FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,883
- 109,213
Hakika inabidi tukupe hongera kubwa sana mama Samia, umetufundisha Watanzania kuwa "matendo huongea kwa sauti kuliko maneno" (actions speaks louder than words).
Tukitazama mitandaoni na jinsi mambo yanavyodhaniwa na wapenda maneno kuwa ndiyo yalivyo, inabidi nikupe heko na hongera nyingi sana tena sana mama Samia, tumeona uchapaji kazi wako na tumeona jinsi unavyotutakia mema Waanzania bila kukurupuka.
Wanaotaka maandamano wanafanya, wanaotaka mikutano ya hadhara wanafanya, wanaotaka kwenda mahakamani wanakwenda, wanaosema hovyo wanasema. Wewe tuliiii, mama unawatia watu "presha" hivyo. Tulidhani unatufanyia tashtiti, kumbe la hasha, wewe unachapa kazi. Sasa nimeamini, kiongozi wa kweli hutenda, Wengine bila maneno maneno.
Kweli umetufundisha somo kbwa sana sote, umetufundisha tuwe watendaji zaidi ya waongeaji. Binafsi naamini na umezidi kuniyakinishia hilo, kuwa wasemaji sana hutaka yaaminiwe maneno yao siyo vitendo vyao na uhalisia uliopo.
Tulitaka na tunatamani sana mama ukurupuke, kama tulivyozoeshwa, lakini kwa hekima zako, unatuwachia tuwe huru kwa maoni yetu. wewe unachapa kazi tu.
Mama tuliyozowea maneno maneno na umbeya unatutia "plesha". Tunaona kama unatufanyia tashtiti.
Mama nakupongeza kwa hilo, tulishazowea siasa za kufokafoka na kuaminishwa maneno ya kuliko uhalisia.
Mama ahsante kwa kutufundisha kwa vitendo, inabidi tubadili mbinu. Twende kama unavyokwenda wewe "boss wetu" kisheria, kidemokrasia, kiusalama na amani, siyo kimihemko.
Kweli nimeamini "Matendo huongea kwa sauti kuliko maneno".