Mapendekezo ya wananchi: Muundo wa Baraza la Mawaziri kwa Serikali ya Awamu ya Tano

lazima ukae

JF-Expert Member
May 15, 2013
788
380
Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumtangaza rais mteule wa awamu ya tano, nani unahisi atateuliwa na mheshimiwa John Pombe Magufuli kuwa Waziri Mkuu ?

Unapendekeza Muundo wa Baraza la Mawaziri kwa Serikali ya Awamu ya Tano uweje?
Natambua JPM ana kazi kubwa ya kuteua baraza la mawaziri. Katika kuchangia juu ya suala hilo, kama mwananchi wa kawaida napendekeza aangalie mawazo haya pia:

1. Harrison Mwakyembe, Waziri Mkuu
2. Asha Rose Migiro, Mambo ya Nje
3. January Makamba, Afrika Mashariki
4. Sospter Muhongo, Maji, Nishati na Madini
5. William Lukuvi, Ardhi, Maliasili na Mazingira
6. Adadi Rajabu, Mambo ya Ndani
7. Kabudi Palamagamba, Katiba na Sheria (mbunge wa kuteuliwa)
8. Mwigulu Nchemba, Fedha na Uchumi
9. Luhiga Mpina, Viwanda, Biashara na Utalii
10. Stephen Wassira, Ofisi ya Rais Kazi Maalum (mbunge wa kuteuliwa)
11. Diodurus Kamala, Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi
12. Aggrey Mwanri, TAMISEMI (mbunge wa kuteuliwa)
13. Mwele Malecela, Afya (mbunge wa kuteuliwa)
14. Assumpter Mshama, Maendeleo ya Jamii
15. Mohamed Seif Khatibu , Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
16. Jumanne Maghembe, Kilimo na Misitu (inajumuisha Uvuvi na Mifugo)
17. Makame Mbarawa, Habari na Mawasiliano
18. Ramo Makani, Miundombinu na Uchukuzi
19. Sifuni Mchome, Elimu, Sayansi na Teknolojia
20. Charles Makakala, Ulinzi na JKT (mbunge wa kuteuliwa)
21. Juma Nkamia, Habari, Utamaduni na Vijana
22. Jennister Mhagama, Uratibu wa Bunge
23. Lazaro Nyalandu, Ofisi ya Rais Uwekezaji na Mahusiano

24. Angela Kairuki, Naibu Ardhi, Maliasili na Mazingira
25. Kangi Lugora, Naibu TAMISEMI
26. Ummy Mwalimu, Naibu Habari, Utamaduni na Vijana
27. Janet Mbene, Naibu Viwanda, Biashara na Utalii
28. Charles Mwijage, Naibu Maji, Nishati na Madini


Haka ni ka-baraza kadogo, kalikozingatia mabadiliko ya wizara, na si kila wizara iwe na naibu. Awape hao kwanza changamoto kisha ataangalia wapi pa kurekebisha mbele ya safari kulingana na utendaji na changamoto. Kwa sasa asijali sana suala la ukabila, aangalie "kazi tu".
Ni vizuri kuwe na baraza dogo lenye wizara zisizozidi 17. Lenye mawaziri Kama ifuatavyo:
Waziri Mkuu- Harrisson Mwakyembe
Waziri wa M/Nje na Ushirikiano wa Kimataifa- Asha-Rose
Waziri wa Ulinzi - Hussein Mwinyi
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii-
Waziri wa Habari na Mawasiliano- Prof. Mbarawa Makame
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Ushirika-
Waziri wa Mambo ya Ndani-
Waziri wa Maji, Nishati na Madini- Prof. S. Muhongo (Awe na Manaibu 3)
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia -
Waziri wa Ardhi, Maliasili, Utalii na Mazingira - W. Lukuvi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Maendeleo ya Jamii-
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji-
Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi-
Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana- Januari Makamba
Waziri wa Maendeleo ya Miundo Mbinu-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano-

NB. Shughuli za michezo ziende Tamisemi na shughuli za Utamaduni ziende Maliasili. Shughuli za EAC zirudi Foreign
- nafasi ambazo hazina majina tupate sura mpya kabisa.
Kulingana na ninavyofahamu utendaji wa Rais Mteule, Bw. Magufuli, natabiri kuwa muundo na Baraza lake la Mawaziri litakuwa kama ifuatavyo:

Waziri Mkuu
Dkt. Harrison Mwakyembe.

