#COVID19 Hoja za baadhi ya Watanzania kuhusu kukataa chanjo bado ni dhaifu sana

For me, side effect ya chanjo ni kubwa kuliko kuishi bila chanjo.
Tunahitaji kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya corona lkn sio lazima tuwe universal, tuwe unique coz hata hivyo ukichanja bado unauwezekano wa kupata tena usipojikinga.
Mkataa kwao ni mtumwa, lazima tukubali kuheshimu vyakwetu ili tusitumikishwe na vyawenzetu. Kwani tukijifukiza na hali ikawa shwari kuna mtu atakupiga risas kisa umejifukiza?
Ikiwa ni kitaalam bas wataslam wa masuala ya chanjo wakwetu wakae chini sio kutathimini uhali wa hio chanjo ya johnson bali wachukue ujuz hapo watengeneze yakwetu then waitathmini uhalali na usahihi wake kwa watumiaji.
Kqa nini unasema side effect ya chanjo ni kubwa kuliko kutichanja ?
 
Mpaka hapa sijaelewa tunachobishana hasa ni nini ilhali unajua kua ni kawaida kwa kitu kutoaminiwa 100%.
Manake ni kuwa kutiliwa shaka sio kigezo cha kwamba chanjo haifai,yaani yapo mengi yanatiliwa shaka na bado yameonesha kufaa kwake.

Kama chanjo nyingi zilizopita,nyingi tumechomwa utotoni huko lakini zimeleta faida japokuwa propaganda ama mashaka watu walitia.

Hivyo hoja isiwe watu wana mashaka kwa sababu mashaka na hofu ni kawaida,hivyo mashaka isiwe hoja ya kukataa chanjo.
Wengi walio na mashaka na chanjo sio ya kua wameingia lab kufanya testing na izo ishu ka izo, ni kupembua taarifa hii na ile kama ulivyofanya wewe na kuangukia upande huo wao nao kulingana na taarifa wanzaopata/pewa wameangukia upande mwingine.
Chanzo cha kwanza cha taarifa ni kutoka kwa wahusika wenyewe wa jambo.

Serikali ikisema imekopa 1trilion alafu mtu mwingine akasema serikali imekopa 3Trilion kiutaratibu tunatakiwa tuchukue data ya serikali kwa sababu ndio mhusika mkuu,utakaposhikilia data ambazo sio za wahusika itakuwa una lako jambo na sio njia ya kuhakikisha jambo.

Ndio maana mahakamani wanakuwepo wahusika wa tukio kwanza wale ndio wathibitishaji.

Hhivyo hata katika chanjo taarifa za mwanzo unatakiwa uchukue kwa watengenezaji chanjo na sio kwenye kanisa fulani au msikiti fulani au kijiwe fulani,huo hautakuwa utaratibu.
Yote kwa yote ni hiar
Ni hiari kuchanjwa au kutichanjwa,lakini sio hiyari kuoiga vita chanjo maa usiipige vita chanjo.

Hiyari ni katika kukubali kuchanjwa ama kukataa basi na sio hiari ya kitu kingine.
 
Manake ni kuwa kutiliwa shaka sio kigezo cha kwamba chanjo haifai,yaani yapo mengi yanatiliwa shaka na bado yameonesha kufaa kwake.

Kama chanjo nyingi zilizopita,nyingi tumechomwa utotoni huko lakini zimeleta faida japokuwa propaganda ama mashaka watu walitia.

Hivyo hoja isiwe watu wana mashaka kwa sababu mashaka na hofu ni kawaida,hivyo mashaka isiwe hoja ya kukataa chanjo.

Chanzo cha kwanza cha taarifa ni kutoka kwa wahusika wenyewe wa jambo.

Serikali ikisema imekopa 1trilion alafu mtu mwingine akasema serikali imekopa 3Trilion kiutaratibu tunatakiwa tuchukue data ya serikali kwa sababu ndio mhusika mkuu,utakaposhikilia data ambazo sio za wahusika itakuwa una lako jambo na sio njia ya kuhakikisha jambo.

