Hoja ya kuwahamishia maafisa ushirika katika tume ya maendeleo ya ushirika na maafisa ugani chini ya Wizara ya Kilimo

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
(Chini ya Kanuni za 60(2) na 61 za Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Februari, 2023)

Mheshimiwa Spika, natambua kuwa mwaka 1998, Serikali ilifanya mabadiliko ya Muundo wa Serikali na kufanya uamuzi wa kugatua madaraka (Decentralization by Devolution) kutoka Serikali Kuu a kuyashusha ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji. Uamuzi huo ulikusudia pamoja na mambo mengine, kuboresha na kupeleka huduma kwa wananchi kwa kuwashirikisha katika maamuzi juu ya huduma zinazowahusu. Chimbuko la mabadiliko havo ni Andiko la Kisera (Policy Paper on Local Government Reform) lililoandaliwa mwezi Oktoba, 1998. Mabadiliko hayo yalifanywa kwa nia ya kuboresha na kuongeza ufanisi kwa kupeleka karibu zaidi utaalam na rasilimali kwa kuzingatia matakwa na vipaumbele vya wananchi. Ugatuaji wa Madaraka ulihusisha kupeleka rasilimali fedha na wataalamu wa aina zote katika ngazi za Mikoa na Halmashauri wakiwemo Warajisi Wasaidizi wa Ushirika katika ngazi ya Mkoa na Maafisa Ushirika ngazi ya Wilaya. Aidha, mabadiliko hayo yaliwahusu pia maafisa ugani.

Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa ugatuaji wa madaraka kwa utaratibu uliopo sasa umesababisha Maafisa ushirika waliopo k w e n e Wilaya na maafisa ugani kwa sehemu kubwa kuwa watumishi wanaowaiibika kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika na Ofisi ya Rais TAMISEMI. Aidha, katika ngazi ya Mkoa kuna Mrajis Msaidizi wa Ushirika wa Mkoa ambaye anawasimamia Maafisa Ushirika wa Wilaya waliopo kwenve Halmashauri. Mrajisi Msaidizi wa Mkoa ambaye ni sehemu ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI
Mheshimiwa Spika, Jimbo la Mbozi kama ilivyo kwa maeneo mengi nchini kwa kiasi kikubwa linategemea maendeleo ushirika katika jitihada zake za kuinua kipato cha wananchi na maendeleo ya Jimbo kwa ujumla. Umuhimu huu unatokana na uhalisia kuwa shughuli kuu ya kiuchumi katika maeneo hayo ni kilimo. Sote tunafahamu kilimo cha kahawa, korosho, pamba, katani na mazao mengine ya biashara katika maeneo yote nchini kinategemea sana ushirika ulio imara kupitia vyama vya ushirika vya msingi na vinginevyo.
Mheshimiwa Spika, Tume ya Maendeleo ya Ushirika imeanzishwa chini va Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya 2013 ambapo kwa mujibu wa Sheria hiyo Tume ndiyo yenye wajibu wa kusimamia na kuendeleza ushirika nchini. Muundo wa Tume hii ulipitishwa na Rais mwaka 2015 ambapo Waraisi wasaidizi ngazi ya Mkoa na Maafisa Ushirika ngazi ya Wilaya ni sehemu ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika. Hili linafanyika kwa mujibu wa Kifungu cha 14 cha Sheria. Hata hivyo, watumishi hao waliopo kwenye Ofisi za Katibu Tawala Mkoa na Halmashauri mtawalia, ni waajiriwa wa Ofisi ya Rais TAMISEMI ambao wakuu wao wa kazi na mamlaka zao za nidhamu ni Katibu Tawala wa Mkoa na Wakurugenzi wa Halmashauri.