Ofisi ya Rais

  1. Utumishi ? Dr. Norman Sigalla
  2. Mipango na Uratibu ? Angelina Mabula
  3. Utawala Bora ? Dkt. Hamis Kigwangalla

Ofisi ya Makamu wa Rais

  1. Muungano - Dr. Hussein Mwinyi
  2. Mazingira ? George Simbachawene

Ofisi ya Waziri Mkuu

  1. TAMISEMI - Dr. Medard Kalemani Chananja
  2. Sera, Uratibu na Bunge ? Mwigulu Nchemba

Wizara Zinazopendekezwa na Mawaziri Wake


  1. Afya na Ustawi wa Jamii ? Dk. Faustine Ndugulile
  2. Ushirikiano wa Afrika Mashariki ? Mahadhi J. Maalim
  3. Ulinzi na Mambo ya Ndani ya Nchi ? Balozi Adadi Rajab
  4. Ujenzi na Uchukuzi ? January Makamba
  5. Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Ummy Mwalimu
  6. Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ? Dr. Asha Rose Migiro
  7. Katiba na Sheria ? Prof. Palamagamba Kabudi (UDSM) (Rais amteue kuwa mbunge)
  8. Habari, Kazi, Ajira, Utamaduni na Michezo ? Leonidas Gama
  9. Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ? Prof. Makame Mbarawa (Rais amteue kuwa mbunge)
  10. Ardhi, Nyumba na Makazi ? William Lukuvi
  11. Maji, Mifugo na Uvuvi ? Kangi Lugola
  12. Kilimo, Chakula na Ushirika - Dr. Mathayo David Mathayo
  13. Maliasili na Utalii ? Charles Kitwanga
  14. Fedha, Uwekezaji na Uwezeshaji ? Amina Salum Ali
  15. Nishati, Madini na Viwanda ? Prof. Sospether Muhongo
  16. Elimu na Mafunzo ya Ufundi ? Jenista Mhagama

TUONE UTABIRI WANGU UTATIMIA KWA KIWANGO GANI WAKATI UKIFIKA. ALAMSIKI.
1. Waziri Mkuu wa Tanzania: Mmoja kati ya vijana hawa - Mwigulu Nchemba au Dr Hamis Kigwangalla ataweza kwenda na kasi ya Dr John Pombe Magufuli

2. Ofisi ya Rais (Mambo yote): William Lukuvi

3. Ofisi ya M/Rais (Mambo yote): Saada Mkuya

4. Ofisi ya W/Mkuu - TAMISEMI: Dr Hamis Kigwangalla (Kama asipoteuliwa kuwa waziri mkuu)

5. Ofisi ya W.Mkuu - Sera, Uratibu, Bunge, Katiba na Sheria: Ummy Mwalimu

6. Fedha, Uchumi na Mipango: Mwigulu Nchemba (Kama asipoteuliwa waziri mkuu) au Balozi Dr. Deodorus Kamala

7. Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda, Uwekezaji, Uwezeshaji, Masoko na Biashara: Anthony Diallo (Mbunge wa Kuteuliwa) au Dr. Kalemani au Mwigulu Nchemba (kama asipoteuliwa kuwa waziri mkuu)

8. Maji, Madini na Nishati: Prof. Sospeter Muhongo

9. Afya, Jinsia, Maendeleo ya jamii, Ustawi wa Jamii: Dr Hamis Kigwangalla (kama asipoteuliwa waziri mkuu)

10. Elimu, Sayansi, teknolojia, mafunzo ya ufundi na elimu ya juu: Prof. Makame Mbarawa

11. Mambo ya Nje, Afrika ya Mashariki na ushirikiano wa kimataifa: January Makamba (kama asipoteuliwa waziri mkuu) au Balozi Dr. Deodorus Kamala

12. Mambo ya Ndani: Balozi Adadi Rajabu au Shamsi Vuai Nahodha/Dr Hussein Mwinyi

13. Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa: Dr Hussein Mwinyi au Shamsi Vuai Nahodha

14. Ardhi, Nyumba, Maliasili na Utalii: George Simbachawene

15. Habari, Utamaduni, Michezo, Kazi na Vijana: Hawa Ghasia

16. Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano: Charles Kitwanga


NAIBU MAWAZIRI

1. Uchukuzi nk - Peter Serukamba
2. Habari nk - Stephen Massele
3. Ardhi nk - Angella Kairuki
4. Mambo ya Ndani - ? Zanzibar
5. Nje nk - Hamad Masauni au ? Zanzibar
6. Elimu nk - Dr Faustine Ndugulile
7. Afya nk - Angelina Mabula
8. Maji, Madini nk - Charles Mwijage
9. TAMISEMI - Kassim Majaliwa na au Leonidas Gama
10. Kilimo nk - Dr. Ole Nasha au Dr. Hadji Mponda
11. Fedha nk - Janeth Mbene

NB: Tumezingatia uwiano wa mikoa, mahitaji ya muungano, wakilishi wa jinsia, umri, ubunifu na uwezo wa kukimbia na spidi ya Rais Magufuli. Pia Baraza la Mawaziri la Magufuli halitozidi Wizara 17, na litakuwa na Naibu Mawaziri wachache sana, wasiozidi 15.