Ndio maana mahakamani wanakuwepo wahusika wa tukio kwanza wale ndio wathibitishaji.

Hhivyo hata katika chanjo taarifa za mwanzo unatakiwa uchukue kwa watengenezaji chanjo na sio kwenye kanisa fulani au msikiti fulani au kijiwe fulani,huo hautakuwa utaratibu.

Ni hiari kuchanjwa au kutichanjwa,lakini sio hiyari kuoiga vita chanjo maa usiipige vita chanjo.

Hiyari ni katika kukubali kuchanjwa ama kukataa basi na sio hiari ya kitu kingine.
Mkuu una maana gani kusema napiga vita chanjo, mbona wanaoitaka wanashawishi watu wakachanje na sio kosa. Na mimi kutoa wasiwasi wangu kuhusu chanjo sio kosa vilevile ni wewe unaesikiliza huku na huku kuamua ni wapi uende.

Narudia kusema ni hiyari, tatizo mtu akitoa mashaka yake mnasema anapinga chanjo. Sio wote ni kina Gwajiboy mkuu, tatizo letu watz tumezoea ubishani ili tushinde na sio kuelimishana.

Yote kwa yote shukran kwa mchango wako mkuu japo una hoja nyepesi. Niliwasikiliza baadhi ya madaktari UFM, wakaeleza kwa urefu na kukata kiu yangu kuhusu chanjo. Sasa ni mimi kuamua tu.
 
Mkuu una maana gani kusema napiga vita chanjo
Kwa sababu unaikataa na unawashawishi wengine waikatae wakati ambapo SERIKALI IMEJIRIDHISHA.

Hii maana yake unapiga vita chhanjo ambayo serikali inaikubali,nadhani neno kupiga vita ndio linakushtua mzee lakini kiuhalisia munaipiga vita chanjo.

Asili ya neno vita ni kuoinga kitu fulani ambaxho wengine wanakitetea.

Vita ya maji maji kuna watu walikuwa wanatetea jambo lao na kuna wengine walikuwa wanapinga.

Hivyo na wewe unaipiga vita chanjo,usibabaike na neno vita.
mbona wanaoitaka wanashawishi watu wakachanje na sio kosa
Ndio kwa sababu serikali imejiridhisha na sisi tunaongozwa na serikali,kama imejiridhisha chanjo salama manake watu wanahamasishwa wakachanje.

Kitendo cha serikali na watu wengine kuhamasisha watu wakachanje hii sio ruhusa ya wewe kueneza uzushi kwa lengo la kupiga vita chanjo.

Kama serikali imetoa ruhusa ama imesema watu walipe kodi kwa atakae,alafu wewe unahamasisha watu wasilipe kodi eti kwa sababu serikali imetoa hiari kwa atakae huo utakuwa ni upigaji vita kodi.

Ikiwa serikali imenunua hizi chanjo alafu kuna watu wanahamasisha tusichanjwe maana yake wanapiga vita serikali wanataka kuitia hasara,huu ni ujinga ambao haupaswi kunyamaziwa.
Na mimi kutoa wasiwasi wangu kuhusu chanjo sio kosa vilevile ni wewe unaesikiliza huku na huku kuamua ni wapi uende.
Anaepaswa kusikilizwa katika mambo ya afya hapa Nchini hasa kwa ishu kama hizi ni wizara ya afya na wataalamu.

Sasa kama anayeongea sio wizara ya afya ni mtu tu kaamua alafu unataka watu wasikilize huku na kule wachambue huku ni kukosa ustaarabu.

Katika ishu kama hizi za chanjo sisi tunapokea taarifa kutoka sehemu moja labda wizara ya afya,hawa ndio wanaopaswa kusikilizwa wanasemaje.

