DOKEZO Hospitali ya Halmashauri ya Kibondo kuna uonevu mkubwa kwa watumiaji wa Bima

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mapema jana(Novemba 30, 2023), wagonjwa tuliokuja hapa hospitalini kutibiwa tulikutana na kadhia ya kutukanwa na muhudumu aliyekuwa chumba cha wagonjwa wa nje(OPD) wanaotibiwa kwa bima.

Mhudumu huyo alituweka benchi tangu saa tatu asubuhi Hadi saa kumi na nusu jioni aliporudi akatuambia muda wa vipimo umeisha hivyo hataweza kutuandikia vipimo kesho yake!

Kuna mama ambaye ni diwani tulikuwa naye, alipomhoji huyo kwamba alikuwa wapi tangu asubuhi hatuhudumiwi, akajibiwa "hili siyo eneo la Siasa, Ni la matibabu"

Tulirudi hospitalini Ijumaa asubuhi lakini Hadi muda wa saa tano walikuwa wanafanya usafi, wagonjwa wa BIMA hatuhudumiwi ila wengine wanahudumiwa.

Ijumaa Kuna clinical officer tuliyemfahamu kwa jina moja la Elivia, anawapitisha mlango wa nyuma wagonjwa wa kabila lake(Wahaya) na wengine anaofwhamiana nao na kuwaandikia vipimo vya maabara kwa hiyo kila saa tunashangaa tu mgojwa ambaye hakuwa kwenye foleni anatokea na kuelekea maabara na baadaye kurudi chumba cha daktari, sisi wengine tupo kwenye viti Kama Jana tu.

Hii changamoto siyo ya Mara ya kwanza. Mwaka Jana Mkurugenzi wa halmashauri(Diocles Rutema Mugishagwa) alikuja kuwaonya madaktari baada ya majeruhi mmoja wa ajali ya barabarani kufia kwenye kiti baada ya kukosa huduma za dharura kwa zaidi ya masaa mawili.

TUNAOMBA SERIKALI ICHUNGUZE NA ICHUKUE HATUA KWA wahudumu hao tuliowataja maana wanasababisha maudhi na usumbufu kwa wagonjwa.
 
Back
Top Bottom