Kila zama zina kitabu chake, huu ni uongozi wa tano na serikali ya Dr. Magufuli. Bila shaka katika watanzania waliopo kwenye wakati mgumu zaidi miongoni mwao ni rais wetu kipenzi Dr. Magufuli, hii ni kwa kuzingatia yupo katika wakati wa kusuka kikosi chake kwa maaana ya wasaidizi wake kuanzia ‪#‎wazirimkuu‬ pamoja na mawaziri na manaibu wao.

Kama mtanzania hii ni fursa yangu adimu kutoa maoni na uchambuzi wa namna ambavyo nadhani inaweza kuwa sehemu ya kuchagiza namna ya kulisuka baraza hasa kimuundo na si nani akae wapi, la hasha endapo ikitokea ulazima wa kuangalia nani awekwe wapi, tutashauri vigezo vitakavyomulika sifa za waziri pamoja na muundo wa kuiitathimini.

Kupitia sanduku la kura watanzania tumetoa mamlaka kwa viongozi wetu kutekeleza sera zao kwavyo ni fursa yao sasa kupanga timu zao kadri watavyoona inafaa katika kutekeleza ilani zao vile vile wao wanawajua zaidi wanaowazunguka kuliko sisi. La hasha kazi yetu ni kushauri tu, na haijawahi tokea ushauri ikawa ni jambo la lazima, kwavyo ni hiyari kuuchukua au la kadri mshauriwa atakavyopendezewa nao.

Katika hoja ya kuunda baraza la mawaziri ningeanza na kuangazia dhana nzima ya utendaji na uwepo wa wizara, najua wajua ila yafaa kukumbushana kwamba kazi kubwa ya wizara ni kushughulikia masuala ya kuunda sera pamoja na kusimamia sera husika, kwamba kazi ya utendaji si ya idara za wizara bali ni jukumu la taasisi zilizo chini ya wizara husika. Hali ya sasa ni tofauti kidogo maana wizara nyingi zinajishughulisha na masuala ya utendaji, mathalani wizara ya viwanda kutoa baadhi ya leseni za biashara katika mfumo huu lazima wafanye ukaguzi kwenye hizo biashara (due diligence), ilitosha BRELA na halmashauri kubeba hili zigo, vile vile nimepata kusikia wizara za kilimo na uvuvi kufanya shughuli za ukaguzi ambazo ni utendaji moja kwa moja, utakuta wizara inakagua samaki bandarini, (iyamkini mamlaka nyingine nao wapo wanakagua samaki hao hao) ama pale airport ya dar kuna desk la watu wa kilimo kufanya ukaguzi mbalimbali sasa kazi hizi zilipaswa kupelekwa kwenye taasisi zilizopo chini ya wizara husika na kama hakuna taasisi hizo basi taasisi nyingine yeyote chini ya wizara husika yenye walau mlengo wa shughuli husika ilipaswa ibebeshwe jukumu hilo.

Kimsingi ufanisi wa utawala au uongozi wowote ule unabebwa na mambo makuu mawili, yaani usimamizi makini na wa karibu (effective close supervision) pamoja na mahudhurio ya mara kwa mara katika jambo husika yaani (constant attendance) na falsa hii nimejifunza kwenye shughuli zangu za kilimo kwamba ili uweze kuvuna na kupata tija katika kilimo huna budi kuhakikisha close supervision na constant attendance havikwepeki njee ya hapo utavuna magugu. Msingi huu unajenga dhana nzima ya kuwa na mfumo thabiti wa ufuatiliaji pamoja na kufanya tathimini (effective and efficient monitoring and evaluation as well a good performance management all of which need to be grounded under strong institutional framework).