Wananchi heshimuni mamlaka za Nchi yenu,Nchi naiendi kama kigenge kwamba kila mtu asikilizwe tu.
Narudia kusema ni hiyari, tatizo mtu akitoa mashaka yake mnasema anapinga chanjo. Sio wote ni kina Gwajiboy mkuu, tatizo letu watz tumezoea ubishani ili tushinde na sio kuelimishana.
Tunakubaliana ni hiari lakini wapi imesemwa kuwa maana ya hiari ni kutoa mabaya dhidi ya chanjo na kuwashawishi wengine wasichanje ?

Hiari ni wewe kuamua nichanje ama nisichanje,hapo ndipo hiari inaishia.

Suala la kuipinga na kuweka madhara na kuwaambia wengine wasichanje hii sio hiari na hakuna serikali imeruhusu watu wafanye hivi kwa sababu ni upotoshaji.
Yote kwa yote shukran kwa mchango wako mkuu japo una hoja nyepesi.
Hoja nyepesi basi zijibiwe,zivunjevunjwe tuone wepesi wake.
Niliwasikiliza baadhi ya madaktari UFM, wakaeleza kwa urefu na kukata kiu yangu kuhusu chanjo. Sasa ni mimi kuamua tu.
Na kuna wengine waliwasikiliza madaktari sehemu zingine wakawaelewa kuhusu kuchanja kwamba ni salama.
 
Ndugu yangu mbona hujanielewa?? Ngoja basi nikueleweshe ni nini nilimaanisha.
Kwa sababu unaikataa na unawashawishi wengine waikatae wakati ambapo SERIKALI IMEJIRIDHISHA.

Hii maana yake unapiga vita chhanjo ambayo serikali inaikubali,nadhani neno kupiga vita ndio linakushtua mzee lakini kiuhalisia munaipiga vita chanjo.

Asili ya neno vita ni kuoinga kitu fulani ambaxho wengine wanakitetea.

Vita ya maji maji kuna watu walikuwa wanatetea jambo lao na kuna wengine walikuwa wanapinga.

Hivyo na wewe unaipiga vita chanjo,usibabaike na neno vita.
Mkuu ni wapi nimeshawishi wengine waikatae?? Ndio maana nikakwambia sio wote ambao hawatachanja basi ni wamefata ushauri wa Gwajima wengine ni sisi tu tumeamua. Lakini wewe umekazana kusema tunashawishi wengine wasichanje.
We jamaa yaani mimi kusema sichanji ni kua nimeipiga vita chanjo??
Tafuta maana halisi ya kupiga vita mkuu huenda unaielewa vibaya. Kua against na kitu fulani sio kupiga vita, yaani kama mimi ni mkristo na siamini katika mafundisho ya kiislam basi napiga vita uislam?? Mkuu nakushauri tafuta maana ya vita halafu urudi.

Ndio kwa sababu serikali imejiridhisha na sisi tunaongozwa na serikali,kama imejiridhisha chanjo salama manake watu wanahamasishwa wakachanje.

Kitendo cha serikali na watu wengine kuhamasisha watu wakachanje hii sio ruhusa ya wewe kueneza uzushi kwa lengo la kupiga vita chanjo.

Kama serikali imetoa ruhusa ama imesema watu walipe kodi kwa atakae,alafu wewe unahamasisha watu wasilipe kodi eti kwa sababu serikali imetoa hiari kwa atakae huo utakuwa ni upigaji vita kodi.

Ikiwa serikali imenunua hizi chanjo alafu kuna watu wanahamasisha tusichanjwe maana yake wanapiga vita serikali wanataka kuitia hasara,huu ni ujinga ambao haupaswi kunyamaziwa.
Ila hii mifano yako ndgu, kulipa kodi ni lazima na sio hiari sasa sijui mfano wa kodi na chanjo vinaingiliana vipi, usipolipa kodi utashtakiwa kwani usipochanja unashtakiwa?? Tafuta mfano sahihi hapo.