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Kifungu cha 14(3) cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya 2013, majukumu ya Tume yanayohusu usimamizi na uhamasishaji wa ushirika yanatekelezwa na Tume kupitia Maafisa Ushirika
wa Wilaya. Msingi wake unajengwa kwenye uhalisia kwamba Afisa Ushirika wa Wilaya ndiye msimamizi wa karibu kabisa wa vyama vya ushirika.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 14(2) cha Sheria kinaipa Tume uwezo wa kutoa maelekezo kwa Maafisa hao au kuomba taarifa kutoka kwao kwa mujibu wa Kifungu cha 16 cha Sheria. Hata hivyo, utekelezaji wa sheria hiyo umekuwa na mapungufu na umeonesha ugumu mkubwa katika eneo hilo kwa kuwa Tume haina uthibiti wa moja kwa moja wa watumishi hao na maelekezo ya Tume yasipofuatwa Tume haina mamlaka ya kuweza kuwawajibisha watumishi husika.
UCHUNGUZI ULIOFANYWA NA TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Mheshimiwa Spika, nina taarifa kuwa mwezi Machi, 2023 Tume ya Ushirika ilifanya uchunguzi wa Vyama vya Ushirika 20 kuhusiana na mwenendo wa undeshaji wa Vyama hivyo. Uchunguzi huo ulibaini kuwa kulikuwa na
mapunjo ya bei kwa wakulima kwa zaidi ya Tsh. 74,219,597.07. Kufuatia mapungufu hayo, wakulima walikatwa makato zaidi ya ilivyotakiwa karibu kwa Tsh. 1,700 kwa kilo ya kahawa. Aidha, wakulima wanachama walikatwa fedha Tsh. 116,962,448/= ili kurejesha mikopo ambayo ilikopwa na watu binafsi. Vilevile, Tume ilibaini kuwepo kwa malipo hewa kiasi cha Tsh. 26,932, 147.60 kwa vyama vitano katika Wilaya ya Mbozi pekee.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Maafisa Ushirika wa Wilaya na Mrajis Msaidizi, Tume ilibaini mapungufu makubwa katika utendaïi wao na kuwataka kuimarisha ukaguzi, usimamizi na udhibiti kwa vyama vya ushirika. Katika hatua nyingine, Waziri wa Kilimo alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo Bungeni tarehe 9 Mei, 2023 alieleza kuhusu uchunguzi uliofanywa, matokeo na mapendekezo ya Tume. Hata hivyo, Wizara haijaweza kuchukua hatua za nidhamu kwa sababu za kimuundo. Waziri alitoa maelekezo Bungeni kuwa vyama vya ushirika visikope fedha na Kuwabebesha riba wanachama. Jambo hilo limetokea tena katika maeneo yaleyale na Maafisa Ushirika na Mrajisi Msaidizi wameridhia ukopaji huo licha ya maelekezo ya Mheshimiwa Waziri wa Kilimo.

CHANGAMOTO ZA USHIRIKA ZILIZOBAINISHWA NA TUME

Mheshimiwa Spika, kabla ya uchunguzi uliofanyika katika Vyama vya Ushirika mwaka 2023, mwanzoni mwa mwaka 2022, Tume ya Maendeleo ya Ushirika iliwasilisha mbele ya Mheshimiwa Waziri wa Kilimo changamoto inayopata Tume katika kuwasimamia Maafisa Ushirika wa Wilaya nchini.
Changamoto hizo ambazo zinagusa c h i nzima ni pamoja na:
a) Baadhi ya Halmashauri kuwa na Maafisa ushirika wengi kuliko uhitaji;
b) Baadhi ya Halmashauri kukosa kabisa Maafisa Ushirika;
c) Baadhi ya Maafisa Ushirika kukaa kwenye kituo kimoja kwa muda mrefu;
d) Tume ya Maendeleo ya Ushirika kutokuwa a Mamlaka ya kuajiri, kuwapangia vituo au kuwachukuliwa hatua za kinidhamu;
e) Baadhi ya Maafisa Ushirika waliopo Sekretarieti za Mkoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa kupangiwa majukumu mengine tofauti na ushirika; na
f) •Mamlaka ya uteuzi wa Maafisa Ushirika wa kusimamia Ushirika katika Halmashauri kutokuwa wazi.

