#COVID19 Hoja za baadhi ya Watanzania kuhusu kukataa chanjo bado ni dhaifu sana

hii ngoma kila mtu acheze kwa style yake.......watanzania ni wajuaji sana.........wangeambiwa hii chanjo inamaliza UKIMWI...... hakika ungekuta vituo vimefurika.......kama unajielewa tafakari kwa makini...........na uelewe.....DUNIA INAENDESHWA "wandu wasungu bana" wangeamua kutuua wangeshatumaliza tokea enzi........mdoa mada hawatakuelewa..........ila usichoke......asante.
 
Una hoja nzuri ila huku mwisho naona umetindinganya mambo. Eti kutokujua kwangu hakumaanishi hiyo chanjo haifai namna gani wewe, sasa hizo ngonjera za kuhamasisha watu wakachanje kwa kuwaambia ni salama zinatoka wapi kama sio muhimu kujua uhatari wake.

Kitu kingine kinachoonesha baadhi yenu watu wa chanjo (ukiwemo wewe) ni weupe kichwani ni kuamini kua mtu asietaka chanjo ni mjinga😂😂.

Yani dunia hii unategemea watu wawe upande wa unachokiamini au upande wa wengi kwa 100%. Mkuu em acheni tabia za kuita wenzenu wenzenu wajinga ilhali hata nyie hamna hoja zaidi ya blah blah tena sio za kidaktari ni zile za wanasiasa wa tz kina ndugai 😂.
Wanaokubali chanjo wote sio kwasababu ya uhalali na usahihi wa chanjo bali kwa kupingana na mwenda zake(hawakubali lakn ndo ukweli). Wanaokataa ni vile tu mindset zao ni kuwa mzungu sio mtu wakutoa vitu kiholela nimjanja sana anamingo yake nyuma ya chanjo.
 
Wasiotaka kuchanjwa sio sahihi kutumia hoja tata kuwaogopesha wenzao ambao wametumia hiari yao kwenda kuchanjwa.
kifupi hi hivi! Chanjo ni HIARI, wanaotaka kuchanja wakachanje na vilevile ni sahihi kuwahimiza wengine wakachanje.
Wasiotaka kuchanja wasichanje lakini SI sahihi kuwahimiza wengine wasichanje.
 
Gwajima si aliwaaminisha waumini wake kua corona imetokana na waves za 5G technology

Kama alikua muongo kwa hoja hiyo kwanini waumini wasimuone muongo kwa hoja hii ya chanjo?

Afu anatuondolea focus ana tusahaulisha kimakusudi tusahau ile video yake
😆😆😆
 
Mkuu umefafanua vizuri sana.Matz ni Makima yaliyochangamka.

Wewe uliona wapi mtu mwenye akili timamu akifurahia Rais kuvunja katiba na sheria?!Ukija hapa tz utasikia haya Makima yakisema kuwa Samia anaupiga mwingi.Ukisia hivyo jua yanafurahia Rais kukanyaga kanyaga katiba na sheria!
 
Kwa nini watie hofu uhuru wa watu wengine katika jambo ambo serikali imesema ni salama ?
Hapo ndo tatizo lilipo anza baada ya serikali kuonyesha undumilakuwili wa hali ya juu sana.
Ukiangalia kwa mama wa afya yule na baadhi ya watu wamegeuka sana maneno yao ya awali
Hivyo mvurugano

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Gwajima si aliwaaminisha waumini wake kua corona imetokana na waves za 5G technology

Kama alikua muongo kwa hoja hiyo kwanini waumini wasimuone muongo kwa hoja hii ya chanjo?

Afu anatuondolea focus ana tusahaulisha kimakusudi tusahau ile video yake
Hahaha wale wanaendeshwa na vivuli vya dini mwache rashid aendelee kukusanya sadaka

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
[B[Wamenkataa WACHANJAJI kuwa sina Vigezo! Sipo kwenye CATEGORIES zao! Mwenye connection anipe jamani!
 
Watanzania hawaishiwi hoja kwa kweli.

ETI Katika hoja wanazotumia wanasema eti chanjo gani ambayo serikali imejitoa kabisa kwamba litakalokupata wao hawawajibiki kwa lolote ?

Watanzania wamesahau kwamba hata ukienda hospitali una haki ya kukataa kutibiwa,una haki ya kukataa sawa,una haki ya kumkataa daktari usiyemtaka asikutibu.

Endapo ukikubali kutibiwa kwa ridhaa yako na katika tiba hiyo ukapata madhara basi hakuna daktari atakayewajibika eti ahukumiwe kwa jambo hilo.

Hata ukienda kufanya upasuaji lazima ukubali kusaini,usaini ukaenda ukafa kwenye upasuaji ujue hakuna utakayemlaumu kwa sababu ulikubali mwemyewe.

Hivyo sio kwenye korona tu hata kwenye tiba zingine wanaohusika na jambo hilo wanajivua endapo ukikubali kufanyiwa jambo hilo litakalo kupata lakwako wewe.

