Wanasema hakuna madhara makubwa kama mwanamke kukosa akili. Kujihusisha kimapenzi na bosi wako tena mwenye sifa ya uhuni na kuyaanika mahusiano yenu mtandaoni ni ufinyu wa fikra. Kuzaa watoto wawili na mwanaume ambaye hajakuoa, halafu ukamuacha kwenda kwingine na ukaanika tena mtandaoni ni ufinyu wa fikra. Kubwa kuliko yote ni kushiriki kuchafua jina la mzazi mwenzio, ambaye bado ni sehemu kubwa ya maisha ya watoto wenu na yako kwa ujumla. Watoto wao watakuwa na kukumbushwa yote haya kupitia mitandao. Zamaradi amefeli sana.