Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Nimepata Taarifa kutoka kwa familia moja ambao wameoa huko Mkoani Arusha zikisema walipata msiba wa Mkwe zaidi ya wiki Sasa lakini mazishi hayajafanyika kwa sababu Hospitali inadai haitotoa mwili hadi walipwe deni la matibabu. Taarifa zinadai wanafamilia wamepeleka zaidi ya nusu ya fedha na hati za nyumba lakini Hospitali imekataa kutoa mwili.
Hii inatokea siku chache baada ya Viongozi wa awamu ya sita kupiga marufuku utaratibu huu wakutoa adhabu kwa Marehemu au kulazimisha familia kulipa frdha ambazo kiukweli awana uwezo nazo.
Nazidi kufuatilia jina la wahusika na viongozi waliohusika kupingana na maelekezo ya Mhe. Rais na ntawaweka adharani hapa pale ntakapofanikiwa kupata Taarifa rasmi.
Aidha, ni wakati muafaka wizara ya Afya kufuatilia kadhia hii ambayo naambiwa imeripotiwa kwa mkuu wa Wilaya na Mganga mkuu na hakuna hatua walizochukua Hadi Sasa. Wizara mnapaswa kusimamia kwa vitendo maelekezo ya Mhe Rais ikiwezekana mkatoa mwongozo wa Nini hospital binafsi na hospital za serikali zifanye pale wanapobaini deni la mgonjwa linaongezeka kuliko kung'ang'ana na mwili wa Marehemu ambao kwa vyovyote vile hautaweza kulipa hizo gharama.
Lakini pia taasisi za dini angalieni utaratibu huu mnaotumia kwenye taasisi zenu