Serikali yakiri uzembe kwenye utoaji Chanjo za Magonjwa mengine baada ya kutokea UVIKO-19

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Wizara ya Afya imebaini kuwepo uzembe katika utoaji wa Chanjo za Magonjwa kutokana na Serikali kuwekeza nguvu kubwa katika Chanjo ya #UVIKO19 na kusahau Chanjo za magonjwa mengine.

Waziri wa Afya #UmmyMwalimu, Amesema hali hiyo imeleta madhara makubwa kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa #Surua na kusababisha vifo vya Watoto 13 wilayani Mlele hadi kufikia Februari 23, 2023.

Amesema “Katika kipindi cha miaka 3, tumesuasua katika kutoa chanjo dhidi ya Surua katika nchi hii, tumebaini kuna Watoto zaidi ya 400,000 Nchini hawajapata kabisa Chanjo ya dozi ya Surua,”.

==============

WIZARA ya Afya imekiri kuwepo uzembe katika utoaji wa chanjo za magonjwa mengine ikiwemo surua kutokana na ukweli kuwa nguvu nyingi zilielekezwa katika chanjo ya UVIKO-19 na kusahau chanjo za magonjwa mengine.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo leo Februari 24,2023 kwa nyakati tofauti, wakati akizungumza na wananchi katika mji mdogo wa Usevya na Kata ya Majimoto Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi katika mkutano wa hadhara alipofika kuzindua chanjo na kutoa salamu za pole.

Amesema hali hiyo imeleta madhara kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa surua nchini, na kusababisha vifo vya watoto 13 wilayani Mlele hadi kufikia jana Februari 23, 2023.

“Katika kipindi cha miaka mitatu tumesuasua katika kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa surua katika nchi hii, tumebaini kwamba kuna watoto zaidi ya 400,000 nchini Tanzania hawajapata kabisa chanjo ya dozi ya surua,” amesema.

Amesema hadi sasa ugonjwa wa surua umebainika katika Wilaya 19 za Tanzania bara ambazo ni Nsimbo, Tanganyika, Mpanda, Chunya, Bagamoyo, Kisarawe, Sikonge, Nzega, Tabora Manispaa, Kalambo, Sumbawanga, Sumbawanga Manispaa, Malinyi, Ulanga, Muleba, Korogwe, Mtwara Manispaa na Uvinza ambapo kati ya Wilaya hizo wilaya iliyoathirika zaidi ni Mlele Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi.

Amesema katika halmashauri hiyo kati ya wagonjwa 100 waliopata surua, wagonjwa 45 wametoka katika Kata ya Majimoto.

Katika kuhakikisha watoto wote nchini wanapata chanjo ya ugonjwa huo, Waziri Ummy amesema serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuhakikisha chanjo zinapatikana za kutosha, kutoa kampeni nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano anafikiwa na amewaagiza wakuu wa mikoa nchini kuwatafuta watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano, ambao hawajapata chanjo ya surua kuhakikisha wanapata chanjo.

Amesema kwa mujibu wa sheria ya afya ya jamii endapo mzazi au mlezi atabainika kutompeleka mtoto kupata chanjo anaweza kutozwa faini ya shilingi 100,000 au kifungo cha miezi mitatu gerezani au vyote kwa pamoja.

Katika hatua nyingine, Waziri Ummy ameitaja mikoa 20 ya Tanzania Bara ambayo watoto wengi bado hawajakamilisha dozi ya pili ya chanjo ya ugonjwa wa surua ni Katavi, Tabora, Dar Es Salaam, Arusha, Geita, Rukwa, Shinyanga, Manyara, Tanga, Lindi, Songwe, Mtwara, Iringa, Singida, Ruvuma, Dodoma, Kigoma, Morogoro na Mbeya na kuwataka viongozi kusimamia ipasavyo jambo hilo.

HABARI LEO
 
Waliwekeza nguvu kwenye gonjwa lisilo na maana yoyote wakaacha magonjwa ya msingi ambayo yana madhara makubwa iwapo mtu asipopata chanjo.

Covid uchanje usichanje unapata covid na kama ni kufa utakufa na chanjo yako mwilini, so chanjo haina maana yoyote. Zaidi wamewaongezea matatizo mengi na makubwa ya muda mrefu waliochanjwa.
 
Wizara ya Afya imebaini kuwepo uzembe katika utoaji wa Chanjo za Magonjwa kutokana na Serikali kuwekeza nguvu kubwa katika Chanjo ya #UVIKO19 na kusahau Chanjo za magonjwa mengine.

Waziri wa Afya #UmmyMwalimu, Amesema hali hiyo imeleta madhara makubwa kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa #Surua na kusababisha vifo vya Watoto 13 wilayani Mlele hadi kufikia Februari 23, 2023.

Amesema “Katika kipindi cha miaka 3, tumesuasua katika kutoa chanjo dhidi ya Surua katika nchi hii, tumebaini kuna Watoto zaidi ya 400,000 Nchini hawajapata kabisa Chanjo ya dozi ya Surua,”.

==============

WIZARA ya Afya imekiri kuwepo uzembe katika utoaji wa chanjo za magonjwa mengine ikiwemo surua kutokana na ukweli kuwa nguvu nyingi zilielekezwa katika chanjo ya UVIKO-19 na kusahau chanjo za magonjwa mengine.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo leo Februari 24,2023 kwa nyakati tofauti, wakati akizungumza na wananchi katika mji mdogo wa Usevya na Kata ya Majimoto Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi katika mkutano wa hadhara alipofika kuzindua chanjo na kutoa salamu za pole.

