Nimegundua kusifu na kuabudu siyo dili kwa Rais Samia

lord atkin

Senior Member
Sep 30, 2018
197
683
Tofauti na zamani nilivyokuwa nadhani nimekuja kugundua kuwa wanasiasa wa Tanzania nao wanakariri maisha kama vile mwanafunzi wa kidato cha kwanza anavyokariri masomo shuleni. Ni wazi kwamba katika awamu ya tano ili kiongozi ateuliwe au atoke kisiasa ilikuwa ni lazima ama ajipendekeze kwa Rais JPM, ajiunge na kundi la wanasiasa la kusifu na kuabudu. Ilikuwa ukijitokeza na kusifu vizuri utawala kwa ubunifu mkubwa basi baada ya muda utateuliwa.

Baada ya kuingia Mama Samia katika hii awamu ya sita cha kushangaza baadhi ya wanasiasa wameendelea kukariri mambo ya awamu ya tano bila kujali mambo yamebadilika Kuna Rais mpya mwenye maono na vision mpya. Watu hawa bado wanaendelea na kusifu na kuabudu, uchawa na kujipendekeza wakijua kuwa ndiyo njia sahihi ya kumpendeza Rais Samia kama ilivyokuwa kwa mwendazake.

Nilichogundua ni kwamba katika swala hili Rais Samia ni tofauti sana na Mwendazake, yeye si Rais anayependelea sana kupambwa na kusifiwa bila mpangilio. Rais Samia anapenda kiongozi ambaye anajisimamia, mwenye misingi na misimamo yake bila kujali misimamo hiyo inakinzana naye kiasi gani. Katika uteuzi huangalia zaidi uwezo na sifa za mtu zaidi kuliko kujipendekeza kwa mhusika.

Mfano watu kama Humphrey Polepole kwa jinsi alivyokuwa akiukosoa uongozi wa Rais Samia baada ya kuondolewa kwenye uenezi CCM basi ingekuwa ni awamu ya tano asingeliteuliwa kuwa balozi, lakini kwa Mama Samia ni tofauti hakuangalia huyu mtu ananipinga kiasi gani bali aliangalia uwezo na hoja za mhusika akamteua Polepole kuwa balozi.

Mfano mwingine ni Askofu Gwajima kwa Kasi ile aliyoanza nayo ya kupingana na Mama Samia kwenye swala la chanjo ingekuwa awamu ya tano pengine angekuwa ashafukuzwa hata chama. Lakini Mama Samia alihudhuria mkutano wake Jimbo la kawe na kuaddress issue ya chanjo.

Hii ni baadhi ya mifano inayoonesha Mama Samia ni mtu wa namna gani. Kwenu wanasiasa mliokariri siasa za kusifu na kuabudu kama nyenzo ya kufanikiwa kwa Mama Samia hamtatoboa badilikeni. Badala ya mbunge kukaa bungeni na kujipendekeza kwa Rais kutaka picha yake iweke kwenye noti isimamie serikali kwa bidii, wabane mawaziri kwa hoja wasipumue nakuhakikishia utateuliwa kuwa naibu waziri au waziri.

Kitu kingine Mama Samia anacho kipenda ni Demokrasia na uhuru, hivyo kwa wateule wanaotaka kumfurahisha ni vizuri wakacheza kwa madaha wimbo wa uhuru na Demokrasia watafika mbali sana.

Nihitimishe kwa kusema nimependa siasa za Mpina siyo muda mrefu anaula uwaziri.

Wakatabahu
 
SIfa lazima mpaka watu wanasahau kama kuna Mungu wanadiriki kusema kama sio mama mgonjwa asingefika pale!
 

Attachments

  • 20240214_120917.jpg
    20240214_120917.jpg
    95.4 KB · Views: 3
Nchi ngumu sana watu wanafiki, wanajipendekeza, wnatumika


Toka maktaba :
Wafanyabishara wapinga maandamano ya tarehe 24 January 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=zSNJXZrdm3E


TOKA MAKTABA :

WAENDESHA PIKIPIKI BODABODA HATUKO TAYARI KUSHIRIKI KTK SIASA

Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki (Bodaboda) mkoani Mwanza kada Makoye John amesema Jumuiya hiyo inalaani vikali Maandamano yaliyopangwa na vyama vya upinzani kwamba yatafanyika kwenye sehemu mbalimbali nchini januari 24, 2024.


View: https://m.youtube.com/watch?v=B0dB4SmQq2g
 
Back
Top Bottom