MAPENDEKEZO YA KUHAMISHIA MAAFISA USHIRIKA CHINI YA TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA

Mheshimiwa Spika, Tume ilipendekeza kwa Waziri wa Kilimo mbinu za kutatua changamoto hizo. Tume ilipendekeza kuwa:
a) Maafisa Ushirika waliopo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wahamishiwe Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kuwa Mamlaka hizo sasa hazina majukumu ya msingi ya kushughulikia Ushirika na badala yake zibakie na uratibu na uhamasishaji;
b) Kuwe na Afisa Ushirika Mfawidhi katika kila Wilaya ambaye atateuliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika;
c) Tume ipewe kibali cha kuajiri Maafisa Ushirika wa kutosha kufikia kama ya Maafisa Ushirika 662 wanaohitajika; na
d) Tume iendelee kuwa na jukumu la kutoa Miongozo ya namna bora ya usimamizi na uhamasishaji wa Ushirika katika ngazi zote.

USHIRIKA NA UGANI
Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na haja ya kumarisha muunganiko wa shughuli za ugani na shughuli na ushirika pamoja na jitihada nyingine zilizopo katika ngazi ya halmashauri hususan umwagiliaji. Umwagiliaji una maeneo makuu mawili, kwanza eneo yabisi hususani miundombinu ( hardware ) na pili eneo la uenezaji wa kanuni bora za kilimo (Good Agricultural Practices - GAP (Software) ambazo hutolewa na maafisa ugani. Kutounganika kwa maeneo hayo ya umwagiliaji ndiko kunakoleta kuwepo kwa mchango mdogo wa huduma za ugani katika uchumi na usalama wa chakula.

MAPENDEKEZO YA KUHAMISHIA MAAFISA USHIRIKA KWENDA TUME YA USHIRIKA NA MAAFISA UGANI KWENDA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI KUTODHOOFISHA UTEKELEZAJI WA UGATUAJI WA MADARAKA
Mheshimiwa Spika, Marekebisho ya Sheria yanayopendekezwa yatasababisha maafisa ushirika waliopo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhamishiwa katika Tume ya Maendeleo ya Ushirika. Kama nilivyoeleza awali Mamlaka za Serikali za Mitaa ziondolewe majukumu ya msingi ya kushughulikia Ushirika na badala yake zibaki na uratibu na uhamasishaji. Marekebisho hayo, yanalenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa
ugatuaji madaraka na sio kudhoofisha, kwani hatua hiyo itaimarisha mifumo va kufikisha huduma kwa wakulima wote nchini na kuboresha utendaji wa maafisa ushirika.
Huduma za umwagiliaji na huduma za ugani hutolewa na wataalam wa kilimo wenye taaluma za agronomia, kilimo mseto, mazao ya bustani (horticulture), uchumi kilimo, uhandisi kilimo, fundi sanifu kilimo, afya ya mimea, uhandisi umwagiliaji, fundi sanifu umwagiliaji, fundi sanifu usimamizi na mipango ya matumizi ya ardhi ya kilimo, uchumi wa nyumbani na sayansi ya chakula, ugani na huduma za jamii. Mabadiliko yanayopendekezwa yataimarisha muunganiko wa shughuli za umwagiliaji na huduma za ugani kwa kuwa hayo ni masuala yanayotegemeana katika kuwezesha kilimo chenye tija. Kwa mantiki hiyo, utekelezaji wa shughuli za uzalishaji mazao hususan kupitia huduma za ugani unahitaji kutumia taaluma mbalimbali zinazoratibiwa kwa pamoja ili kuongeza uzalishaji na tija. Uratibu huo utafanyika vizuri zaidi ikiwa mageuzi ya uboreshaji wa hudma za ugani na maendeleo ya umwagiliaji unaratibia na taasisi moja ambayo kwa muhtadha huu ni Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa suala kama hili linalopendekezwa limewahi kujitokeza kwenye sekta ya Ardhi, Barabara na Maji. Serikali ilichukua hatua ambazo zimeonesha kuzaa matunda. Mamlaka ya uwajibikaji kwa Maafisa katika Idara ya ardhi ya Halmashauri valihamia kwenye Wizara ya Ardhi na kumpa Waziri wa Ardhi na Katibu Mkuu katika Wizara ya Ardhi fursa ya kuwapangia vituo, kuwahamisha, na kuwawajibisha kinidhamu Maafisa waliopo kwenye Halmashauri.

