#COVID19 Hoja za Askofu Gwajima zimewaumbua wataalam wetu na waliomuingiza 'mkenge' Rais Samia kwenye chanjo ya Corona

MR TOXIC

Senior Member
Jun 4, 2019
190
525
Nilitegemea wataalam wetu wa afya pamoja na washauri wa Rais waliomshauri kuagiza chanjo ya corona watakuwa mstari wa mbele kujibu hoja za askofu badala yake wamekuwa watu wa kumshambulia yeye binafsi na kumpa vitisho badala ya kujibu hoza zake kitaalam.

Katika hoja ya kwanza, Askofu gwajima ana hoji: Endapo mtu akichanjwa bado ataendelea kuambukiza na kuambukizwa virusi vya corona na kama ndivyo, kuna maana gani ya kuchanja?

Hoja ya pili Askofu anahoji endapo mtu amechanjwa bado atatakiwa kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuvaa barakoa ili kujikinga na maambukizi. Askofu anataka kujua, kama kweli chanjo ya corona ni kinga kwanini mtu aliyechanjwa anatakiwa tena kuvaa barakoa?

Askofu anaendelea kuhoji, mataifa makubwa kama vile marekani yote yana chanjo zao. Kwa mfano, marekani wana chanjo ya jonhson&jonhson na moderna, china wana sinovac, uiongereza wana Astrazeneca, germany wana Pfizer, urusi wana ya kwao, Cuba pia wana ya kwao na mataifa mengine yana chanjo zao. Je ni kwanini haya mataifa yenyewe kwa yenyewe yanaogopana kutumia chanjo ya mwingine?

Gwajima ana hoji kwamba katika kipindi cha zaidi ya miezi sita iliyopita wataalam wetu wanaotaka tupambane na corona kwa njia ya chanjo ndio hawa hawa walisema tusiziamini chanjo kwamba zinaweza kuwa na madhara na kwamba tutumie njia za asili ikiwemo kujifukiza wakajenga hadi banda la kujifukizia pale muhimbili wengine wakafanya mahojiano TBC kuonyesha wasi wasi wao juu ya chanjo ya corona, kwanini leo wamebadilika?

Swali la nyongeza: kwenye fomu ya chanjo ya corona kuna kipengele kinasema serikali haitahusika kwa namna yoyote ile endapo mtu aliyechanjwa atapata maudhi ambayo kwa sasa hayafahamiki. Tunataka wataalam wetu watwambie kama hii chanjo wameifanyia utafiti wa kutosha kwanini wanasema tena kwamba mtu aliyechanjwa anaweza kupata maudhi ambayo hayafahamiki?

Napenda sana wataalam wajibu hoja za gwajima kwa sababu vile wanavyomshambulia badala ya kujibu hoja zake ni kudhihirisha kwamba hawana utaalam wa walichosomea kitu ambacho ni hatari kwa uhai na afya za watanzania.
 
Hakuna wa kuweza kumjibu Gwajima , sababu hzo chanjo ni agenda ya Siri ambayo gwajima yeye mwenyewe anaijua na Raisi anaijua...!! Sema Raisi kabanwa na wala sio maamuz yake hayo ....!!Hana namna , na sote tutachanjwa, itategemea na pressing speed ya wababe wa dunia, so ni Suala la mda tuu..
 
Hata mm sijawahi kupata majibu haya nikaridhika. Tujiulize kama kweli Samia kachanja kwanini anavaa barakoa? Yeye ana tofauti gani na mimi ambaye sijachanja? Kuna umuhimu gani wa chanjo kama utaendelea kuchukua tahadhari zile zile?
 
Hata mm sijawahi kupata majibu haya nikaridhika. Tujiulize kama kweli Samia kachanja kwanini anavaa barakoa? Yeye ana tofauti gani na mimi ambaye sijachanja? Kuna umuhimu gani wa chanjo kama utaendelea kuchukua tahadhari zile zile?
Katika kujiuliza kwenu mnafikiri ile Chanjo ni kwa ajili ya Nini?
 
Msio wataalamu mtoeni humo alimoingizwa, kwani mnasubiri nini?
Anatolewa kwa kushawishiwa na hoja nzito zenye nguvu kama atoazo askofu gwajima .kwahiyo ni wajibu wake kuzipokea na kuzifanyia kazi ama kuendelea kuzipuuza ili siku ya siku tujue nani yupo sahihi
 
Anatolewa kwa kushawishiwa na hoja nzito zenye nguvu kama atoazo askofu gwajima .kwahiyo ni wajibu wake kuzipokea na kuzifanyia kazi ama kuendelea kuzipuuza ili siku ya siku tujue nani yupo sahihi

Uko vizuri:

IMG_20210718_063455_991.jpg
 
Back
Top Bottom