Kwavyo nadhani ni wakati muafaka kuzipa wizara mamlaka yake ya kufanya usimamizi wa sera ambazo wanazitunga wenyewe kisha wanazitupia taasisi zilizo chini yake kutekeleza sera husika. Endapo tukilihuisha hili ni dhahiri tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika mfumo makini wa utawala bora, kimsingi ni nadra sana kupata ufanisi katika mfumo umeojengwa kwenye dhana ya taasisi moja kuwa yenyewe ndio mshitaki na vile vile ndio hakimu (refarii ni wewe mwenyewe na timu yako ndio inacheza), sera umetunga mwenyewe na kusimamia unasimamia mwenyewe. Endapo hoja hii itapita basi wizara nyingi itabidi zipunguzwe ukubwa na kubakia na maofisa wachache sana kwa ajiri ya kufanya kazi za M&E pamoja na kuratibu uundwaji wa sera na sheria mbalimbali, nguvu kazi nyingine itakayobakia ipelekwe kwenye taasisi husika. Kwavyo kila wizara itakuwa na kazi kuu ya msingi ya kuzitathimini taasisi zake kwa kila juma, mwezi na kutoka mwaka mmoja hadi mwingine; tukifikia hapa tutakuwa tumepiga goli la kisigino.

Baada ya kukubaliana na muundo wa kiujumla wa kila wizara sasa linafuata suala la kuzipanga wizara katika sekta za kimkakati ili kutekeleza yale waliyowaahidi wananchi wakati wa kuomba ridhaa ya kuongoza, na zifuatazo ni sekta za kimkakati amabazo nadhani zitakuwa tija kwa taifa kuelekea uchumi wa kati:

  1. Uchumi na fedha
  2. Afya na ustawi wa jamii (Jinsia na watoto itaingizwa humu)
  3. Biashara, Utalii na Maliasili (wizara za viwanda na biashara pamoja na wizara ya utalii na maliasili ziunganishwa pamoja vile vile wizara ya uwezeshaji na uwekezaji itafutwa ambapo itabakia kama idara katika ofisi ya waziri mkuu kwa sababu ni masuala mtambuka ambapo shughuli za kiutendaji zitahamishiwa TIC pamoja na NEEC. Vile vile wizara ya masuala ya mazingira ifutwe na kuingizwa humu)
  4. Kilimo, ufugaji na uvuvi
  5. TAMISEMI
  6. Utumishi wa umma (wizara ya kazi na vijana ifutwe harafu dawati la kazi lihamie utumishi huku masuala ya michezo, habari na utamaduni yahamishiwe elimu)
  7. Maji, Nishati na madini (hapa kuna hoja nyingi kinzani wengi wakishauri maji na nishati viendelee kutenganishwa lakini ikumbukwe kama tukiwa na mfumo makini wa perfomance management, basi kurugenzi ya maji yatosha kabisa kufanya maboresho katika sekta husika hali kadharika nishati na madini; ati waziri si mtaalamu cha muhimu ni kuziweka vizuri portfolio husika ili kuleta tija)
  8. Utawala bora, uhusiano na uratibu ziunganishe (hii vile vile itahusika na masuala ya bunge na masuala ya ikulu)
  9. Muungano, Katiba na sheria
  10. Elimu, mawasiliano na teknolojia (masuala ya habari, michezo na utamaduni yanaingizwa humu)
  11. Nje na mahusiano ya Afrika mashariki
  12. Mambo ya ndani
  13. Ulinzi na jeshi la kujenga taifa
  14. Miundombinu na Uchukuzi

Kwa mchanganuo huo tutakuwa na mawaziri 14 na manaibu waziri 13 bimana wizara ya utawala bora, uhusiano na uratibu yenyewe itakuwa haina naibu waziri. Kwavyo jumla ya mawaziri pamoja na manaibu wao itakuwa ni 27 tu.

FALSAFA yangu ya uongozi wa nchi ni kuratibu shughuli za serikali mithili ya uendeshaji wa kampuni kubwa yenye kutengeneza faida hali ya kuwa ikidhibiti matumizi ya fedha kwa mantiki ya kubana matumizi.

Kwa muktadha huu napendekeza Mh. Raisi yeye ajikite kwenye wizara zifuatazo:

  1. Uchumi na fedha
  2. Utawala bora, uhusiano na uratibu
  3. Utumishi wa umma
  4. Nje na mahusiano ya Afrika mashariki/kikanda
  5. Mambo ya ndani
  6. Ulinzi na jeshi la kujenga taifa

Katika mchanganua huo zifuatazo zitakuwa zinaratibiwa na makamu wa raisi kama msaidi wa raisi.

  1. Muungano, Katiba na sheria
  2. Afya na ustawi wa jamii
  3. Biashara, Utalii na Maliasili

Waziri mkuu kama msaidi wa raisi atajikita katika wizara zifuatazo:

  1. TAMISEMI
  2. Kilimo, ufugaji na uvuvi
  3. Maji, Nishati na madini
  4. Elimu, mawasiliano na teknolojia
  5. Miundombinu na Uchukuzi

Huu ndio mtazamo wangu wa namna ya kupanga wizara tukielekea kwenye uchumi wa kati, haya yangu maoni, mawazo na mitazamo mingine inakaribishwa zaidi kwa nia ya kuboresha ama kukosoa.

