Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,270
- 9,716
Ndugu zangu Watanzania,
Rasmi sasa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan ametimiza umri wa miaka 64 kutokana na kuwa alizaliwa siku ya jumatano ya tarehe 27 januari 1960.
Kwa hakika ni furaha kuona Rais wetu akitimiza miaka hiyo akiwa mwenye afya njema,nguvu na uimara mkubwa sana katika kulitumikia Taifa letu ambalo analipenda kwa dhati ya moyo wake.ameonyesha upendo wake kwa Taifa hili kwa maneno,kauli na Matendo.
Mikono yake imegusa maisha ya watu wengi na kuwapa matumaini,tabasamu na furaha. Kauli na Maneno yake yameinua matumaini ya watu wengi sana waliokuwa wamekata tamaa.macho yake yamemtizama kila mtu aliyehitaji msaada.ulimi wake umelileta na kuliunganisha Pamoja Taifa letu.
Mungu aendelee kumjalia maisha marefu yenye amani,baraka na furaha .Amjalie afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania ili tufaidike na kipawa na Karama kubwa ya kiuongozi aliyonayo pamoja na upendo mkubwa kwa Taifa letu.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.