Hivyo serikali ipo sahihi kujitoa lwenye lawama kwa sababu mtu atachoma chanjo akiumwa kichwa tu atataka aiwajibishe serikali kwamba chanjo inamdhuru,katika hili serikali imefanya vyema.

ETI Katika hoja wanazotumia wanasema eti chanjo gani ukishachanja unaambiwa uendelee kuchukua tahadhari ?

Watanzania hakuna chanjo utakayochukua alafu ukaambiwa ukae katika mazingira hatarishi ati kwa kuwa umepata chanjo,hakuna chanjo hiyo.

Angalia tu ukidungwa sindano ya kujikinga na tetenasi haina maana kwamba ujiachie tu wewe ujikate ovyo na kujiachia kwenye mazingira hatarishi.

Ukidungwa chanjo ya yellow fever haina maana eti ndio utaambiwa ukae tu kwenye mbu na mazingira hatarishi,lazima iwe ni muhimu kujiepusha na mazingira hayo hatarishi.

Hivyo hata chanjo ya korona ukidungwa haina maana ujiachie tu,lazima uendelee kujikinga.

Maana ya chanjo sio kutafuta matatizo yalipo,maana ya chanjo ni kukukinga endapo kwa bahati mbaya umepata ugonjwa,sasa wewe utafute kwa makusudi.

Ukicheza karate unatakiwa uepuke ugomvi,haina maana kwamba unajua kupigana ndo uchokoze watu.

ETI Baadhi husema sijui ukichanjwa utapata madhara kadha wa kadhaa,ni kweli unaweza kupata madhara kdha wa kadha lakini swali la msingi ni je chanjo hiii pekee tu ya corona ?

Jawabu ni kuwa chanjo zote zina madhara fulani yanaweza kutokea kwa mtu.

Mfano.
Kuna chanjo watoto wachanga wakichomwa wanapata homa sana lakini baadae wanatulia maisha yanaendelea chanjo hizi hazipigiwi kelele.

Unaweza kuchoma chanjo ukapata aleji kinga za mwili zikaanza kushambulia seli mwenzake za mwili ukaanza kupata machovu na matatizo mengine ambayo yanaweza kupotea baada ya muda fulani.

Zipo kinga au chanjo mfano kinga ya homa ya manjano tafuta side effects zake utaona miongoni mwa matatizo ambayo unaweza kupitia ni kama vilee.

Maumivu ya joints,maumivu ya misuli,kupata homa,mapele,kichwa kuuma n.k

Kwa hiyo kama chanjo ya corona itakuwa inaambatana na matatizo basi tukubaliane hakuna chanjo iliyosalimika.

Lakini pia naomba kuwauliza wanaosema hii chanjo baada ya muda ina madhara.

Je wamejuaje kama ina madhara wakati hapo hapo wanasema haijafanyiwa utafiti wa kutosha kuhusu usalama na madhara yake ?

Na je hayo madhara yataonekana baada ya muda gani ukishachoma chanjo ?

Swali la mwisho ambalo naomba niliulize ni kwamba tokea tuanze kudungwa hizi chanjo utoto wetu ambazo tisema tunajaribiwa mpaka hivi leo hii tumepata madhara gani kwa watu wote ambayo tutasema kisayansi yametokana na chanjo hizo za utotoni ?

NB : siko hapa kutetea chanjo,bali niko hapa kuvunja hoja dhaifu zinazotumika na baadhi ya watu kuwatisha wengine.

Nakubaliana na mambo ambayo kisayansi yana hoja zenye nguvu zinazoingia akilini na sio kuokota kila hoja tu na kuisema ili tuendee kulaumu.
Mimi sijakataa kuchanjwa nataka sana! Ila naogopa tu ile sindano halaf sina uhakika kama hiyo chanjo ina uhakika wa kukinga hayo maradhi au tunachoma tu halaf baada ya muda inaisha nguvu tatu naona hata nikichanjwa bado natakiwa kuchukua tahadhari vilevile sasa yanini?
 
Kuthibitishwa kwake hakufanyo watu wasiwe na mashaka mkuu.

Halafu unajua nyie watu wa chanjo mmekaa kukejeli na sio kutoa hizo hoja zenu.
Bado nafatilia kupitia vipindi mbali mbali wanaelekeza vizuri na kwa weledi ila humu naona wote sawa tu , hakuna hoja mnazodai mnazo zaidi ya mifananisho.
Point ya kusema watu wasiwe na mashaka bado haibadilishi uhalisia, watu wamekua na mashaka kwenye vitu vingi sana ambavyo sayansi imekua ikifanya. Hata ishu ya moon landing watu kibao wana mashaka kua sio kweli

Sayansi haipo kwa ajili ya kuwafurahisha wadau, kusema kitu fulani ni uongo eti kwasababu wewe haikikuridhishi sio sawa.
 
Sikupingi kwa hilo, kumbe tuko pamoja kua sio ajabu watu kua na mashaka na hiyo chanjo. Kwahivyo sioni haja ya kushambulia wasioiamini kama alivyofanya mleta uzi.

Na nikusahihishe hapo, hakuna aliesema ni uongo, kua na mashaka na kitu haimaanishi ni cha uongo mkuu, kinaweza kua kweli na mashaka yangu yakatoweka kabisa ama kikawa uongo.
 
