Hongera Dkt. Anna Makakala, Diaspora tumeona mabadiliko upokeaji maombi ya pasipoti ila Sasa maafisa wachache wamekalia maombi bila kutoa pasipoti

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Mara mwisho nikiwahi kuleta Uzi hapa kuishauri Uhamiaji iache kuwarudisha waombaji wa pasipoti bila kuwapokea Jambo lililopelekea vishoka nje ya ofisi zao kushirikiana na maafisa kushawishi ndipo maombi yapokelewe. Vijana wengi na watu wengi tulionao kwenye group la WhatsApp na tunaojadili nao kuhusu umuhimu wa Watanzania kwenda kufanya kazi nje wanasema Kwa Sasa watu wao wanapokelewa mara tu wanapowasilisha maombi yao.

Lililkuwepo tatizo la mabinti wanaokwenda kufanya kazi nje wengi wakitokea Dodoma ,Singida na Iringa. Hawa Bado wanasumbuliwa Sana. Kwa mfano Nina ndugu yangu yupo Oman alimtafuta dada wa kazi akamwombea pasipoti na ikatoka lakini zilipobadilishwa akalazimika arudi nchini kuomba upya pasipoti nyingine. Pamoja na kuwa na kibali Cha kufanya kazi nje lakini amezuiliwa kwa maelezo kwamba serikali imekataza mabinti kwenda kufanya kazi nje; anadai amefuatiliwa Kwa viongozi wengi lakini majibu ni kwamba Uahamiaji wamefungwa mikono kutoa pasipoti Kwa mabinti na wanawake wanaoeleza kuwa wanakwenda kufanya kazi nje. Nikajiuliza haya maelekezo kwanini yamekaa Kwa ubaguzi? Katiba inaruhusu free movement kwanini haya maelekezo yanayokinzana na katiba yanaendelea kuwepo? Dr. Nikuombe ufuatilie kama suala hili lina ukweli basi tangazieni umma wajue kwamba ni marufuku kwenda kufanya kazi nje ya Nchi ukiwa na miaka 18- 45, tangazeni watu wasiangaike kulipia maombi ya pasipoti.

Lakini Kwa ushauri wangu Ili kuepusha rushwa ambayo ndiyo inayotumika Sasa kuwawezesha kupata hizo pasipoti nadhani Dr. unaweza kuwaelekeza wananchi kwamba hakuna katazo la aina hii Ili akitokea kishoka au afisa asiye mwadilifu basi wananchi waweze kuripoti kwako lakina taasisi Yako ikiendelea kukaa Kimya maana yake unaruhusu usumbufu huu wanaoapata Watanzania.

Lakini tatizo kubwa lililoibuliwa na maafisa Uhamiaji wachache ni kwamba wanapokea maombi na kutafungia ofisini bila kuyashughulikia. Kibaya zaidi maombi yanapokwama vishoka wamekuwa wakiwapigia wakishirikia na waombaji kushawishi waajiri walioko nje watoe kitu kidogo ndipo wapewe pasipoti. Huu urasimu ulioanzishwa na maafisa na kwakuzingatia Bado vishoka wapo umezalisha tatizo kubwa zaidi. Afisa anakaa na maombi mwezi bila hata system kumpa update Mteja kwanini wateja wasiangukie Kwa matapeli? Au kwanini wateja wasiwategemee vishoka ambao wamezagaa kwenye ofisi za umma wakigombania waombaji wa pasipoti? Nadhani kama mama anavyofungua Nchi watendaji wako wanapaswa pia kufungua mipaka na kurahisisha huduma.

Badilisheni mfumo wenu wa pasipoti uwe kama mifumo Mingine ambayo ukiomba huduma basi unaweza kuomba pia kupata updates Kwa kukatwa kiasi flani Cha fedha. Mfano benki ukitaka salio unalipa shs mia, kwenye mfumo wa pasipoti wekeni kipengele Cha MTU kufuatilia ombi lake akiwa ofisini kwake au nyumbani hii itapunguza watu kuja kwenye ofisi zenu nakukutana na vishoka au watendaji wasio waaminifu.

Endapo ombi linamapungifu mnshindwa nini kumtumia Mteja ujumbe ambao ataulipia kumweleza rekebisha A,B, C.........?

Mwisho nikupongeze Dr. Kwamba Kila jambo positive linaloletwa hapa au kuwasilishwa na diaspora na wananchi umekuwa ukichukua hatua. Pokea pongezi za wananchi huko nje kwamba umewaondolea kabisa usumbufu wa kusafiri kuja Tanzania Kwa ajili ya pasipoti. Umefanya mabadiliko makubwa, lakini pia nikujulishe kwamba huduma za Balozi zetu nyingi Ulaya na mashariki ya mbali zimeimarika kero zimepungua naamini Mhe. Mulamula mdogo wangu Kwa kushirikia na na Wewe Kuna mabadiliko ya watendaji mtakuwa mmefanya; kuna kind of professionalism tunaiona ubalozini huko tofauti na awali ambapo ukienda ubalozini wanakuona kama mzamiaji usiye na mbele Wala nyuma.

Mama piga amsha amsha kwenye madroo ya watendaji wako utakuta wamezuia maombi ya watu kibao na naamini huu ni mgomo baridi baada ya mbinu Yao ya kurudisha watu kubainika. Miezi miwili MTU anasubiri pasipoti wakati wapo wadosi watoto wao wanapata pasipoti Kwa siku Moja. Wanawatuhumu watoto wa watu kuwa wanakwenda kuwa ma house boy na girls wakati maafisa hao hao Wana mabinti makwao wamewaajiri Kwa shughuli hizo hizo. Badilikeni Ninyi viumbe; wahaya tusingetoka Bukoba tukaamua kuambatana na wamisionary those year Leo tusingekuwa tumetapakaa Dunia, wachaga ze same; waacheni wanyampaa na wanyalu wakaione Dunia. Mnajua mijengo mingi ya maana singida na Dodoma imejengwa na ma house girl? Acheni umwinyi waacheni vijana wakatafute riziki; baadhi yenu may be hata huko nje amjawahi kufika mnapadis tu lakini mkipewqa fursna naamini mtakimbilia airport
 
Ni kweli nje kuna fursa nyingi kwa Watanzania lakini kinachokwamisha ni ukiritimba uliopo kwenye mamlaka za maamuzi. Watu wawe fair, walioko nje watambuliwe. Balozi zote zishirikiane kuwafanyia connection Watanzania ziwasaidie mahali wanapokwama na siyo kuwachukulia wote wenye matatizo kama waalifu.
 
Back
Top Bottom