berty
Senior Member
- Jun 30, 2021
- 135
- 136
oja za wezio unaita dhaifu ila atuchanjiWatanzania hawaishiwi hoja kwa kweli.
ETI Katika hoja wanazotumia wanasema eti chanjo gani ambayo serikali imejitoa kabisa kwamba litakalokupata wao hawawajibiki kwa lolote ?
Watanzania wamesahau kwamba hata ukienda hospitali una haki ya kukataa kutibiwa,una haki ya kukataa sawa,una haki ya kumkataa daktari usiyemtaka asikutibu.
Endapo ukikubali kutibiwa kwa ridhaa yako na katika tiba hiyo ukapata madhara basi hakuna daktari atakayewajibika eti ahukumiwe kwa jambo hilo.
Hata ukienda kufanya upasuaji lazima ukubali kusaini,usaini ukaenda ukafa kwenye upasuaji ujue hakuna utakayemlaumu kwa sababu ulikubali mwemyewe.
Hivyo sio kwenye korona tu hata kwenye tiba zingine wanaohusika na jambo hilo wanajivua endapo ukikubali kufanyiwa jambo hilo litakalo kupata lakwako wewe.
Hivyo serikali ipo sahihi kujitoa lwenye lawama kwa sababu mtu atachoma chanjo akiumwa kichwa tu atataka aiwajibishe serikali kwamba chanjo inamdhuru,katika hili serikali imefanya vyema.
ETI Katika hoja wanazotumia wanasema eti chanjo gani ukishachanja unaambiwa uendelee kuchukua tahadhari ?
Watanzania hakuna chanjo utakayochukua alafu ukaambiwa ukae katika mazingira hatarishi ati kwa kuwa umepata chanjo,hakuna chanjo hiyo.
Angalia tu ukidungwa sindano ya kujikinga na tetenasi haina maana kwamba ujiachie tu wewe ujikate ovyo na kujiachia kwenye mazingira hatarishi.
Ukidungwa chanjo ya yellow fever haina maana eti ndio utaambiwa ukae tu kwenye mbu na mazingira hatarishi,lazima iwe ni muhimu kujiepusha na mazingira hayo hatarishi.
Hivyo hata chanjo ya korona ukidungwa haina maana ujiachie tu,lazima uendelee kujikinga.
Maana ya chanjo sio kutafuta matatizo yalipo,maana ya chanjo ni kukukinga endapo kwa bahati mbaya umepata ugonjwa,sasa wewe utafute kwa makusudi.
Ukicheza karate unatakiwa uepuke ugomvi,haina maana kwamba unajua kupigana ndo uchokoze watu.
ETI Baadhi husema sijui ukichanjwa utapata madhara kadha wa kadhaa,ni kweli unaweza kupata madhara kdha wa kadha lakini swali la msingi ni je chanjo hiii pekee tu ya corona ?
Jawabu ni kuwa chanjo zote zina madhara fulani yanaweza kutokea kwa mtu.
Mfano.
Kuna chanjo watoto wachanga wakichomwa wanapata homa sana lakini baadae wanatulia maisha yanaendelea chanjo hizi hazipigiwi kelele.
Unaweza kuchoma chanjo ukapata aleji kinga za mwili zikaanza kushambulia seli mwenzake za mwili ukaanza kupata machovu na matatizo mengine ambayo yanaweza kupotea baada ya muda fulani.
Zipo kinga au chanjo mfano kinga ya homa ya manjano tafuta side effects zake utaona miongoni mwa matatizo ambayo unaweza kupitia ni kama vilee.
Maumivu ya joints,maumivu ya misuli,kupata homa,mapele,kichwa kuuma n.k
Kwa hiyo kama chanjo ya corona itakuwa inaambatana na matatizo basi tukubaliane hakuna chanjo iliyosalimika.
Lakini pia naomba kuwauliza wanaosema hii chanjo baada ya muda ina madhara.
Je wamejuaje kama ina madhara wakati hapo hapo wanasema haijafanyiwa utafiti wa kutosha kuhusu usalama na madhara yake ?
Na je hayo madhara yataonekana baada ya muda gani ukishachoma chanjo ?
Swali la mwisho ambalo naomba niliulize ni kwamba tokea tuanze kudungwa hizi chanjo utoto wetu ambazo tisema tunajaribiwa mpaka hivi leo hii tumepata madhara gani kwa watu wote ambayo tutasema kisayansi yametokana na chanjo hizo za utotoni ?
NB : siko hapa kutetea chanjo,bali niko hapa kuvunja hoja dhaifu zinazotumika na baadhi ya watu kuwatisha wengine.
Nakubaliana na mambo ambayo kisayansi yana hoja zenye nguvu zinazoingia akilini na sio kuokota kila hoja tu na kuisema ili tuendee kulaumu.