Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 876
- 4,101
Nimeona Makonda akisema madereva wapatiwe pasipoti kwa gharama za Mhe. Rais nikashtuka sana kwamba nchi ina viongoz wasiojua tatizo la watu wake
Nchi ya Zambia ukiingia kama dereva kwa kutumia pasipoti kubwa ya Tanzania unalipishwa zaidi ya milioni moja kama gharama za vibali. Hii kero hata Mh. Rais aliikuta Zambia.
Lengo la Zambia nikuwakwamisha madereva wa Tanzania wasiingie Zambia ili RAIA wa Zambia wawe wanafanya kazi za udereva kuchukua mizigo Tanzania.
Madereva wetu kwa kujua tatizo lilipo wamekuwa wakitumia pasipoti za muda mfupi ambazo ukiingia Zambia hata mara kumi hakuna gharama za ziada.
Kwa mtu anayefanya biashara na Zambia hasa usafirishaji wa mizigo atakubaliana na mimi kwamba anachosema Makonda sicho tunacholalamikia; alipaswa aeleze ni nini Wizara ya Mambo ya nje imefanya kuondokana na changamoto hii.
Kama mnakumbuka hivi karibuni Mhe. Rais alitangaza wazambia waingie Tanzania bure wakae siku 180. Lakini hakuna Mtanzania anaweza kuishi Zambia zaidi ya siku 90 bila kukamatwa.
Wanasiasa wanapokwenda kwenye majukwaa wasipende kubeba hoja nyepesi wakaacha hoja za msingi. Kwanini madereva wasiwe wanapanga foleni kutafuta pasipoti kwenda Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Malawi? Ni kwa sababu hizo nchi hakuna masharti magumu kwa waajiri na madereva kama Zambia.
Tukitaka kuwatetea madereva tuzungumze na serikali ya Zambia waheshimu makubaliano ya kiplomasia. Tuliona kama wao kuja Tanzania ni bora ila sisi kwenda Kwao ni kero.
Politicians fanyeni tafiti, shirikini kwenye busines mjifunze tunavyoteseka. Leo unakwenda kumpa kazi Mhe. Rais kulipa gharama za pasipoti sijui atakuwa analipishaje hayo malipo maana kila ukiomba pasipoti lazima utoe control number.......na kibaya zaidi hizi pasipoti za Tunduma ukiondoka ukarudi imeisha.