Wanaokubali chanjo wote sio kwasababu ya uhalali na usahihi wa chanjo bali kwa kupingana na mwenda zake(hawakubali lakn ndo ukweli). Wanaokataa ni vile tu mindset zao ni kuwa mzungu sio mtu wakutoa vitu kiholela nimjanja sana anamingo yake nyuma ya chanjo.
Mkuu kwenye hiyo ya kwanza uko sawa kabisa, wengi wao ndio wako hivyo.

Kwa upande wangu siipingi hiyo chanjo na mi nilikua napenda walete chanjo ila tu jinsi ilivoletwa ndio imenitia mashaka kidogo na najaribu kufatilia zaidi. Lakini humu ndugu zetu hawa ukiwaambia mashaka yako wanakushukia jumla jumla kama mwewe na kifaranga.
Hizi mindset za kua watu fulani wako sahihiwakati wote zaidi ya mwingine tuzipunguze jama
 
Sikupingi kwa hilo, kumbe tuko pamoja kua sio ajabu watu kua na mashaka na hiyo chanjo. Kwahivyo sioni haja ya kushambulia wasioiamini kama alivyofanya mleta uzi.

Na nikusahihishe hapo, hakuna aliesema ni uongo, kua na mashaka na kitu haimaanishi ni cha uongo mkuu, kinaweza kua kweli na mashaka yangu yakatoweka kabisa ama kikawa uongo.
Niambie kitu gani ambacho watu wote 100% hawana mashaka nacho

Unakua na mashaka kulingana na observation uliyofanya juu ya hicho kitu kua majibu yake haya relate na namna ambavyo wao wanavyosema au ni yale mashaka yasiyo hitaji uchunguzi bali mhemko?
 
Sawa...
Mbona kuna watu wanaenda pale kairuki wanaambiwa,chanjo ni kwa ajili ya wale wenye miaka 50,wazee na wagonjwa
Nyie wengine subirieni

Ova
 
Niambie kitu gani ambacho watu wote 100% hawana mashaka nacho
Mpaka hapa sijaelewa tunachobishana hasa ni nini ilhali unajua kua ni kawaida kwa kitu kutoaminiwa 100%.
Unakua na mashaka kulingana na observation uliyofanya juu ya hicho kitu kua majibu yake haya relate na namna ambavyo wao wanavyosema au ni yale mashaka yasiyo hitaji uchunguzi bali mhemko?
Wengi walio na mashaka na chanjo sio ya kua wameingia lab kufanya testing na izo ishu ka izo, ni kupembua taarifa hii na ile kama ulivyofanya wewe na kuangukia upande huo wao nao kulingana na taarifa wanzaopata/pewa wameangukia upande mwingine.
Yote kwa yote ni hiari ni ujinga kumshambulia mtu kwa dhihaka ikiwa haamini kama wewe.

Ushauri.
Tuelimishane sio kupayukiana kutafuta mshindi nani.
 
Mkuu kwenye hiyo ya kwanza uko sawa kabisa, wengi wao ndio wako hivyo.

Kwa upande wangu siipingi hiyo chanjo na mi nilikua napenda walete chanjo ila tu jinsi ilivoletwa ndio imenitia mashaka kidogo na najaribu kufatilia zaidi. Lakini humu ndugu zetu hawa ukiwaambia mashaka yako wanakushukia jumla jumla kama mwewe na kifaranga.
Hizi mindset za kua watu fulani wako sahihiwakati wote zaidi ya mwingine tuzipunguze jama
For me, side effect ya chanjo ni kubwa kuliko kuishi bila chanjo.
Tunahitaji kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya corona lkn sio lazima tuwe universal, tuwe unique coz hata hivyo ukichanja bado unauwezekano wa kupata tena usipojikinga.
Mkataa kwao ni mtumwa, lazima tukubali kuheshimu vyakwetu ili tusitumikishwe na vyawenzetu. Kwani tukijifukiza na hali ikawa shwari kuna mtu atakupiga risas kisa umejifukiza?
Ikiwa ni kitaalam bas wataslam wa masuala ya chanjo wakwetu wakae chini sio kutathimini uhali wa hio chanjo ya johnson bali wachukue ujuz hapo watengeneze yakwetu then waitathmini uhalali na usahihi wake kwa watumiaji.
 
Sikupingi kwa hilo, kumbe tuko pamoja kua sio ajabu watu kua na mashaka na hiyo chanjo. Kwahivyo sioni haja ya kushambulia wasioiamini kama alivyofanya mleta uzi.

Na nikusahihishe hapo, hakuna aliesema ni uongo, kua na mashaka na kitu haimaanishi ni cha uongo mkuu, kinaweza kua kweli na mashaka yangu yakatoweka kabisa ama kikawa uongo.
Sijashambulia mkuu,kushambulia ni kufanya kitu bila hoja.

Mimi nimesema tu kwamba hoja zao dhaifu,na nimeonesha udhaifu wa hoja hizo kwa maoni yangu.
 
Back
Top Bottom