😂😂😂 Umenichekesha hapo mwisho eti wanaitia hasara serikali kisa wamekataa. Sasa si hiari jamani, wangekua hawataki hasara si wangeweka ni lazima. Kwahiyo kisa serikali itapata hasara basi huna uhuru wa kukataa hata kama kitu ni kibaya kwako?? Utu una thamani kuliko pesa wewe, usijirahisishe namna hiyo kisa kuogopa serikali kupata hasara.

Anaepaswa kusikilizwa katika mambo ya afya hapa Nchini hasa kwa ishu kama hizi ni wizara ya afya na wataalamu.

Sasa kama anayeongea sio wizara ya afya ni mtu tu kaamua alafu unataka watu wasikilize huku na kule wachambue huku ni kukosa ustaarabu.

Katika ishu kama hizi za chanjo sisi tunapokea taarifa kutoka sehemu moja labda wizara ya afya,hawa ndio wanaopaswa kusikilizwa wanasemaje.

Wananchi heshimuni mamlaka za Nchi yenu,Nchi naiendi kama kigenge kwamba kila mtu asikilizwe tu.
Ndgu nakushauri ufungue ubongo wako kupokea mambo mapya. Ndio maana humu jf watu huulalamikia sana mfumo wetu wa elimu. Ona sasa yaani wewe utakachoaminishwa unakalili hicho hicho huna haja ya kutafuta maarifa kwingine??

Rejea hata shuleni kulikua na vitabu vya kiada na ziada, ukiwa mtu wa kukalilishwa namna hiyo hatutapeleka nchi popote kwa watu wa namna yako, wavivu wa kutafuta taarifa mbalimbali.
Ngoja nikuulize mkuu vipi kipindi cha mwenda zake ulipiga nyungu?? Na upi ulikua msimamo wako kuhusu chanjo??

Tunakubaliana ni hiari lakini wapi imesemwa kuwa maana ya hiari ni kutoa mabaya dhidi ya chanjo na kuwashawishi wengine wasichanje ?

Hiari ni wewe kuamua nichanje ama nisichanje,hapo ndipo hiari inaishia.

Suala la kuipinga na kuweka madhara na kuwaambia wengine wasichanje hii sio hiari na hakuna serikali imeruhusu watu wafanye hivi kwa sababu ni upotoshaji.
Mkuu ndio maana nakwambia una hoja nyepesi sana, ona kama hapa yaani kisa ni hiari basi mtu haruhusiwi kusema mabaya (kama yapo). Hii ndo maana halisi ya hiari, mtu ajue mabaya na mzuri ili aamue sasa. Lakini wewe serikali imekulazimisha wala huchanji kwa hiari, kwasababu hutaki kusikia kwa wengine, hutaki kusikia mabaya kuhusu chanjo.

We umejifungia tu kwenye mazuri na kuona wenye mtazamo tofauti na wewe wamepotoka. Pole sana mkuu.

Hoja nyepesi basi zijibiwe,zivunjevunjwe tuone wepesi wake.
Nimekupa jibu hapo juu.

Na kuna wengine waliwasikiliza madaktari sehemu zingine wakawaelewa kuhusu kuchanja kwamba ni salama.
Nani aliesema amewasikiliza madaktari na kuona kuchanja si salama🤔🤔??

Rejea usome tena nilichoandika mkuu, ndio maana nikasema wewe unatafuta ligi ili tu ushinde na sio kuelimisha. Mimi niliandika kua niliwasikiliza madaktari na wakakata kiu yangu kuhusu chanjo, hivyo ni mimi tu kuamua. Lakini wewe umeshaconclude kua nimewasikiliza na kua chanjo si salama.

Mkuu tuishie hapa maana naona hata nikikubaliana na wewe bado unachepusha maneno unaendeleza kubishana.
 
Back
Top Bottom