Amesema hali hiyo imeleta madhara kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa surua nchini, na kusababisha vifo vya watoto 13 wilayani Mlele hadi kufikia jana Februari 23, 2023.

“Katika kipindi cha miaka mitatu tumesuasua katika kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa surua katika nchi hii, tumebaini kwamba kuna watoto zaidi ya 400,000 nchini Tanzania hawajapata kabisa chanjo ya dozi ya surua,” amesema.

Amesema hadi sasa ugonjwa wa surua umebainika katika Wilaya 19 za Tanzania bara ambazo ni Nsimbo, Tanganyika, Mpanda, Chunya, Bagamoyo, Kisarawe, Sikonge, Nzega, Tabora Manispaa, Kalambo, Sumbawanga, Sumbawanga Manispaa, Malinyi, Ulanga, Muleba, Korogwe, Mtwara Manispaa na Uvinza ambapo kati ya Wilaya hizo wilaya iliyoathirika zaidi ni Mlele Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi.

Amesema katika halmashauri hiyo kati ya wagonjwa 100 waliopata surua, wagonjwa 45 wametoka katika Kata ya Majimoto.

Katika kuhakikisha watoto wote nchini wanapata chanjo ya ugonjwa huo, Waziri Ummy amesema serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuhakikisha chanjo zinapatikana za kutosha, kutoa kampeni nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano anafikiwa na amewaagiza wakuu wa mikoa nchini kuwatafuta watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano, ambao hawajapata chanjo ya surua kuhakikisha wanapata chanjo.

Amesema kwa mujibu wa sheria ya afya ya jamii endapo mzazi au mlezi atabainika kutompeleka mtoto kupata chanjo anaweza kutozwa faini ya shilingi 100,000 au kifungo cha miezi mitatu gerezani au vyote kwa pamoja.

Katika hatua nyingine, Waziri Ummy ameitaja mikoa 20 ya Tanzania Bara ambayo watoto wengi bado hawajakamilisha dozi ya pili ya chanjo ya ugonjwa wa surua ni Katavi, Tabora, Dar Es Salaam, Arusha, Geita, Rukwa, Shinyanga, Manyara, Tanga, Lindi, Songwe, Mtwara, Iringa, Singida, Ruvuma, Dodoma, Kigoma, Morogoro na Mbeya na kuwataka viongozi kusimamia ipasavyo jambo hilo.

HABARI LEO
Haya Sasa Chaka ni COVID.

Wafadhili watoe pesa ya kampeni.
 
Huu ni utopolo wa Hali ya juu! Yaani mlishiriki kuharibu/kuua Kwa kutokuwajibika kwenye nafasi zenu kisa kukimbilia kukwapua pesa ya COVID 19!! Ni Tanzania pekee utasikia Msaada wa COVID 19 umetumika kwenye miradi na yenyewe inasuasua Kwa mfano madarasana vyoo!Viongozi Hovyo sana! Na mnaendeleaje kuwepo kwenye hizo nafasi.

Kwani kazi ya hii wizara ni Nini? Kwa hizo Hospitali na Zahanati hamuweki data na Kwa hao watoto waliozaliwa hamuwapi wazazi ratiba na kuhakikisha wamewarejesha hao watoto Kwa hizo chanjo?

Na je kama hizo dawa zipo wahusika walikuwa na kazi gani hapo kwenye huduma?!

Na Waziri/Naibu mpo, Ma DR's mpo, Nurses mpo, maabara mpo na mnachukua mshahara! Hoples!!
 
Ni vizuri wamekuwa mbele kulizungumzia suala hili.

Waziri na Wizara yako, mnastahili pongezi.
 
Huu ni utopolo wa Hali ya juu! Yaani mlishiriki kuharibu/kuua Kwa kutokuwajibika kwenye nafasi zenu kisa kukimbilia kukwapua pesa ya COVID 19!! Ni Tanzania pekee utasikia Msaada wa COVID 19 umetumika kwenye miradi na yenyewe inasuasua Kwa mfano madarasana vyoo!Viongozi Hovyo sana! Na mnaendeleaje kuwepo kwenye hizo nafasi.
Kwani kazi ya hii wizara ni Nini? Kwa hizo Hospitali na Zahanati hamuweki data na Kwa hao watoto waliozaliwa hamuwapi wazazi ratiba na kuhakikisha wamewarejesha hao watoto Kwa hizo chanjo?
Na je kama hizo dawa zipo wahusika walikuwa na kazi gani hapo kwenye huduma?!
Na Waziri/Naibu mpo, Ma DR's mpo, Nurses mpo, maabara mpo na mnachukua mshahara! Hoples!!
Umebweka Kama magufuli, vitu ambavyo huvijui.
 
Gharama za chanjo ya homa ya ini kwenye hospital za umma ziangaliwe upya.

Wenzangu na mie zinawakata "stimu" japokuwa ni za kulipa kwa awamu.

Total inafika 60,600/-

Consultation=5000
Kipimo= 10,000
1st Dose=15,200
2nd Dose= 15,200
3rd Dose= 15,200
 
Back
Top Bottom