Lukuvi kafanya kazi mzuri ila kosa lake ni kujiunga na hao jamaa wa 2025.Salam!
Naweza kusema Mh. William Lukuvi ni miongoni mwa viongozi wachache walioweza kusifiwa kwa utendaji wao angali wakiwa hai
Jana baada orodha ya mawaziri waliochwa kwenye baraza la mawaziri kutoka nimeona kwenye mitandao ya kijamii na huku mtaani watu wengi wakiumia sana kwanini mh Rais kamuacha lukuvi wakati huyu kiongozi alikuwa ni mchapa kazi mahiri.
Kinachonishangaza kwanini watu wengi wameuzunishwa na kuondolewa kwake. Hakika hapa kuna kitu cha kujifunza kutoka kwa kiongozi huyo
Kwenu viongozi tunapopewa nafasi za kutumikia taifa hili tujitahid kuzitendea haki na tusiwe waimba mapambio tuige mfano wa Mh Lukuvi.
Kila la kheri William Lukuvi katika majukumu yako.