Hongera Lukuvi, kazi yako tumeiona

Salam!

Naweza kusema Mh. William Lukuvi ni miongoni mwa viongozi wachache walioweza kusifiwa kwa utendaji wao angali wakiwa hai

Jana baada orodha ya mawaziri waliochwa kwenye baraza la mawaziri kutoka nimeona kwenye mitandao ya kijamii na huku mtaani watu wengi wakiumia sana kwanini mh Rais kamuacha lukuvi wakati huyu kiongozi alikuwa ni mchapa kazi mahiri.

Kinachonishangaza kwanini watu wengi wameuzunishwa na kuondolewa kwake. Hakika hapa kuna kitu cha kujifunza kutoka kwa kiongozi huyo

Kwenu viongozi tunapopewa nafasi za kutumikia taifa hili tujitahid kuzitendea haki na tusiwe waimba mapambio tuige mfano wa Mh Lukuvi.

Kila la kheri William Lukuvi katika majukumu yako.
Lukuvi kafanya kazi mzuri ila kosa lake ni kujiunga na hao jamaa wa 2025.
 
Maza kabugi sana hapa!

Lukuvi alikuwa tayari ameielewa Vizuri hiyo wizara.
 
Lukuvi kafanya kazi mzuri ila kosa lake ni kujiunga na hao jamaa wa 2025.
Kazi ipi?? ya kufuta hati za mashamba ya watu na kujimilikisha viwanja kila mahali na kuwa na kampuni za kutathmini ardhi hivi kweli mambo kama haya yanaogopwa kusemwa Tanzania??
 
Wizara ilikuwa mali yake na maofisa wake wachache
Kama ni kwa maslahi ya wengi poa tu.

Hao maofisa wa Ardhi wenyewe ndiyo chanzo cha migogoro ya Ardhi.

Nimesikia wanasherekea kuondolewa kwa Lukuvi.
 
Kama ni kwa maslahi ya wengi poa tu.

Hao maofisa wa Ardhi wenyewe ndiyo chanzo cha migogoro ya Ardhi.

Nimesikia wanasherekea kuondolewa kwa Lukuvi.
Hata yeye mwenyewe alikuwa chanzo cha migogoro alafu anakusuma kwa maofisa wake kamishna wake mkuu ndio balaa yaani anapora mchana kweupe
 
Waziri mpya wa ardhi asipoangalia atashindwa kuthibiti matapeli na majambazi wa Lukuvi kwanza aanze na kamishna afukuze kabisa alafu aende kwenye kila wilaya aondoe matapeli sugu wa ardhi wanajiita maofisa ardhi kama anataka tumsadie atuambie tuweke majina hapa bila kuonea mtu watanzania tuwe wazi tuache unafiki Mimi nina list ya majambazi wa ardhi na jinsi wanavyofanya kuiba ardhi na kusingizia watu uongo na kesi za ajabu kwa hiyo tusipoteze mda tufunguke we have nothing to lose we have lost everything the only thing left is justice and karma
 
Takukuru walikuwa hawasubutu kumgusa Lukuvi na kamishna wake kwani walikuwa wanawaogopa nasikia walikuwa wanaahidiwa viwanja na kwa hiyo Lukuvi alitashika ardhi kama mali yake na ardhi ni kitovu cha taifa ndio sababu alikuwa anajiona mungu mtu Viwanja vingi viko mifukoni mwao havilipiwi kodi hayo ni mapato ya serikali.Kama kweli Serikali inataka kukomesha utapeli wa Lukuvi na maofisa wake wanitafute niwape ukweli nazungumaza kwa kujiamini kwani ukweli tushaupeleka Takukuru wakatugeukia sisi tuliopeleka ukweli kwa hiyo Tanzania sio nchi inauotaka ukweli na haki hiki kieleweke kwa kila mtu mtaka haki. Mungu mlinde Raisi Samia kwa kutokumuogopa huyu Mtu mdhulumati mkuu na muongo mkuu.
 
Tuache chuki binafsi zidi ya lukuvi
Ukiona kiongozi kutoka ccm analiliwa na watu wa vyama vyote basi jua huyo alikuwa muadilifu kwenye majukumu yake
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom