ni kweli
 
Updates: Confirmed, ni Mama mtu mzima zaidi ya miaka 60 ambaye kwa sera ya wizara ya afya alipaswa kutibiwa kwa bima lakini pamoja na bima anadaiwa zaidi ya milioni 30 kutokana na kuwekewa oxygen kwa zaidi ya miezi miwili aliyolazwa hospitalini hapo.

Kitengo Cha uhasibu, menejimenti ya hospital ambayo ina viongozi wa dini pia ndiyo inayofanya haya. Tatizo la kukataliwa dhamana ni mgongano wa kisheria uliopo kwamba deni si la familia Bali ni la Marehemu hivyo kuliamishia kwa familia itasumbua kulipa.

Uongozi wa serikali wamekaa kimya na baadhi wameungana na Hospitali hiyo kwamba kinachofanyika ni sahihi. Kwa Mimi nadhani tatizo hizo hili la matumizi ya gesi ni kubwa kutokana na COVId na wanaopata changamoto hizi ni wazee zaidi. Endapo serikali itaendelea kujitenga na gharama za matibabu ya covid familia nyingi zitaongia mgogoro na serikali pamoja na Hospitali.

Wizara ya Afya najua mnaelewa mkasa huu kwa sababu naambiwa familia hiyo imeripoti serikalini zaidi ya wiki na nusu Sasa na hakuna hatua.

Awali nilidhani Hospitali ndiyo ina makosa kumbe ni msimamo wa baadhi ya viongozi japo unapingana na tamko la serikali. Nani yupo sahihi? Msimamo wa serikali, msimamo wa hospital na ofisi za Wilaya serikali Wilaya?

Naendelea kuchimba ntaleta majina ya mhusika na eneo exactly msiba ulipo ili vyombo vya habari vifike kuanika ukweli
 
Kumbuka hospital hyo inahitaji pesa kulipa wafanyakazi.

Kama serikali inataka hvyo ni bora serikali ibebe majukumu yote ya marehemu kulipa garama za hospital.

Unakuta mgonjwa katumia zaidi ya mil 30 na bahati mbaya amefariki. Unazani hospital za private itasemehe tu.
 
Kumbuka hospital hyo inahitaji pesa kulipa wafanyakazi...

Kama serikali inataka hvyo ni bora serikali ibebe majukumu yote ya marehemu kulipa garama za hospital..

Unakuta mgonjwa katumia zaidi ya mil 30 na bahati mbaya amefariki.. Unazani hospital za private itasemehe tu...
Hapo ni serikali ilipie sio kulaumu hospital maana private hospital hazina ruzuku kama za serikali
 
Hizi changamoto zinajitokeza kwasababu serikali imeshindwa kua na sera inayoeleweka ya matibabu.

Swala la bima tu lenyewe liko kimtindo mtindo kiasi ambacho wananchi wengi na watoa huduma hawalielewi.

Sasa matukio kama haya serikali ndio iliyotakiwa itoe ufumbuzi wa nini kifanyike ili kurejesha gharama alizotumia marehemu nasio kuja tu na matamko bila kusema how fedha zitalipwa.

kwasabsbu ukisema tu marehemu asidaiwe usifikiri kuna ndugu atakaye lipia ndugu zao watakaofariki.sasa jiulize ni wagonjwa wangapi wanafariki uko mahospitalini.

Na hili linakuja kwasababu hospitali nyingi mgonjwa akishalazwa anaendelea kupatiwa huduma kisha malipo badae. ila ingekua ni No pesa no huduma ingekua tabia mbaya japo hilo lingemaliza hii kazia.

Kwahiyo badala yakulaumu hospitali tuiulize serikali ituambie swala la matibabu na madai ya marehemu yanatatuliwaje.
 
Back
Top Bottom