Maafisa hao wameendelea kuwa na vyeo vilevile, majukumu yaleyale, kutumia majengo yaleyale a vitendea kazi vya Halmashauri zao isipokuwa sasa Waziri na Katibu Mkuu wa sekta wanaweza kuwafikia na kuwahoji juu
ya utendaji wao. Hali hi inasaidia kuleta ufanisi kwani Wizara ya kisekta inafahamu kuhusu taaluma yao, majukumu yao na sera zilizopo kwenve eneo hilo vyema zaidi kiasi cha kutambua utendaji unaofaa na usiofaa wa Maafisa wake.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa B a r b a r a a Maji zilianzishwa Wakala zinazojitegemea za TARURA na RUWASA mtawalia ili kuimarisha ufanisi na kuweka mtiririko mmoja wa maelekezo kwa Wataalamu. RUWASA
ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5 ya Mwaka 2019. Katika utendaji kazi, RUWASA imefungua Ofisi katika ngazi ya Mkoa na Wilaya zinazoongozwa na Meneja wa Mkoa na Wilaya ambao wanawajibika kutoa taarifa za kiutendaji kwene vikao mbalimbali; ikiwemo Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC). Aidha, wanawajibika kuwasilisha mipango na taarifa za utekelezaji katika Baraza la Madiwani kwa taarifa. Taasisi hiyo hushiriki katika vikao na shughuli mbalimbali za halmashauri kwa mwaliko maalum kutoka Mkurugenzi Mtendaji. Muundo huo umeboresha ugatuaji wa madaraka na kuimarisha utekelezaji wa utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wa Ushirika ipo Tume ya Maendeleo ya Ushirika ambayo inasimamia ushirika na kwa mujibu wa muundo wao ni mabadiliko machache tu yanahitajika kuweza kupata mtiririko wa usimamizi unaotarajiwa na unaofaa hususan kuiwezesha Tume kuwasimamia maafisa ushirika w o e na kuwa muunganiko katika uratibu kuanzia ngazi ya taifa hadi halmashauri.

Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo hayo, naomba kutoa hoja kama ifuatavyo;
KWAKUWA, Maafisa Ushirika ni kiungo muhimu katika kuendeleza kilimo cha mazao ya biashara kwa kuvisimamia vyama vya ushirika chini na pia maafisa ugani ni kiungo muhimu katika utoaji wa maarifa na kueneza teknolojia na Kanuni Bora za Kilimo kwa wakulima umwagiliaji; katika skimu za

NA KWAKUWA, katika utekelezaji wa majukumu yao maafisa ushirika wanapata wakati mgumu wa kutekeleza maelekezo ya Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika na maelekezo ya Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa wengine wa Ofisi ya Rais TAMISEMI:

NA KWAKUWA, Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Maendeleo a Ushirika ndio wasimamizi wa ushirika na wanashindwa kuwasimamia kikamilifu Maafisa Ushirika wa Wilaya hivyo kusababisha kulegalega kwa ushirika katika maeneo mengi nchini;

KWAHIYO BASI Bunge lako tukufu linaazimia kwamba Serikali ibadili mfumo uliopo sasa na kuwafanya Maafisa Ushirika wa Wilaya na maafisa ugani waliopo kwenye Halmashauri zote chini kuajiriwa, kusimamiwa na kuwajibika kwenye Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Tume ya Umwagiliaji mtawalia.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
 

Attachments

  • Hoja Binafsi ya Mhe. George R. Mwenisongole.pdf
    4.7 MB · Views: 4
Hii hoja enzi za magufuli ilishika kasi sana, na maelekezo yalikuwa yashatolewa kwenye LGAs. Ilivyokufa hata haijulikani.
 
Back
Top Bottom