Salaam, Shalom!!
Ulichokifanya ni WAJIBU wako kama kiongozi, ila Si vibaya kukupongeza sababu wamekuwapo wakuu wa mikoa wengi tangu uhuru lakini hawakupata mafanikio kama uliyofikia Hadi sasa!! Kongole!!!🙏
Kupambana na biashara ya ukahaba inahitaji mtu kuwa na akili kama ya Mwendawazimu, katika hili nakupongeza sana.
Umetumia GIA kubwa, ya kubomoa nyumba zilizotumiwa kufanya biashara ya madanguro, baadhi ya nyumba,milango imengolewa MADIRISHA nknk ,Na nyumba zilizokumbwa na kadhia hiyo ni nyumba za uswahilini.
Naamini HUJAKURUPUKA kuchukua hatua hizo, naamini unazo SHERIA zinazokulinda kufanya hivyo, kwamba ikitokea wamiliki wa nyumba hizo wakifungua kesi mahakamani kudai nyumba zao, una pa Kutokea, naamini zipo SHERIA zitakulinda kwamba, iwapo nyumba yenye leseni ya makazi ikitumika kufanya biashara haramu nyumba inavunjwa....
Tumeona, magari au marori yaliyobeba mihadarati yakitaifishwa bila kujali mmiliki alihusika au hakuhusika kubeba mihadarati hiyo.
Umeenda mbali na kupiga MARUFUKU mabaa kutowakaribisha wadada hao haramu.
FAIDA ZA KUTOKOMEZA MADANGURO NA BIASHARA HARAMU YA UKAHABA.
1. KUDHIBITI VITENDO VYA USHOGA .
Madanguro pia yalikaribisha mashoga, hivyo umepiga ndege wawili jiwe moja.
2. KUONDOA AJIRA HARAMU YA WATOTO.
Ukahaba ulifanywa Hadi na watoto chini ya miaka 18, hili lingetufikisha pabaya sana.
3.KUDHIBITI MADAWA YA KULEVYA.
Ukahaba na uuzaji na Ununuzi madawa ya kulevya ulienda sambamba hivyo kudhibiti ukahaba ni kudhibiti biashara hiyo pia.
4. KUIMARISHA MAADILI KATIKA JAMII.
Madanguro yaliondoa Heshima ya mzazi mbele ya JAMII maana vitendo hivyo haramu vilifanyika hadharani katika nyumba za familia watoto wakiona.
5. KUDHIBITI VITENDO VYA UHALIFU.
MAKAHABA na majambazi hushirikiana kuumiza familia nyingi, kudhibiti madanguro itapunguza uhalifu huo.
6. KUIMARISHA NDOA.
NDOA nyingi zilivunjika sababu ya tamaa ya wanawake kutamani pesa haramu Kutoka biashara haramu ya kujiuza, umesaidia NDOA nyingi zitaimarika.
7.PANYA ROAD& WATOTO MITAANI WATAPUNGUA.
Ukahaba ni chanzo Cha kutupwa hovyo watoto wachanga, utoaji mimba na kuzagaa hovyo watoto wasio na malezi ya wazazi mitaani.
KUDHIBITI ukahaba, kutusaidia kuinua malezi ya watoto, Panya road pia WATAPUNGUA.
ANGALIZO: Hatua ulizochukua Kwa madanguro, kamwe usijethubutu kufanya kwenye nyumba za Ibada zisizo na KIBALI au usajili. Nimewahi kukusikia ukisema mnaweza siku moja kufuta makanisa.
Njoo Polepole, Angalia Rungu ulilolishika lisirudi kukuponda. Hayupo mwenye mamlaka na uwezo kufuta Kanisa, kujaribu kufuta makanisa ni kutunishiana misuli na Muumba, mshindi katika pambano Hilo anajulikana.
Lakini Kwa hatua ulizochukua kuhusu madanguro nakupa kongole 🙏.