Asante!

Wako,

Safari Fungo
Dar es Salaam, Tanzania
fungolee@gmail.com
+255 783 107 531

Moja ya msisitizo mkubwa wa wagombea wa urais wakati wa kampeni ulikuwa uboreshaji wa elimu hasa elimu ya msingi na sekondari.Kwa kuwa rais wa awamu ya tano Mheshimiwa Magufuli,ameshatoa maagizo kadhaa yanayohusu mabadiliko katika sekta ya elimu kama vile kufutwa kwa ada na michango kwa shule za msingi na zile za sekondari mpaka kidato cha nne,kudhibiti mahudhurio ya walimu kazini,kudhibiti utoro kazini,kuboresha ufundishaji,kudhibiti ufujaji wa fedha za elimu n.k,maagizo hayo yanahitaji usimamizi wa hali ya juu.Waziri atakayekabidhiwa wizara itakayosimamia shule za msingi na sekondari,anatakiwa awe mtu makini,mwenye maamuzi magumu,mwadilifu na mchapa kazi kwelikweli.

Baada ya kutafakari kwa kina, nimemfikilia mtu mmoja ambaye nafikiri anafaa kupewa wizara hii nyeti kuliko zote.

MAMAJOYCE NDALICHAKO,huyu mama anastahili kabisa kuteuliwa kuwa mbunge na kisha kupewa wizara hii ambayo kwa sasa ipo ICU,inapumulia mashine,inahitaji mtu wa shoka,kama washauri wa Magufuli watapitia hii clip basi wamfikishie mheshimiwa.Ndalichako anafaa kwa kuwa
  1. Anao uzoefu wa kuongoza taasisi nyeti,alikuwa katibu wa baraza la mitihani kwa miaka kadhaa
  2. Alilikuta baraza likiwa mahututi,akaliacha likiwa moja ya taasisi za mfano
  3. Alifukuza watendaji wote wazembe bila woga
  4. Ni miongoni mwa wasomi waliotukuka
  5. Ni mtu mwenye misimamo,alipoambiwa abadili matokeo ya O-level mwaka 2012 alikataa katakata
  6. Ni mbunifu,alionyesha ubunifu wa hali ya juu kupambana na tatizo sugu la mitihani (a) Alianzisha mfumo wa wasimamizi wote kutoka nje ya chuo (b) Alianza kuwashirikisha usalama wa taifa (C) Alibuni mfumu wa usahihishaji,'conveyer belt',ulioigwa na nchi zote barani Afrika (d) Alianzisha mfumo wa kubadilisha wasahihishaji (e) Akaanzisha matumizi ya picha katika vyeti na photoentry (f) Akaanzisha matumizi ya komputa katika usahihishaji
  7. Wizi wa mitihani ulikoma kabisa kipindi chake
  8. Malalamiko ya walimu waliohusika katika utunzi,usimamizi na usahihishaji wa mitihani yaliisha kabisa,morali wa ufanyaji kazi uliongezeka,baada ya Ndalichako kwenda subatical leave,malalamiko yameanza tena,hakika huyu mama ni kiongozi bora kabisa,mbunifu na mchapakazi hodari kabisa
  9. HUYU NDIYE ANAYEFAA KUONGOZA WIZARA YOYOTE ILE ITAKAYOSIMAMIA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
  10. Kwa bahati mbaya simuoni mtu mwingine yoyote yule anayeweza kupambana na uongozi mbovu katika ngazi za shule,wilaya,mikoa na taifa, anayeweza kudhibiti uvivu wa walimu na atakayekomesha ubadhilifu katika ngazi zote za elimu zaidi ya mama huyu wa shoka,Dr Joyce Ndalichako,Mkikutana na Rais Magufuli,mwambieni asihangaike,amchague Dr Ndalichako,atatimiza kwa vitendo kauli mbiu ya HAPA KAZI TU,haya niyasemayo ni hakika,thabiti na kweli kabisa
 
mwigulu kahangaika sana yule jamaa,,aliacha jimbo lake na kuzunguka nchi nzima
 
bavicha mnahangaika sana na utabili vp mbowe waziri mkuu wa low ass
 
Apewe Muhongo ndo chemistry itanoga zaidi kama siyo uPM arudi kwenye Nishati na Madini.
 
Back
Top Bottom