Chanzo channel ten habari 3/11/2023 saa moja usiku.
Wakazi wa Jiji la DSM tunampa hongera RC Chalamila kwa kupambana na biashara haramu ya kuuza miili/ngono, biashara hii imekuwa chanzo kikuu cha maambukizi ya ukimwi lakini pia mmomonyoko wa maadili kwenye jamii.
Naomba viongozi wwngine kuanzia wenyeviti wa mitaa, madiwani, wakuu wa wilaya kwenye kila eneo wapambane na utovu huu wa maadili.
Sisi wananchi tutaendelea kufichua vyanzo vyote vya biashara ya ngono.
---
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa siku tano kwa wamiliki wa madanguro akiwataka kuyavunja wenyewe, na kwamba wasipofanya hivyo, atataifisha nyumba hizo.
Pia amewaagiza wamiliki wa baa zote ambazo nje kunafanyika biashara hiyo kuhakikisha wanawaondoa vinginevyo atazifunga.
Chalamila ametoa maagizo hayo leo ijumaa Novemba 3,2023 wakati alipotembelea madanguro yaliyovunjwa na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni.
Novemba Mosi mwaka huu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akishirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo Saad Mtambule, walivunja madanguro hayo na kuwakamata baadhi ya wasichama waliodaiwa kuhusika kufanya biashara hiyo.
Chalamila amesema,nyumba zilizopewa leseni kwa ajili ya makazi na kubadilishwa matumizi ni kosa kisheria na kuwataka kuzivunja ndani ya siku tano."Natoa siku tano nyumba zote zilizojengwa na kugeuzwa madanguro muwe mmezivunja vinginevyo ntazitaifisha,"
"Na wale wamiliki wa baa ambazo nje biashara hii inafanyika, wakina dada wanajipanga,ikome maramoja vinginevyo nitazifinga zote,hatuwezi kulea ujinga wa namna hii," amnesema Chalamila.
Hata hivyo RC huyo amewataka Wakuu wa Wilaya katika mkoa huo kuhakikisha operesheni hiyo inaendelea kwenye maeneo yote ya kiutawala na kwamba wahakikishe biashara hiyo inakomneshwa.
Kuhusu biashara ya kusingwa mwili (massage) amesema baadhi ya saluni zinatoa huduma hiyo.
Alisema siku chache zilizopita kuna mtu alifariki kwenye chumba akipatiwa huduma hiyo,na kwambani ngumu kujua ni nini kilichompata na kuwataka viongozi hao kuzichunguza.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule alisemna eneo hilo lina nyumba nane zenye leseni za makazi lakini zimegeuzwa kuwa madanguro.
Alisema Juni mwaka huu walifanya kikao na wamiliki wa nyumba hizo pamoja na viongozi wa dini, na kukubaliana kuzibomoa lakini wakaomba kupewa miezi sita ili waweze kuondoka, japo walikuta biashara hiyo ikiendelea.
Amesema baada ya kukuta biashara hiyo inaendelea, waliamua kuchukua hatua ikiwemo kung'oa milango na kuwataka wamiliki wa nyumba hizo kuzivunja wenyewe kabla hawajachukua hatua zaidi.
"Tutaendelea kuchukua hatua kama ulivyotuelekeza, wakina dada hao wanazo kazi nyingi ambazo wangeweza kuzifanya ikiwemo kukopa mikopo ya asilimia kumi na kufanya biashara," alisema.
"Tumeendelea kushirikiana na baadhi ya kina dada ikiwemo watatu waliokuwa wakifanya biashara eneo hili wapo tuliowashauri, wakachukua ushauri wetu lakini wengi wamelikaidi," amesema Mtambule.
Amebainisha kuwa wote wenye madanguro wanafahamika kwa muda mrefu na kwamba hatua hiyo ya utekelezaji ilikuwa ni suala la muda tu, hivyo watahamia na maeneo mengine.
Kwa upande wake Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge amesema wamedhamiria kukomesha biashara hiyo ilivyokuwa inadhariirisha utu wa mwanamke kwa muda mrefu. Amesema watu waliokuwa hapo wameamua kukaa kimya na kusababisha watoto wadogo kufanya vitendo visivyo na maadili wakiwemo wanafunzi.
"Cha kusikitisha biashara hiyo inaanzia Sh 1,000 hadi 3,000, pale Halmashauri kuna mikopo ya asilimia kumi timewaambia waje wakope waachane na hii biashara wengi wao hawataki," amesema.